Hivi utajisikiaje mbunge umehamia CCM halafu unaenda kukataliwa na wanaccm kwenye kura za maoni? Angalizo: mtatukanwa sana na wapinzani wenu chamani!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Mbunge umehamia CCM tena unawatukana waliokupa ridhaa ya chama kugombea. Unatukana sana huku unajisahau kuwa unaenda kugombea ubunge kwa tiketi ya chama ambacho umehamia juzi. Chama ambacho unaenda kukutana na magwiji ha propaganda chafu yaliyojipanga tangia 2016.

Nawaambieni mtapata tabu sana. Kwanza mtatukanwa matusi haya haya mnayotukana sasa! Mtachambwa na mwisho hamtapita hata mmoja wenu kwenye kura za maoni.

Mnajisahau sana, mnapata kiburi sana ila muda utaongea. Nyie ni mazuzu yasiyoona mbele na kwa hakika mtakuja kujikuta mnamlalamikia tena huyu huyu anayewaita kwake ila kwa wakati huo hakuna wa kuwasikilizeni maana kila mtu atakuwa anapambana na hali yake. Kwa sasa nyie jitoeni ufahamu vya kutosha kabisa!

Na ikiwa kamati kuu itajifanya ubabe na kuwapa ugombea kinguvu basi yatakayofuatia yatafurahisha sana.

Nimwambie tu Rais Magufuli kuwa anachokijenga sasa na kwa miaka minne iliyopita ndicho atakachokiona kwenye uchaguzi mkuu na kuanzia mwaka 2021. Hapo ndipo atajua kuwa kumbe ubabe si kitu chochote mbele ya siasa! Tukutane ulingoni palipojaa umamluki, fitina, uchawi, uuwaji na kila aina ya takataka linalojulikana.

Ulingoni si mbali kutoka sasa.
 
Hakuna shida!

Najua mnaumia roho sana enyi wafuasi wa mwamba tuvushe.

Hawa watatumika kuanika uozo uliomo chadema maana wametoka humo ghafla sana kabla hamjajiandaa kuwatenga.

Hivyo sio lazima wapewe ubunge, kuna teuzi nyingi sana za kitaaluma na kisiasa pia, so kila mmoja atawekwa anapo fit.

Tunaingia kwenye mechi kwanza,point zikishapatikana ndio tunajipanga kazi kwenu na konyagi.
 
Kuna mtu anayejua uozo wa Chadema kuliko Slaa? Mbona hakuweza kuutoa mwaka 2015 hadi ukubalike kwa watanzania achilia mbali kupewa airtime ya masaa mawili ndani ya radio na TV zote nchini akiizungumzia Chadema pale Serena hotel?

Unategemea Lijualikali aje au Silinde aje na lipi la ziada?
 
Mbunge umehamia CCM tena unawatukana waliokupa ridhaa ya chama kugombea. Unatukana sana huku unajisahau kuwa unaenda kugombea ubunge kwa tiketi ya chama ambacho umehamia juzi, mtapata tabu
Mkuu G Sam, wahamiaji hawatapata taabu kwasababu CCM imebadili utaratibu, unaanza uteuzi kwanza wa majina matatu ndio yanakwenda kupigiwa kura.
Hivyo wale wanaotakiwa, watabebwa.
P
 
Kwenye hayo hayo majina matatu hawatapita kwa wapiga kura mkuu. Labda majina yote matatu yawe ya wahamiaji haramu jambo ambalo litaipasua pasua CCM kila kona.
 
Hakuna shida!

Najua mnaumia roho sana enyi wafuasi wa mwamba tuvushe.

Hawa watatumika kuanika uozo uliomo chadema maana wametoka humo ghafla sana kabla hamjajiandaa kuwatenga.

Hivyo sio lazima wapewe ubunge, kuna teuzi nyingi sana za kitaaluma na kisiasa pia, so kila mmoja atawekwa anapo fit.

Tunaingia kwenye mechi kwanza,point zikishapatikana ndio tunajipanga kazi kwenu na konyagi.
Hizo nafasi zingine zote zimejaa na hao ataowatoa nao atawapeleka wapi ili hali walihama upinzani ili maisha yaendelee kupitia CCM na serikali yake?

Mjiandae kwa uasi wa chini chini kutoka kwa wale wataonyang'anywa au kukosa tonge kinyume na makubaliano yenu.
 
Mbunge umehamia CCM tena unawatukana waliokupa ridhaa ya chama kugombea. Unatukana sana huku unajisahau kuwa unaenda kugombea ubunge kwa tiketi ya chama ambacho umehamia juzi. Chama ambacho unaenda kukutana na magwiji ha propaganda chafu yaliyojipanga tangia 2016.

Nawaambieni mtapata tabu sana. Kwanza mtatukanwa matusi haya haya mnayotukana sasa! Mtachambwa na mwisho hamtapita hata mmoja wenu kwenye kura za maoni.

Mnajisahau sana, mnapata kiburi sana ila muda utaongea. Nyie ni mazuzu yasiyoona mbele na kwa hakika mtakuja kujikuta mnamlalamikia tena huyu huyu anayewaita kwake ila kwa wakati huo hakuna wa kuwasikilizeni maana kila mtu atakuwa anapambana na hali yake. Kwa sasa nyie jitoeni ufahamu vya kutosha kabisa!

Na ikiwa kamati kuu itajifanya ubabe na kuwapa ugombea kinguvu basi yatakayofuatia yatafurahisha sana.

Nimwambie tu Rais Magufuli kuwa anachokijenga sasa na kwa miaka minne iliyopita ndicho atakachokiona kwenye uchaguzi mkuu na kuanzia mwaka 2021. Hapo ndipo atajua kuwa kumbe ubabe si kitu chochote mbele ya siasa! Tukutane ulingoni palipojaa umamluki, fitina, uchawi, uuwaji na kila aina ya takataka linalojulikana.

Ulingoni si mbali kutoka sasa.
Kuna kale kabwana mdogo ka kilombero, kwanza kana shule ya wasiwasi pili kanadai kaliiba kura, sijaona takukuru au DCI akihangaika nako, tusubiri mtiti wa kura za maoni
 
Back
Top Bottom