Hivi unapata wapi ujasiri wa kumtukana mwanamke?

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
762
772
Katika dunia kuna jambo ambalo huwa linafikirisha sana, kila mtu anapoamua kumtukana mtu lazima ataje sehemu za siri za mwanamke.

Hivi huyu mwanamke ameikosea nini dunia hii
hata sehemu yake ya siri ndo iwe tusi kubwa kuliko yote. Tukumbuke kwamba hiyo sehemu inayokuwa tusi ndo kila mmoja wetu ametokea hapo.

Ikumbukwe kuwa ukimtukana mama wa mwenzako ujue mama yako nae anacho kitu kama hicho. Wakati mwingine unamkuta mwanamke anamtukana tusi hilo mtoto wake sasa najiuliza hivi anamtukana au anajitukana.

Jamani tuwaheshimu wazazi wetu kwa kutowatukana wazazi wa wenzetu.
 
Malezi mabovu. Walolelewa wakaleleka kamwe huwezi kukuta akitamka matusi hayo.
 
Katika dunia kuna jambo ambalo huwa linafikirisha sana, kila mtu anapoamua kumtukana mtu lazima ataje sehemu za siri za mwanamke.

Hivi huyu mwanamke ameikosea nini dunia hii
hata sehemu yake ya siri ndo iwe tusi kubwa kuliko yote. Tukumbuke kwamba hiyo sehemu inayokuwa tusi ndo kila mmoja wetu ametokea hapo.

Ikumbukwe kuwa ukimtukana mama wa mwenzako ujue mama yako nae anacho kitu kama hicho. Wakati mwingine unamkuta mwanamke anamtukana tusi hilo mtoto wake sasa najiuliza hivi anamtukana au anajitukana.

Jamani tuwaheshimu wazazi wetu kwa kutowatukana wazazi wa wenzetu.
Inategemea mtukanaji ana mindset zipi!

Kwa mfano, tusi zito la kisukuma ni la kutaja nyeti za kiume, sasa unasemaje na kwa hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom