Hivi unaweza kujua kuwa gesi imekaribia kuisha?

delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,743
1,492
Habari wana JF,

Kuna swali huwa najiuliza nakosa majibu. Kama nilivyouliza kwenye kichwa cha habari hapo juu!

Hivi ninawezaje kujua gesi imekaribia kuisha??Gesi kwenye mtungi ambao natumia nyumbani maana kuna wakati umerudi saa 4 usiku unataka kufanya kitu gesi kwesheniii.

Wakuu kuna mbinu,mbuni,mbwinu yoyote ya kujua au ni makadirio tu kama mapato na matumizi?

Naomba kuwasilisha
 
Nunua mzani digital!Hili ni suluhisho la uhakika!Ila kwa wale watu wenye experience,gas ikikaribia kuisha kwa hii mitungi mikubwa basi utasikia sauti kubwa ya gas unapowasha,lakini pia harufu ya gas inakuwa inasikika kwa mbali,inahitaji uwe unajua kunusa kama mbwa!
 
Ni upuuzi Tu wa makampuni ya gas, Kwa nn wasiweke Mita ya kujua kias cha gas kilichobak, mpak uanze kutumia local method, mara moto wa njano, mara ufute na maji mara unuse harufu,aaah sidhan kama mitungi ya ulaya ipo hivi aisee, ndo mana kwenye gari mafuta yakielekea kukata unaona kabisa, hakuna haja ya kutegea mungurumo wa gar kujua wese linaelekea kibla...
 
Hakikisha kila siku unatingisha mtungi ili kubaini kiasi cha gas ndani ya mtungi....
 
Ni upuuzi Tu wa makampuni ya gas, Kwa nn wasiweke Mita ya kujua kias cha gas kilichobak, mpak uanze kutumia local method, mara moto wa njano, mara ufute na maji mara unuse harufu,aaah sidhan kama mitungi ya ulaya ipo hivi aisee, ndo mana kwenye gari mafuta yakielekea kukata unaona kabisa, hakuna haja ya kutegea mungurumo wa gar kujua wese linaelekea kibla...
Gauge zipo kiongozi, sema tu wengi wetu hatuna utaratibu wa kuzinunua. Zinafanana na zile zinazofungwa kwenye mitungi ya mafundi welder
 
Gauge zipo kiongozi, sema tu wengi wetu hatuna utaratibu wa kuzinunua. Zinafanana na zile zinazofungwa kwenye mitungi ya mafundi welder
Asante mkuu jibu lako zuri. Wengine hatuna uelewa vizuri hebu tueleweshe hizo gauge zipoje na unazifunga vipi?
 
Hizo gauge ni applicable kwa mitungi yote yaani kale kadogo(kirikuu) na mkubwa? Majibu tafadhali
 
Kuna meter/ gauge huwa zinauzwa na kufungwa pamoja na outlet valve kuonyesha kiwango cha gesi iliyobaki. Changamoto yake kinauzwa bei kidogo (around 55k hivi) unless bei iwe imeshuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom