Hivi unapofiwa na mzazi/ mkwe inashauriwa kuomboleza siku ngapi?

matron

Member
Nov 16, 2011
66
56
Majuzi hapa kuna mdada nilimsimamia ndoa yake kwa bahati mbaya nikapata habari kuwa kafiwa na baba mkwe kilichonisikitisha ni kuwa yule binti na mmewe walisafiri kwenda msibani siku ya kuzika na asubuhi iliyofwata wazazi wa binti wakaja kuzugazuga hao wakasepa zao na kijana aliyefiwa na baba plus mkewe,hii ilinishangaza sana hadi sasa sina jibu au ndio mambo ya kimjini?Naombeni darasa kwa hapa jameni.
Nawasilisha
 
Angel Msofe ni hivi kijana aliyefiwa kaingia siku ya kuzika na kulipokucha wakwezake wakaingia asubuhi na mchana wakawazoa wakaishia siku hiyo hiyo,so inamaana mfiwa kalala usiku mmoja tu basi natumai umenielewa.
 
Majuzi hapa kuna mdada nilimsimamia ndoa yake kwa bahati mbaya nikapata habari kuwa kafiwa na baba mkwe kilichonisikitisha ni kuwa yule binti na mmewe walisafiri kwenda msibani siku ya kuzika na asubuhi iliyofwata wazazi wa binti wakaja kuzugazuga hao wakasepa zao na kijana aliyefiwa na baba plus mkewe,hii ilinishangaza sana hadi sasa sina jibu au ndio mambo ya kimjini?Naombeni darasa kwa hapa jameni.
Nawasilisha
matron, kwa uhandishi huu, tayari ushaonesha umesimama upande gani, unaposema "wakaja kuzugazuga" una maanisha nini, yaani walikuja na hawakuwa na la maana kwenye huo msiba...!?

Kuhusu maombolezo ya msiba inategemea na Iman yao ya dini au Mila za kabila lao...! Wapo ambao wanamaliza msiba baada ya kuzika, wapo wanao maliza msiba baada ya siku tatu tangia kwa marehemu kufariki, wapo wanao maliza msiba siku ya tatu baada ya kuzika.
 
Last edited by a moderator:

duh hii kali kukaa siku mbili tu msiba wa baba mkwe na afadhali hiyo na kijana mwenyewe aliyefiwa na yeye hivyo hivyo...hata kama ulikua una ugomvi na mzee lakini angalau angempa heshima..bila yule mzee asingekuepo leo katika hii dunia na hicho ki mke chake kisingekua kinatanua nae...Binadamu wengine wana roho mbaya!!:disapointed:
 
matron, kwa uhandishi huu, tayari ushaonesha umesimama upande gani, unaposema "wakaja kuzugazuga" una maanisha nini, yaani walikuja na hawakuwa na la maana kwenye huo msiba...!?

Kuhusu maombolezo ya msiba inategemea na Iman yao ya dini au Mila za kabila lao...! Wapo ambao wanamaliza msiba baada ya kuzika, wapo wanao maliza msiba baada ya siku tatu tangia kwa marehemu kufariki, wapo wanao maliza msiba siku ya tatu baada ya kuzika.

Asante X Paster kwa ufafanuzi ila nnaposema wakaja kuzugazuga ni kwamba walikaa kama lisaa limoja wakainuka na kuondoka,ila mimi kwa sababu ya uhusiano nilionao kwa hiyo familia ya mfiwa ilibidi tubakie kwa siku mbili.ingawa sikuelewa nini hasa maana ya wale kuondoka wakati bado tulukua hatujaanua tanga
 
Hayo matanga yalikuwa kwa masiku mangapi?

Wakati mwingine ni bora kuyapotezea mambo kama haya, kwa sababu yanaweza kupelekea ugomvi usio na lazima, kama walishazika hata mimi sioni sababu ya kuendelea kukaa msibani na kuongeza gharama kula na mambo mengine. Si watu wote uchukulia hali ya msiba kwa uzito au wepesi kila mtu na hisia zake...!

Kama wangekuja kuzika na kisha wakaondoka bila kuzika hapo kungekuwa na kila sababu ya kujiuliza, kulikoni, maana si katika tamaduni zetu, lakini kama ni kukaa matanga tu, kuna ambao wanayakubali na kuna ambao wanayaona kama kupoteza pesa, maana wanaona kuwa kama maiti kisha zikwa kuna sababu gani ya kukaa hapo...! Hiyo ni misimamo tu, basi inabidi kuwa elewa hao walio ondoka wanasimamia wapi, kabla ya kukaa na kuanza kuwalaumu.
 
Hakuna utaratibu maalum, akishazikwa na kilio kimeisha unless kuna maongezi yanayohusu mirathi. Msiba uko kumoyo sio kupiga kambi.
 
Mmmhh hayaga ya malimwengu ni mengi lol!
hii ndo dunia matron kula maisha kufa kwaja...ukifa na habari zako ni kwisha .... ukishawekwa kaburini watu wanaendelea na maisha kama kawaida... kwani utatufanya nini?
 
sawa Smile nimekupata na kweli sina cha kuwafanya
 
ndugu mleta mada, na wewe ulienda msibani kuomboleza au kuchunguza nani kaja na nani kakaa muda gani?
 
hii ndo dunia matron kula maisha kufa kwaja...ukifa na habari zako ni kwisha .... ukishawekwa kaburini watu wanaendelea na maisha kama kawaida... kwani utatufanya nini?

hata waliopendana kama kumbikumbi awajawai omba wafe siku moja ndo maana,hapa duniani mpende MUNGU sana wengine ni wasafir kama wewe kila mmoja ataondoka kwa wakati wake na maisha yatasonga kwa tunaobaki.
 
kweli mdau..... kila mtu kwa muda wake...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom