Hivi Urais wa Taifa la Tanzania ni Mali ya Watanzania au Kikundi cha watu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Urais wa Taifa la Tanzania ni Mali ya Watanzania au Kikundi cha watu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Nov 4, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  WanajF nimeleta thread hii baada ya kukosa majibu kuwa taasisi ya Urais [Presidential Power] je ni mali ya Watanzania au ni mali ya kajikundi ka watu?Kwanini nasema hivyo kwa kuwa humu ndani ya Jamiiforum kumekuwa kila kukicha kuna thread nyingi zinazolenga kuonyesha kuwa Rais ajae anatokana na aina ya kundi fulani au mlengo fulani [tena kwa majina] na si kutokana na Wananchi wa Tanzania.

  Imefikia Rais anawaambia mawaziri wake kuwa anasikia mitaani wanautaka Urais hivyo wachape kazi.Hakika sipati picha kuwa Rais ndiye msimamizi mkuu wa Serikali na shughuri zote za kulinda Mali na Maisha ya Wananchi wa Taifa hili.Leo iweje kuwa Rais anakuwa ni mteule wa kutwajwa na kakikundi au kundi fulani la watu.Leo kuna thread kuwa Rais ajae ni Mwanamke.Hivi inakuwaje haya mambo ya utaasisi wa taasisi Nyeti kama hiyo kuwa na picha ambayo siyo imara [stable ] ngumu kuelezeka midomoni mwa watu kwa kuwa ni taasisi yenye kubeba uhai na maisha ya Wananchi.

  Ndio maana Baba wa Taifa alisema IKULU ni mahala PATAKATIFU,na kuwa shida nyingi na mahangaiko ya watu vijijini na mijini ni mzigo wa Rais,kutafuta majibu ya kuepusha watu wake na maisha ya shida.

  Lakini leo hii taasisi ya Urais tumeithaminisha kama taasisi au NGO ya mtu binafsi au shirika kwamba fulani ndio CEO,Mwenyekiti, Manager au Director mtarajiwa.Hivi ile nguvu ya kitaasisi kwa taswira [Institutional Ethics and Morals image] imepotelea wapi mpaka tunapaka rangi ya picha /taswira kuwa Rais ajae ni fulani, jina lake ni fulani, mwanamke, mwanamme, mwislamu au mkristu, au ni wa jinsia gani, na tena tumepoteza uwezo wa kutamka sifa za Rais ajae na hatuna taswira ya kutamka Rais ajae kuwa ni mwenye haiba au sura hii-

  MUUMINI ANAEFAHAMU KUWA KUNA MUNGU [KWA KUTEGEMEA IMANI YA DINI YAKE].
  1: Mjamaa
  2: Mzalendo
  3: Mwadilifu
  4: Anawajibika
  5: Hana dharau wala Visasi
  6: Mtetezi wa Watanzania wote wenye kutafuta Maisha halali [wawe ni Matajiri,Watu wa Kati na Wenye Hali duni] sina msamiati wa Mtu Masikini
  7: Mpiganaji wa Vita ya Rushwa, Ufisadi, Uzembe, Unafiki, Uongo
  8: Msikivu
  9: Mvumilivu kwa wale wanaotofautina na yeye kwenye ujenzi wa Taifa.
  10: Asiyekubali Kuyumbishwa
  12: Mkorofi kwa wahujumu na wenye nia Mbaya na Taifa na watu wake
  13: Msomi mwenye uelewa wa dunia Mpya ya Ulimwengu wa Sasa wa Digital Generation Technology
  14: Mpenda Maadili na Utamaduni wa Kiafrika na Ya Kitanzania
  15: Mpenda Maendeleo tena ikibidi kwa viboko sawa.
  16: Mbunifu,mwenye kujua mbinu na mahitaji ya vizazi,kama uanzishwaji wa taasisi zenye kwendana na mahitaji ya wakati husika.
  17: Asie Mwoga na Mbishi yaani aambiliki
  18: Muongozaji kwa Vitendo,kusikia Rais leo atashinda shambani na Wananchi wa Kijiji fulani isiwe shida wala ajabu.
  19: Mpenda Mabadiliko kwa kasi na welevu wa umakini kwa faida ya Taifa.
  20: Asiye lala kwa kuwazia atalifanyia nini Taifa lake,na kuwapa moyo huo huo wananchi wake,na kila wakimuona wanaona wanajukumu sawa na lake la kulifanyia nini Taifa.Na sio Wananchi watamfanyia nini yeye.
  21: Mwenye Kupenda jamii yake kwa kushirikina nayo kwenye michezo, misiba, ibada, sherehe n.k.
  22: Mlinzi Namba Moja wa Mali Asili za Watanzania wa leo na Vizazi Vijavyo
  23: Rais atakae tafuta Utaifa na Alama Ya Utaifa kwa Vitendo ambayo itamjenga Mtanzania Kujisikia Yuko Tofauti na Mataifa Mengine na Mataifa mengine kujua kweli huyu ni Mtanzania.Manake hapa Tulipo tunakizazi ambacho ni Marekani na si Marekani, basi shida tupu katika kujitanabaisha na Utaifa
  24: Rais atakaekuwa Mlinzi wa Amani na Umoja wa Taifa
  25: Rais atakae kuwa anaona raha akiona mamilioni ya Watanzania wenzie wanaridhika na Maisha yao na vizazi vyao.wakiishi kwa raha na neema.

  Huyu Rais ndiye tunaepaswa kujua si Rais wa Majina ya Kitabaka,Ukoo, Urafiki, Ufisadi, Umwanamke, Ukanda nk.

  Tumekuwaje WanaJF kuwakubalia hawa jamaa kuwa tunajadiliana habari za watu na sio mambo [issues].Please tujuzane ukweli kuwa Urais ni Mali Ya nani pengine wengine sisi hatujui Urais ni taasisi ambae mmilki wake ni tofauti na Wananchi?
   
Loading...