Elections 2010 Hivi ushindi ni idadi ya kura au majimbo

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,491
7,505
nashindwa kuwaelewa waandishi wetu wa habari, utasikia jk anaongoza majimbo, kwani kinachoamua ushindi ni majibo au idadi ya kura, je angekuwa ameshindwa kwa idadi ya majimbo lakini anaongoza kwa kura wangeripoti vipi? nadhani wanajaribu kucheza na akili( psychology) za watu na si vizuri wanavyofanya.
 
Ndio maana mkapa alisema tanzania hamna waandishi alikuwa anamaanisha upuuzi kama huu wanaoripoti, eti lipumba anashika nafasi ya pili kwa majimbi aliyoshinda majimbo yenyewe ya pemba ambayo wapiga kura wake hata hawafikii wapiga kura wa Ubungo
 
Mimi naomba mnisaidie, hivi hadi sasa chadema wameshinda majimbo mangapi? Naona magazeti yananichanganya.
 
NEC wenyewe wachovu, hata kutoa summaries za matokeo ya ubunge na Urais kwenye tovuti yao hamna.
 
Labda tusubiri watatoa kwa wakati wao! Nimesearch sana sipati matokeo ya uhakika! Wanaojua watatusaidia. Asante Mwanamayu kwa response yako!
 
Kilichokuwa kinafanyika ni Propoganda ilikusudi kuwakatisha tamaa watu waliokuwa wanaisapoti Chadema ili wasifuatilie results za urais kwakuaminishwa Slaa amezidiwa hata na Lipumba,huu mkakati umefanyika kwakutumia itv na tbc nakwakufanya ivyo wamefanikiwa sana kuchakachua kura za Slaa.Rais wa Tanzania anapatikana kwa wingi wa kura hata kama atazidi kwa kura1.
 
Back
Top Bottom