FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,052
- 40,715
Chukulia mfano umeenda bar, tena umelipa kiingilio, ukaagiza bia moja baridi kisha ukaanzwa kuinywa taratiiibu kwa raha zako, halafu baada ya nusu saa unaambia bia yako ime-expire kwahiyo tunaiondoa na unatakiwa ununue nyingine, la sivyo pisha kiti akae mtu mwingine.
Hilo linaweza likawa ni jambo la ajabu lakini hivyo ndivyo ilivyo kwenye mitandao yote ya simu, na tumezoeshwa kidogo kidogo hadi tumezoea na kuona hiyo ndio haki, wakati ukweli ni kwamba huu ni unyang'anyi na ujambazi na si haki kumpokonya mtu kitu alichokilipia in full!
Nimefarijika kusikia kuna wakili mmoja anafuatilia suala hilo, hivyo nikaona nitoe tu pongezi kwake na kumuonyesha supprt yangu nikiwa kama mmoja wa wanaonyang'nywa haki yao, hapa yenyewe nina kama MB 800 kwenye simu ila zimebaki dk 5 tu liexpire, hivyo naandika haraka kweli ili nipost kabla sijaporwa bando langu.
Sasa basi, uzi huu ukilata walau comment 20,000 na likes walau 10,000 nadhani tunaweza fika mahali.
============================

===============================Hii ilianzia Kenya kuna wakili aliishtaki Safaricom na mitandao mingine...badae makampuni yakashtuka yakabadili wakati kesi inaendelea. So huyu wakili kapata idea Kenya, in other words wabongo ubunifu huo hatuna mpaka tukiona kwa wengine then nasisi tunaamsha popo
Update: Mashtaka dhidi ya makampuni manne ya simu
UPDATE MASHTAKA DHIDI YA MAKAMPUNI MANNE YA SIMU. Bashir Yakub, WAKILI 0714047241. Niliwaahidi kwamba nitakuwa nikiwaeleza kila tukio kuhusu mchakato wa kuyashitaki makampuni ya simu kwa unyonyaji. Mnakumbuka kuhusu yale mambo yetu matano, vifurushi kutokuwa na muda wa kuexpire,ruhusa ya...
www.jamiiforums.com