Hivi unawezaje kuishi na mwanaume ambaye humjui ndugu yake hata mmoja?

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Huwa nashangaa sana kuona binti anachukuliwa na mwanaume wanakubaliana kuishi pamoja bila hata ndoa, na cha ajabu utakuta masikini ya Mungu binti huyo anaishi na jamaa huyo akiwa hamjui ndugu yoyote wa upande wa bwana yake huyo.

Shida huanza pale linapotokea tatizo; binti hajui amtafute nani na aanzie wapi kwani hakuna ndugu yoyote anayemjua zaidi ya huyo bwana yake.

Ndoa za kuokotana tu mtaani zina changamoto kubwa sana. Utakuta binti tena ana watoto juu ila hamjui baba wa mume wake, mama wa mume wala ndugu yoyote wa bwana yake.

Ungana na mimi kupinga janga hili linalozidi kuzoeleka katika jamii.
 
Naona ndio maana ndoa nyingi siku hizi hazidumu kwa sababu hazina baraka za wazazi

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wazazi nao unakuta wanaishi kisela....mzazi kama mwenyewe anaishi kisela atatoaje baraka kwa ndoa ya mwanae!!!.........
 
Hilo nalo neno
Kwa maisha yalivyo hilo linawezekana ndio likawa tatizo

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Haya ndiyo yanayoendelea hapa kwa jirani yangu.....wazazi wanajua Bint yao anafanya kazi zanzibar kumbe bint kashaolewa
Huwa nashangaa sana kuona binti anachukuliwa na mwanaume wanakubaliana kuishi pamoja bila hata ndoa, na cha ajabu utakuta masikini ya Mungu binti huyo anaishi na jamaa huyo akiwa hamjui ndugu yoyote wa upande wa bwana yake huyo.

Shida huanza pale linapotokea tatizo; binti hajui amtafute nani na aanzie wapi kwani hakuna ndugu yoyote anayemjua zaidi ya huyo bwana yake.

Ndoa za kuokotana tu mtaani zina changamoto kubwa sana. Utakuta binti tena ana watoto juu ila hamjui baba wa mume wake, mama wa mume wala ndugu yoyote wa bwana yake.

Ungana na mimi kupinga janga hili linalozidi kuzoeleka katika jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom