mikedean
JF-Expert Member
- Mar 15, 2018
- 3,255
- 4,599
Umeongea point ya muhimu sana hapa.Mimi nilikuwa nilinunua bodaboda used lakin ilikuwa imetumika kidogo maana mshua yule alimnunulia mtoto wake wa kiume ila dogo ubishoo wake akakataa kuwa bodaboda.Mshua akapaki mzigo hatimaye akatuuzia.Mii nilishafanya hii biashara ya kukodisha vitu tangu mwaka 2001-2003.
Karibu na pale mbezi Sasa kimejengwa kituo Cha mabasi. Niliweka mashine za kupiga matofali, vibao vya matofali, manailoni ya kufunika matofali ikija mvua.
Pia nilikuwa na welding machine 4 niliziweka hapa Sinza kwa Remmy Sasa Pana ukumbi unaitwa majestic hall. Nilikuwa nawakodisha mafundi uchomeleaji.
Nikawa na guta 2 zilikuwa zinapaki manzese.
Ic matumizi ya hivi vitu daah. Mtu akichukua kitu chako anavyokitumia yaani anakikomesha.
Hazingatii uwezo wa kitendea kazi. Mashine ndogo ya welding anataka aweke Moto mpaka mwisho ili skate chuma wakati Ile niya kuungia chuma na sio kukatia.
Baadae nilianza kukodisha screen kwaajili ya kombe la dunia Kama mtakumbuka mwaka 2002 world cup ilifanyika Japan na Korea. Jamaa walikodi mwezi mzima, lkn ilibidi wavunje mkataba kwa sababu hawakuwa na wateja maana mechi zilikuwa zinachezwa alfajili.
Ninachotaka kusema hapa unatakiwa kuwa makini Sana na kifaa chako. Matumizi ya wanaokodi huwa Ni mkomoeni. Vinginevyo kifaa chako kitachakaa kabla ya kukulipa..
Unaweza kukuta chombo kimewekwa upside down. Kipo kwenye vumbi, yaani unaweza kulia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tukatafuta kijana mmoja wa kanisani akawa bishoo akashindwa hata kupata 40 au 50 elfu kwa wiki wakti ndo bei ya kawaida kwa bodaboda alichofanya bila kukutaarifu sisi nae akawa anampa mshikaji wake ambaye wanafahamiana.Wakaanza kuikongoloa yani full kupiga pesa halafu kwetu wanaleta matatizo tu mara leo sijui blaabla tu kila wiki tena wanaleta blabla siku ya kukabidhi pesa,sasa yukawa tunajiuliza kwa nini wasiyutaalifu mapema?
Baadae mi na jamaa yangu tukachoka tukawanyang'anya pikipiki baada ya wiki kadhaa tukasikia mshikaji tuliyempa saiz kanunua yake,inamaana alikuwa anaficha hela ili aongezee anunue yake.Tukatafuta kijana mwingine ni mwaminifu na anatupa kiasi tunachotaka na kukitokea hitilafu kabla ya jumapili anatutaalifu na kwa ushahidi unaoonekana.
Kwa hiyo ukinunua, kitu kama ukampa mtu akusaidie kuendesha halafu akulipe kias kadhaa hakikisha unakuwa mfuatiliaji(management)na wakati mwingine unamwongoza(leadership)mfano kufanyia ukarabati chombo n.k.Sisi hatukufanya yote hayo kwa sababu tulikuwa wote wanafunzi mwaka wa 1 na jamaa yangu mwaka wa 3.Saiz jamaa amemaliza na yuko huru anaguatilia vizuri sana na kila hatua yuko nao.Saizi faida inapatikana.Ila ukiwa mwanafunzi au mfanyakazi kutwa kazini au chuoni basi hakikisha hata akisema amenunua sijui nini mwambie apige picha atume whatsup uone mwenyewe lakin kama yuko mbali na anauhakika humchunguzi anakuambia tu leo nimenunua helmet mpya ya abiria kumbe mwongo tu.
Sent using Jamii Forums mobile app