Hivi ungejisikiaje kama umenunua bia halafu ikipita nusu saa hujaimaliza unanyang'anywa na kuamrishwa ununue nyingine au upishe kiti wateja wengine?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,003
40,670
Chukulia mfano umeenda bar, tena umelipa kiingilio, ukaagiza bia moja baridi kisha ukaanzwa kuinywa taratiiibu kwa raha zako, halafu baada ya nusu saa unaambia bia yako ime-expire kwahiyo tunaiondoa na unatakiwa ununue nyingine, la sivyo pisha kiti akae mtu mwingine.
Hilo linaweza likawa ni jambo la ajabu lakini hivyo ndivyo ilivyo kwenye mitandao yote ya simu, na tumezoeshwa kidogo kidogo hadi tumezoea na kuona hiyo ndio haki, wakati ukweli ni kwamba huu ni unyang'anyi na ujambazi na si haki kumpokonya mtu kitu alichokilipia in full!

Nimefarijika kusikia kuna wakili mmoja anafuatilia suala hilo, hivyo nikaona nitoe tu pongezi kwake na kumuonyesha supprt yangu nikiwa kama mmoja wa wanaonyang'nywa haki yao, hapa yenyewe nina kama MB 800 kwenye simu ila zimebaki dk 5 tu liexpire, hivyo naandika haraka kweli ili nipost kabla sijaporwa bando langu.
Sasa basi, uzi huu ukilata walau comment 20,000 na likes walau 10,000 nadhani tunaweza fika mahali.
============================
Hii ilianzia Kenya kuna wakili aliishtaki Safaricom na mitandao mingine...badae makampuni yakashtuka yakabadili wakati kesi inaendelea. So huyu wakili kapata idea Kenya, in other words wabongo ubunifu huo hatuna mpaka tukiona kwa wengine then nasisi tunaamsha popo
===============================
 
Hata mifuko ya nailoni walisubiri hadi Kenya wapige kwanza marufuku, hivi ni kwanini sisi tunakuwa watu wa kufuata nyuma tu, kwanini sisi tusiwe ndio waongoza njia??!
 
Hii ilianzia Kenya kuna wakili aliishtaki Safaricom na mitandao mingine...badae makampuni yakashtuka yakabadili wakati kesi inaendelea. So huyu wakili kapata idea Kenya, in other words wabongo ubunifu huo hatuna mpaka tukiona kwa wengine then nasisi tunaamsha popo
Yeye mwenyewe alisema ameiga kutoka nchi nyingine....!Tumuunge mkono kwa jitihada zake...wewe uliyesikia kutokea kenya kabla kwanini hukuchukua hatua hizo?
 
Hii ilianzia Kenya kuna wakili aliishtaki Safaricom na mitandao mingine...badae makampuni yakashtuka yakabadili wakati kesi inaendelea. So huyu wakili kapata idea Kenya, in other words wabongo ubunifu huo hatuna mpaka tukiona kwa wengine then nasisi tunaamsha popo
Siyo lazima kila kitu mtu abuni. Kuna mengine ya kuiga na kuiga kwake kunakubalika. Ukienda nyumba ya mtu ukikuta ni safi na ukaiga hilo siyo jambo baya.
 
Habari wakuu.

Niende kwenye mada ni kwamba hili suala la ukomo wa vifurushi vya mitandao ya simu unapojiunga limekaaje?

Hivi ni haki mtu akijiunga apangiwe muda wa ku-expire kwa kifurushi?

Mfano nimeuziwa kifurushi kwa shilingi 1,000 halafu nikapewa mathalan dakika 20,SMS 100 na MB 100 kwa saa 24 halafu nikatumia dakika 10 pekee let say ambazo gharama yake ni shilingi 300 kati ya shilingi 1,000 niliyonunua kifurushi sasa muda unapoisha hiyo 700 wanayoichukua sio kitendo cha wizi?

Mfano umeniuzia bidhaa kwa shilingi 1,000 na nikakulipa kikamilifu iweje unipangie muda wa matumizi wakati nimeshakulipa pesa yako kikamilifu?

Hivi serikali haioni wizi wa mchana kweupe wanaofanyiwa wananchi wake kupitia mitandao hii ya simu? Nchi nyingi zimeachana na vitendo hivi vya wizi vyakumpangia mlaji muda wa kutumia bidhaa yake aliyoilipia kihalali nadhani bado sisi ndo tunaendelea kuibiwa na mitandao ya simu.

Kwanini wasijifunze kwa wenzao wa Tanesco ambapo wakikuuzia unit za LUKU hawakupangii ukomo wa muda wa matumizi badala yake utatumia unit zako hadi zitakapokwisa.

Unakuta wakati mwingine umejiunga kifurushi halafu mtandao wao ukasumbua kutwa nzima unakuja kushtuka kifurushi chako kimekwisha bila kukitumia na wala hawakufidii salio lako.

Au mwinhine amejiunga halafu umeme ukakatika hivyo kutokutumia kifurushi chake au mwingine alikuwa bize tu hajatumia kifurushi chake anashtuka anaambiwa muda wa kutumia kifurushi umeisha.

Yapo mengi yanayofanywa na mitandao ya simu kinyume na sheria ntaendelea kuyaorodhesha angalau watuhurumie kwa muda ambao wametupiga inatosha.

Serikali yetu sikivu tunaomba mlifanyie kazi hili kwa maslahi ya wanyonge ambao kuipata shilingi mia tano kwao ni mtihani mkubwa halafu bado akijiunga anapangiwa ukomo wa kutumia kifurushi chake ambacho amekinunua hivyo kuwa mali yake.

Pia mitandao ya simu iruhusu kugawa baadhi ya dakika, sms ama data kwa mteja mwingine ndani ya mtandao husika. Mfano mimi nimejiunga nimepata dakika, SMS na data lakini kuna mtu hana salio kabisa basi iwe ni kawaida kupunguziana dakika, meseji ama data.

Nawasilisha.
 
Wizi wa wazi wazi tunafanyiwa na serikali inayojiita ya wanyonge sijasikiaga ata wale wabunge wetu wanaopiga kelele nao ni wahanga wa hili maaan ni watumiaji wa mitandao ila kimya bungeni
Wabunge wetu wauone ujambazi huu
 
Back
Top Bottom