Hivi unawakilishwaje na Mbunge asiyekatwa KODI?Anaanzaje kuwa na huruma na wewe? Hapo bado unadhani KATIBA sio muhimu!!

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,232
2,000
Basi mimi niwatakie sikukuu njema, mengine yaishie humu.

Ni akili gani inayokataa utaratibu mzuri wa kupata viongozi waliochaguliwa kihalali na kistaarabu?
Ni akili gani inayopinga utaratibu wa wananchi kuwaondoa viongozi wao wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao kabla ya muhula wao kuisha? Ni akili ya zamani sana.

Pengine hata CHADEMA wangeshika dola kwa katiba hii wasingetamani kubadili kwa sababu ingewasaidia.. ni ujinga tu. Ndio maana nasema wanaopinga madai ya katiba mpya sio wanaCCM, ni watu wajinga. Na wanaodai katiba mpya sio wanaCHADEMA, ni wananchi wenye tamaa ya kurekebisha mambo ya hovyo ya nchi yetu.

Tunatamani kuwa na katiba mpya yenye tija kwa Taifa letu.

Sio eti CCM itoke madarakani au ibaki madarakani.
Sio eti CHADEMA ishike dola au isishike dola. Si hivyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza - SACP Ramadhan Nghanzi, akizungumza na Viongozi wa CHADEMA amesema ameagizwa na Rais kuzuia kongamano la KATIBA na anatekeleza maagizo hayo mpaka atakapo pokea Taarifa nyingine.

Baada ya wizara ya fedha kuamua kuuumiza wananchi kwa tozo za miamala ya simu, na bunge kubariki maumivu hayo, bado unadhani kuna watu wapo bungeni kwa ajili yako?

Ukiwa kiongozi wa nchi, ukadhani kwamba wapinzani wa kisiasa ni maadui, ukawatazama kama watu wa kupambana nao badala ya kushirikiana nao, ukawapuuza na kuwadharau; na kama sauti za wapinzani hao ni kwa faida ya nchi, na kama wanapata kueleweka vema miongoni mwa jamii yenye uelewa mpana wa mambo (ukiondoa mashabiki), basi tarajia mwisho usio mzuri.

Waliokuwepo bungeni sio wetu wale tudai KATIBA.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,533
2,000
Katiba mpya ni mwanzo mwema wa mwisho wa matatizo. Haitapatikana bila ya kuwa tayari kuwa sadaka kwa Tanzania iliyo bora zaidi.

Pana thwawabu kubwa katika kuipigania bila kujali consequences kutoka kwa madwalimu!
 
mr yamoto

JF-Expert Member
Oct 2, 2016
920
1,000
Endeleeni kusema ooh hawa wanapiga tu kelele mitandaoni... ooh wanaharakati uchwara... ooh hawana jipya wanapinga kila kitu.
Endeleeni kuwazodoa wanaowasemea badala ya kujisemea wenyewe. Makelele yanasikika! Na tutapiga sana makelele.
 
mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,232
2,000
Endeleeni kusema ooh hawa wanapiga tu kelele mitandaoni... ooh wanaharakati uchwara... ooh hawana jipya wanapinga kila kitu.
Endeleeni kuwazodoa wanaowasemea badala ya kujisemea wenyewe. Makelele yanasikika! Na tutapiga sana makelele.
Ni wajinga tu hao.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,533
2,000
Kuna watu wanadhani ni utani.

Nimewaona watu waliodhamiria. Binafsi nimedhamiria na nina usongo kijima. Nikiwa kifua mbere ninasema tumedhamiria.

Consequence gani au ipi itatusimamisha sasa?

Wametuonyesha wao kuwa ustaarabu wetu haulipi kuwashawishi umuhimu wa kutumia busara.

Sasa kitaumana!
 
kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,685
2,000
Basi mimi niwatakie sikukuu njema, mengine yaishie humu.

Ni akili gani inayokataa utaratibu mzuri wa kupata viongozi waliochaguliwa kihalali na kistaarabu?
Ni akili gani inayopinga utaratibu wa wananchi kuwaondoa viongozi wao wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao kabla ya muhula wao kuisha? Ni akili ya zamani sana.

Pengine hata CHADEMA wangeshika dola kwa katiba hii wasingetamani kubadili kwa sababu ingewasaidia.. ni ujinga tu. Ndio maana nasema wanaopinga madai ya katiba mpya sio wanaCCM, ni watu wajinga. Na wanaodai katiba mpya sio wanaCHADEMA, ni wananchi wenye tamaa ya kurekebisha mambo ya hovyo ya nchi yetu.

Tunatamani kuwa na katiba mpya yenye tija kwa Taifa letu.

Sio eti CCM itoke madarakani au ibaki madarakani.
Sio eti CHADEMA ishike dola au isishike dola. Si hivyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza - SACP Ramadhan Nghanzi, akizungumza na Viongozi wa CHADEMA amesema ameagizwa na Rais kuzuia kongamano la KATIBA na anatekeleza maagizo hayo mpaka atakapo pokea Taarifa nyingine.

Baada ya wizara ya fedha kuamua kuuumiza wananchi kwa tozo za miamala ya simu, na bunge kubariki maumivu hayo, bado unadhani kuna watu wapo bungeni kwa ajili yako?

Ukiwa kiongozi wa nchi, ukadhani kwamba wapinzani wa kisiasa ni maadui, ukawatazama kama watu wa kupambana nao badala ya kushirikiana nao, ukawapuuza na kuwadharau; na kama sauti za wapinzani hao ni kwa faida ya nchi, na kama wanapata kueleweka vema miongoni mwa jamii yenye uelewa mpana wa mambo (ukiondoa mashabiki), basi tarajia mwisho usio mzuri.

Waliokuwepo bungeni sio wetu wale tudai KATIBA.
Mbona umeshuka sana? Anza juu. Tunatawaliwa na rais ambaye halipi kodi, anapata wapi ujasiri wa kuhamasisha watu kulipa kodi?
 
Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,211
2,000
Wengi hawaelewi umuhimu wa Katiba mpya.
Na watanzania wengi ni fuata mkumbo wakiambiwa na hao CCM kuwa Katiba mpya italeta vita basi na wao wanaitikia ndio na wanaufyata kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom