Hivi ungependa kulelewa na wazazi wa aina ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ungependa kulelewa na wazazi wa aina ipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by agika, Jul 9, 2009.

 1. a

  agika JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kila mmoja wetu amelelewa kwenye mazingira tofauti na tamaduni tofauti , baadhi yetu tumeridhika na aina ya malezi tuliyopewa na kuahidi kwenye mioyo yetu kwamba na watoto wetu tutawalea kama tulivyolelewa sisi, na baadhi yetu pia hatujaridhika na malezi tuliyopewa na wazazi wetu kiasi kwamba tukaweka nia kwamba watoto wetu tutawapa malezi bora zaidi kuliko tuliyopewa sisi, hiii inatokana na ukweli kwamba miongoni mwetu wapo waliolelewa na wazazi wao wawili ,wapo waliolelewa na mzazi mmoja na pia wapo waliolelewa na mama au baba wa kambo.
  sasa basi JE! wewe mwana JF UNGEPENDA UWE MZAZI KAMA RAFIKI KWA MTOTO WAKO UMLEE KIUPENDO NA KIMAADILI ili mtoto akiwa na matatizo uwe kimbilio lake la kwanza AU UNGEPENDA UWE MZAZI MWENYE UPENDO WA KUJIFICHA KWA WATOTO NA KILA MARA FIMBO MKONONI, WATOTO WAKISIKIA SAUTI YAKO TU GETINI AU MLANGONI WANAKIMBIA SEBULENI WANAKIMBILIA VYUMBANI KWAO?
  Karibuni wanaJF tupeano mawazo juu ya kuwa wazazi bora.....
   
Loading...