Hivi utajuaje Kama Mungu ndo Kakupa Huyo?

Khan

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,241
2,000
Kuna kamsemo watu wanakasema kwamba Mungu atakupa wa kufanana naye

watu wengi wameoa either kwa kuamini huyo aliyenaye anafanana nae au labda kuoa/kuolewa kwa basi tu.

Je sisi ambao hatujaoa/kuolewa utajuaje kwamba huyo ndo Mungu Kakupangia?
ikumbukwe kuna wakati una fall in Love mpaka unahisi ulienae Mungu ndo kakuumbia lakini baadaye mnaeza kutengana!

Je sasa utatambuaje kama Huyo uliyenaye ni chaguo la Mungu Je?

Na Je kama sio utajuaje wako uliyepangiwa na Mungu ni flani je?

Na Je utajuaje kama mtu fulani ni soul mate wako je?

Na Je tutanye nini ili ujue Chaguo la Mungu Kwako Je?
 
nyaggad

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,154
2,000
Mkuu,mbona ni rahisi sana kumjua mwenza wako kama amefanana na wwe kitabia,kama wewe ni malaya ukimpata Malaya mwenzako huyo ndio umefanana nae,kama wewe ni mcha mungu na mwaminifu utampata mcha Mungu mwenzako huyo ndio umefanana nae,usitegemee kumpata Mwenza kama malaika na wakati wewe upo kama shetani!
 
Jiwedogo

JF-Expert Member
May 23, 2017
2,820

Kuna wakati hatujui tunapomuomba Mungu kuhusu WENZI wa maisha (mke ama mume)... Anapojibu huwa hatuelewi... Hatuielewi lugha yake ajibuye...
Kunaa baadhi ya mambo ambayo nina yaamini kwa uhakika...

1. Mungu huwa hadanganyi, aliposema atakupa wa kufanana nae, hii huwa halibadiliki.

2. Mungu huangalia kusudi aliloliweka ndani yako kwamba lazima litimie, SASA, lazima akupe mtu atakayekusaidia kulifikia kusudi aliloliweka kwako, maana ni la kwake sio la kwako... Hivyo nimuhimu akupe aliyekusudia yeye.

Sasa upo wakati huwa sisi tunaamua kuwa na wale wasio elekea kwenye kusudi la Mungu... Ikitokea hivyo;
Mungu anaamua kuingilia kati... Akiingilia kati, yatatokea mambo kadhaa;

1. Uliyeamua kujitwalia ataondoka kwako.

2. Namna ya kuondoka hupanga Mungu kulingana na ugumu wa wewe kutokumuelewa alipokuambia kuwa huyu sio wako , sio atakayefanikisha kusudi lake kupitia wewe.

Ataondokaje, haijalishi atakapoondoka utaumia ama utafurahi, lazima aondoke...
anaweza kwenda kwa aliye wa kwake, sasa haijalishi atakuwa ni wa karibu yako ama usiyemjua ...
Wakati mwingine anaweza hata akafa, ndio... Maana pengine Mungu alijua utashupaza shingo , na yeye anajukumu na wewe zito mnoo.

Sasa inapotokea uliyedhani ni wako anaondoka kwako, na wewe ulikuwa unaomba Mungu, elewa kwamba ndio majibu ya ulichoomba (ingawa kwa baadhi ya mambo yafaa kumsikiliza vyema Mungu uliyemwomba, kuna saa unaweza jibiwa na usiyemuomba)
 
Khan

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,241
2,000
Mkuu,mbona ni rahisi sana kumjua mwenza wako kama amefanana na wwe kitabia,kama wewe ni malaya ukimpata Malaya mwenzako huyo ndio umefanana nae,kama wewe ni mcha mungu na mwaminifu utampata mcha Mungu mwenzako huyo ndio umefanana nae,usitegemee kumpata Mwenza kama malaika na wakati wewe upo kama shetani!
Very False
 
Jiwedogo

JF-Expert Member
May 23, 2017
2,820
2,000
Kuna kamsemo watu wanakasema kwamba Mungu atakupa wa kufanana naye

watu wengi wameoa either kwa kuamini huyo aliyenaye anafanana nae au labda kuoa/kuolewa kwa basi tu.

Je sisi ambao hatujaoa/kuolewa utajuaje kwamba huyo ndo Mungu Kakupangia?
ikumbukwe kuna wakati una fall in Love mpaka unahisi ulienae Mungu ndo kakuumbia lakini baadaye mnaeza kutengana!

Je sasa utatambuaje kama Huyo uliyenaye ni chaguo la Mungu Je?

Na Je kama sio utajuaje wako uliyepangiwa na Mungu ni flani je?

Na Je utajuaje kama mtu fulani ni soul mate wako je?

Na Je tutanye nini ili ujue Chaguo la Mungu Kwako Je?
1. Mtegemee na umtangulize Mungu kwa kila hatua ktk jambo hili. Mungu hamtupi kamwe mtu anayemtegemea yeye. Kwa kuwa unamtegemea Mungu, basi, utaomba kwa ajili ya kutaka mwongozo wa Mungu ktk jambo hili. Mungu atakachofanya ni kuuelekeza moyo wako umuelekee mtu aliyekusudia awe mwenzi wako wa ndoa maisha yako yote. Mungu husema nasi kupitia mioyo yetu. Huweka nia na mawazo, au hali ya upendo mioyoni mwetu ktk yale makusudi yake tuliyomuomba. Kwa hiyo ukimtegenea ukamwomba atafanya hivyo.

2. Usiwe na haraka ya maisha {ya ndoa}, kuwa mtulivu na ukubali kusubiri.
Mtu mwenye haraka ya maisha hutapatapa kwa kutaka mafanikio ya haraka, hawezi kusubiri na kwa sababu hiyo ataangukia ktk mtego wa shetani. Maombi yatafanya kazi iwapo hutakuwa na haraka. Mara nyingi wa kwanza kukujibu maombi yako huwa ni shetani ili aharibu mpango na kusudi la Mungu ktk maisha yako. Kama utakuwa na haraka ya ndoa shetani atakupa mume au mke ili aharibu maisha yako. Kwa hiyo ni vyema kuwa muangalifu sana. Kubali kusubiri hata kama unaona umechelewa. Uhakika wa safari sio kuwahi kufika bali ni usalama wa safari. Haraka inaweza kusababisha ajali njiani hatimaye ukafa na usifike mwisho wa safari yako.

3. Tumia Akili yako Vizuri.
Mungu amekataza kuzitegemea akili zetu lkn ameamuru kuzitumia akili zetu kwa jinsi ipasavyo. Kwa hiyo tumia akili yako kufanya hukumu {judgement} ili kupambanua mwema na mbaya. Hata kama unaasilimia 100 kuwa huyo anayetaka au unayemtaka kuwa mwenzi wako anatoka kwa Mungu bado tumia akili yako kabla, wakati, na baada ya kufanya maamuzi.
Chunguza familia yao na ukoo anaotoka, hapa huitaji maombi, unahitaji akili.
Chunguza tabia yake, tafuta kujua mahusiano yake na jamii inayomzunguka.
Tabia ni muhimu kuliko vitu alivyonavyo, hautaishi naye kwa sababu ya mali, elimu au uzuri alionao, utaishi naye kwa sababu ya tabia njema aliyonayo.
Usiwe mvivu wa kufikiri, usiwe mvivu wa kutumia akili yako kupambanua mambo.

4. Upendo wake kwako. Si kila anayekuja kukuchumbia anakupenda, na wala si kila anayekukubali umuoe anakupenda. Kwa hiyo ni vyema kuhakikisha upendo wake kwake.
Upendo si vitu anavyokupa upendo ni namna yeye anavyojitoa kwako si kwa manufaa na faida yake, bali kwa faida yako. Upendo ni nia yake juu yako, haujajengwa ktk vitu au mali alizonazo mtu, umejengwa ktk utu wa mtu ktk hali yoyote. Muda tu ndio kipimo cha upendo.
Pia anayetaka tendo la ndoa kabla ya ndoa hakupendi. Anayekupenda atakulinda.

5. Utayari wake kwako. Ukiona mtu amekuchumbia halafu hayuko tayari kukuoa huyo si wako, anatafuta kukuharibia. Ukiona umemchumbia mtu halafu hayuko tayari kuolewa na wewe, hakupendi ila kuna kitu anatafuta. Lkn ukichumbiwa au kuchumbia mtu asiyekuwa tayari kuweka bayana mahusiano yenu kwa wazazi wa pande mbili au kwa viongozi wenu wa dini, au walezi wenu jua kabisa umeliwa. Haiwezekani muwe kwenye mahusiano miaka miwili, hata mmoja hakuna anayefahamu tena hata bila sababu za msingi.
 
Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,309
2,000
Matendo huwa hayadanganyi,

Ila kuwa watu wanajua Sana kupretend, kuwa makini katika jambo
 
God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,822
2,000
Mkuu hivi ushapata mke?

Ok kwako mtoa mada.
Kwanza uliwahi kusema huku ww ni freemason! basi huwezi pata hiyo neema labda huyo freemason unaemtukuza akupe.

Pili kwa watu wa Mungu tuu ndio wenye uwezo wa kupata hiyo neema! Unapaswa uwe mtu wa imani ndipo ufunguliwe! vinginevyo utatangatanga ndugu yangu bila mafanikio.

Ni lazima utumie akili aliyokujalia mwenyezi Mungu kufanya mambo yako ila sasa kuna mambo mengine ni magumu mno kwa akili ya kawaida huwezi kuyatambua... hivyo basi unahitaji msaada wa Mungu.

Chakufanya ndugu yangu naomba uachane na huo mtandao wa shetani halafu uokoke. Ukihitaji msaada zaidi nipe namba yako pm nikusaidie kwa hali na mali kwani uwezo upo.

Halafu nyinyi waabudu mapepo mnapata faida gani? mnafurahia kuishi bila mahusiano? au tamaa za ulimwengu? mnafurahia kutoa roho za watu? mmesikia yaliyowakumba wenzenu kwenye huo mtandao wale waliokosea masharti? kwa uweza wa Mungu naomba awaepushe na shetani.
 
ibraton

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
347
250
Kuna kamsemo watu wanakasema kwamba Mungu atakupa wa kufanana naye

watu wengi wameoa either kwa kuamini huyo aliyenaye anafanana nae au labda kuoa/kuolewa kwa basi tu.

Je sisi ambao hatujaoa/kuolewa utajuaje kwamba huyo ndo Mungu Kakupangia?
ikumbukwe kuna wakati una fall in Love mpaka unahisi ulienae Mungu ndo kakuumbia lakini baadaye mnaeza kutengana!

Je sasa utatambuaje kama Huyo uliyenaye ni chaguo la Mungu Je?

Na Je kama sio utajuaje wako uliyepangiwa na Mungu ni flani je?

Na Je utajuaje kama mtu fulani ni soul mate wako je?

Na Je tutanye nini ili ujue Chaguo la Mungu Kwako Je?
bnadam wanapenda kila kitu kumsingizia mungu....huku tunachaguana wenyewe mungu kazi yake ilikua kuumba tu mzuri na mmbaya
 
Binti Christ

New Member
Jul 7, 2019
1
20
1. Mtegemee na umtangulize Mungu kwa kila hatua ktk jambo hili. Mungu hamtupi kamwe mtu anayemtegemea yeye. Kwa kuwa unamtegemea Mungu, basi, utaomba kwa ajili ya kutaka mwongozo wa Mungu ktk jambo hili. Mungu atakachofanya ni kuuelekeza moyo wako umuelekee mtu aliyekusudia awe mwenzi wako wa ndoa maisha yako yote. Mungu husema nasi kupitia mioyo yetu. Huweka nia na mawazo, au hali ya upendo mioyoni mwetu ktk yale makusudi yake tuliyomuomba. Kwa hiyo ukimtegenea ukamwomba atafanya hivyo.

2. Usiwe na haraka ya maisha {ya ndoa}, kuwa mtulivu na ukubali kusubiri.
Mtu mwenye haraka ya maisha hutapatapa kwa kutaka mafanikio ya haraka, hawezi kusubiri na kwa sababu hiyo ataangukia ktk mtego wa shetani. Maombi yatafanya kazi iwapo hutakuwa na haraka. Mara nyingi wa kwanza kukujibu maombi yako huwa ni shetani ili aharibu mpango na kusudi la Mungu ktk maisha yako. Kama utakuwa na haraka ya ndoa shetani atakupa mume au mke ili aharibu maisha yako. Kwa hiyo ni vyema kuwa muangalifu sana. Kubali kusubiri hata kama unaona umechelewa. Uhakika wa safari sio kuwahi kufika bali ni usalama wa safari. Haraka inaweza kusababisha ajali njiani hatimaye ukafa na usifike mwisho wa safari yako.

3. Tumia Akili yako Vizuri.
Mungu amekataza kuzitegemea akili zetu lkn ameamuru kuzitumia akili zetu kwa jinsi ipasavyo. Kwa hiyo tumia akili yako kufanya hukumu {judgement} ili kupambanua mwema na mbaya. Hata kama unaasilimia 100 kuwa huyo anayetaka au unayemtaka kuwa mwenzi wako anatoka kwa Mungu bado tumia akili yako kabla, wakati, na baada ya kufanya maamuzi.
Chunguza familia yao na ukoo anaotoka, hapa huitaji maombi, unahitaji akili.
Chunguza tabia yake, tafuta kujua mahusiano yake na jamii inayomzunguka.
Tabia ni muhimu kuliko vitu alivyonavyo, hautaishi naye kwa sababu ya mali, elimu au uzuri alionao, utaishi naye kwa sababu ya tabia njema aliyonayo.
Usiwe mvivu wa kufikiri, usiwe mvivu wa kutumia akili yako kupambanua mambo.

4. Upendo wake kwako. Si kila anayekuja kukuchumbia anakupenda, na wala si kila anayekukubali umuoe anakupenda. Kwa hiyo ni vyema kuhakikisha upendo wake kwake.
Upendo si vitu anavyokupa upendo ni namna yeye anavyojitoa kwako si kwa manufaa na faida yake, bali kwa faida yako. Upendo ni nia yake juu yako, haujajengwa ktk vitu au mali alizonazo mtu, umejengwa ktk utu wa mtu ktk hali yoyote. Muda tu ndio kipimo cha upendo.
Pia anayetaka tendo la ndoa kabla ya ndoa hakupendi. Anayekupenda atakulinda.

5. Utayari wake kwako. Ukiona mtu amekuchumbia halafu hayuko tayari kukuoa huyo si wako, anatafuta kukuharibia. Ukiona umemchumbia mtu halafu hayuko tayari kuolewa na wewe, hakupendi ila kuna kitu anatafuta. Lkn ukichumbiwa au kuchumbia mtu asiyekuwa tayari kuweka bayana mahusiano yenu kwa wazazi wa pande mbili au kwa viongozi wenu wa dini, au walezi wenu jua kabisa umeliwa. Haiwezekani muwe kwenye mahusiano miaka miwili, hata mmoja hakuna anayefahamu tena hata bila sababu za msingi.
Its true umeongea points tupu,.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom