mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Basi mimi niwatakie sikukuu njema, mengine yaishie humu.
Ni akili gani inayokataa utaratibu mzuri wa kupata viongozi waliochaguliwa kihalali na kistaarabu?
Ni akili gani inayopinga utaratibu wa wananchi kuwaondoa viongozi wao wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao kabla ya muhula wao kuisha? Ni akili ya zamani sana.
Pengine hata CHADEMA wangeshika dola kwa katiba hii wasingetamani kubadili kwa sababu ingewasaidia.. ni ujinga tu. Ndio maana nasema wanaopinga madai ya katiba mpya sio wanaCCM, ni watu wajinga. Na wanaodai katiba mpya sio wanaCHADEMA, ni wananchi wenye tamaa ya kurekebisha mambo ya hovyo ya nchi yetu.
Tunatamani kuwa na katiba mpya yenye tija kwa Taifa letu.
Sio eti CCM itoke madarakani au ibaki madarakani.
Sio eti CHADEMA ishike dola au isishike dola. Si hivyo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza - SACP Ramadhan Nghanzi, akizungumza na Viongozi wa CHADEMA amesema ameagizwa na Rais kuzuia kongamano la KATIBA na anatekeleza maagizo hayo mpaka atakapo pokea Taarifa nyingine.
Baada ya wizara ya fedha kuamua kuuumiza wananchi kwa tozo za miamala ya simu, na bunge kubariki maumivu hayo, bado unadhani kuna watu wapo bungeni kwa ajili yako?
Ukiwa kiongozi wa nchi, ukadhani kwamba wapinzani wa kisiasa ni maadui, ukawatazama kama watu wa kupambana nao badala ya kushirikiana nao, ukawapuuza na kuwadharau; na kama sauti za wapinzani hao ni kwa faida ya nchi, na kama wanapata kueleweka vema miongoni mwa jamii yenye uelewa mpana wa mambo (ukiondoa mashabiki), basi tarajia mwisho usio mzuri.
Waliokuwepo bungeni sio wetu wale tudai KATIBA.