Dar wametangaza kupuliza dawa mitaani jamani, jamani!
Sina uhakika na hiki wanachotaka kufanya Dar. Je, kinafanywa kwa utaratibu gani, lakini nahisi kuna shida.
Mimi sio mtaalamu wa afya lakini nahisi tunaweza kufanya vitu ambavyo tutatumia gharama lakini hatutapambana na korona.
Corona haizururi mitaani bali inasambazwa na watu, inatembea na watu na ninavyoijua Dar dawa haiwezi kupulizwa kila mtaa bali kutapulizwa maeneo fulani tu.
Lakini nahisi wale ambao wanabaini virusi vimeingia katika miji yao wanachokifanya
1. Ni kutangaza watu wakae majumbani mwao kwa siku kadhaa. maana yake unaondoa miingiliano ya watu. Kama kuna watu walikuwa na ugonjwa tayari basi ndani ya kipindi hicho watabainika na watapelekwa hospitali. Watu waliokuwa wamewazunguka watafuatiliwa kama ni familia na nyumba inaweza kupuliziwa dawa.
2. Mitani na hasa sehemu hatarishi ambazo watu wanakusanyika wengi zinapuliziwa dawa ili kama kuna sehemu virusi bado vimejibanza basi vinaangamizwa.
Ni lazima ufunge mipaka kuzuia wageni kukuletea ugonjwa tena. Inashangaza Dar bado wageni wanaingia, watu wanarandaranda mitaani, viongozi wanatuhamasisha kukusanyika kwa shughuli za ibada alafu wanatangaza kupuliza dawa.
Tusikopi vitu kwa kuwa tumeona watu wanafanya kitu fulani basi tunaiga na katika kuiga tunaonyesha jinsi gani tulivyo ama makini au tusivyo makini.
Ninatumaini upuliziaji uko well planned.