Hivi unajua kwamba Taarifa zako za siri kwenye smartphone yako zinaweza kuvuja bila kujua???!!

article

Senior Member
Joined
Sep 10, 2016
Messages
100
Points
250

article

Senior Member
Joined Sep 10, 2016
100 250
1480066519102.png

Smartphone ni simu ya mkononi inayotumia "mobile operating system" kama vile "ios","Blackberry 10 Os","Windows mobile 10 OS","Android,Sailfish","Tizen" kwa kutaja chache inayofanya kazi kama vile "computer operating system" ambayo inaiwezesha smartphone kupiga simu, kutuma "texts" ,barua pepe ,kuperuzi internet na kuwezesha vifaa vingine vya ziada vilivyomo kwenye smartphone kama vile Fingerprint sensors, GPS,Radio na Camera kufanya kazi kikamilifu.

Nchini matumizi ya smartphone yameongezeka kwa kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni ukiliganisha na siku za nyuma kidogo kutokana na watu kuwa na ufahamu mkubwa kuhusiana na manufaa ya matumizi smartphone na pia kutokana na ushindani mkubwa miongoni mwa wazalishaji wa smartphone duniani uliopelekea kushuka kwa bei ya bidhaa hii na kuifanya iweze kununulika hata na mwananchi wa kawaida mwenye kipato cha chini.

Makampuni kama vile Blackberry na Apple yamejikita katika kutengeneza smartphone za daraja la juu kwa ajili ya watu wenye kipato kikubwa wakati makampuni kama vile Samsung, Huawei, Techno,LG,Mi,ZTE,HTC kwa kutaja machache yanatengeza smartphone za daraja la juu kwa wenye kipato kikubwa na daraja la chini pia kwa watu wenye kipato cha chini hasa wa nchi za dunia ya tatu.

Watu wengi ambao wanatumia smartphone hasa katika nchi za dunia ya Tatu kama vile Tanzania wana uelewa mdogo kuhusiana na technologia ya habari na mawasiliano hasa katika masuala yanayohusu usalama wa taarifa zao za siri kwenye smartphone zao.Mara nyingi wanajikuta wanafanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa Taarifa zao za siri bila hata ya wao kujua wakati wa matumizi ya smartphone zao.

Taarifa muhimu za siri kwenye smartphone yako kama vile taarifa za kibenki , texts,Emails, mafaili ya siri au muhimu ya picha ,audio ,video au mafaili ya ofisini zinaweza kuvuja au kuibiwa au kunaswa na wadukuzi .Wadukuzi pia wana uwezo wa kuingilia mawasiliano yako wakati wa kupiga simu na kusikiliza mazungumzo yako na mtu mwingine upande wa pili.

Wadukuzi (Hakers) ni waovu wenye uelewa na utaalamu wa hali ya juu wa masuala ya computer wanaotumia technoligia ya habari na mawasiliano kufanya uharifu wa mtandaoni ili kukidhi mahitaji yao).Yafuatayo ni mambo makuu yanayoweza kusababisha Taarifa za siri au muhimu kwenye smartphone yako kuangukia mikono isiyo salama:

1.Kupakua na kuingiza kwenye simu 'Apps' dukuzi au Pelelezi:
Ni vizuri ukafanya utafiti kuhusiana na "App" fulani kabla ujaipakua na kuitumia kwenye smartphone yako kwani kuna App nyingine hasa za games na mitandao ya kijamii ambazo zinaweza dukua taarifa zako bila ya ya wewe kujua au kupeleleza mwenendo wa matumizi yako ya simu bila ya wewe kujua kama haujachukua hatua za kiusalama.Hatua za kiusalama unazoweza chukua ni kuzima mibadala ya kuona taarifa na vifaa kwenye simu yako kwa App husika.

2.Kuwa na kuta(firewalls) zisizo imara au zilizozimwa kwenye smartphone : Hakikisha unanunua smartphone yenye kuta imara zisizoweza kuvunjwa kirahisi na wadukuzi pia hakikisha wakati wote huwe zimewashwa.Simu zenye kuta ngumu ni Blackberry na Apple simu nyingine pia zina kuta ngumu ila kama una taarifa nyeti ni vizuri ukatumia simu nilizotaja kwani zinaaminika kwenye suala hili sana.

3.Kutokuwezesha "encryption" au kutokuwa na encryption :
Inatakiwa uwezeshe encryption kwenye smartphone yako na memory card kama ipo wakati wote ili mdukuzi akifanikiwa kuiba taarifa zako za siri asiweze kuzisoma au kuzielewa."Texts",au "Emails" na faili nyingine mbalimbali au "audio calls" zilizo "encrypted" ni vigumu kuingiliwa hivyo, encryption ni muhimu sana.

4.Kutochukua hatua za kiusalama wakati wa kutumia WiFi ya Umma:
Unapotumia WiFi hakikisha umechukua hatua zote za kiusalama kama vile kuwasha kuta (firewalls),kuwezesha encryption usipofanya hivyo mtu mbaya ambaye mnatumia WiFi pamoja anaweka kuingia kwenye smartphone yako na kuchukua anachotaka na kuondoka bila ya wewe kujua kama ufahamu wako utakuwa ni mdogo kwenye masuala ya technologia ya habari na mawasiano au kama hautakuwa na programme ya kiusalama kwenye simu yako.

5.Kutokuwa na "software" ya usalama au kuto "update" "software" hiyo: smartphone yako inapokuwa haina software ya usalama au unaposhindwa kui "update" kwa wakati inakuwa kwenye hatari kubwa ya kushabuliwa na wadukuzi hivyo hakikisha smartphone yako ina "security software" nzuri kama haina na kama inayo hakikisha wakati wote inakuwa "up to date".

6.Kutoweka passcode au kutotumia Fingerprint sensors :
Watu wengi taarifa zao uvuja au kuibiwa kutokana na kutotumia passcode au Fingerprint sensors kwenye kufunga simu zao hivyo kuziweka taarifa zao za siri matatani pindi smartphone zao zinapoangukia kwenye mikono isiyo salama.

Hakikisha hautumii passcode rahisi kukisiwa kama vile jina lako au jina la mtoto wako au tarehe yako ya kuzaliwa tumia passcode yenye mchanganyiko wa maneno na namba na picha kama smartphone yako inaruhusu.

Kwa kuwa watudukuzi wanajifunza mbinu mpya kila kukicha za kudukua taarifa za siri kwenye smartphone inawezekana hatua nilizozitaja hapo juu zisiweze kumzuia mdukuzi kuchukua anachokitaka kwenye smartphone yako.

Hivyo auna budi kuwa na sehumu mbadala salama ya kuhifadhia taarifa zako za siri kama vile "external SSD" au "HDD" kwa kuwa hizi haziwezi kudukuliwa au kupelelezwa kutokea mbali (remotely) kama hazijaunganishwa na mtandao au kwenye smartphone yako.

Nawakilisha,

Article.
 
Rudbway

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Messages
243
Points
225

Rudbway

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2014
243 225
Niko mbele kabisa nasikiliza darasa la udukuzi, nami nlkua nataka kujua namna ya kuweka encryption kwny computer na android
 
utakuja

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
919
Points
1,000

utakuja

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
919 1,000
Elimu nzuri, lakini nataka kujua jinsi gani ya kuwezesha encryption kwenye simu hasa hizi za android. Asante.
Kwenye simu za Android encryption inawezekana kwanzia version 5.0,6.0 hadi 7.0 ambayo ni Lolipop Marshmallow na Nougat cha kufanya nenda Settings>Security >Encrypt phone/Encrypt device.
 
Rudbway

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Messages
243
Points
225

Rudbway

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2014
243 225
Kwenye simu za Android encryption inawezekana kwanzia version 5.0,6.0 hadi 7.0 ambayo ni Lolipop Marshmallow na Nougat cha kufanya nenda Settings>Security >Encrypt phone/Encrypt device.
Mbona hapa kuna android version ni ndogo lakini hyo option encryption phone ipo? Hilo lipoje mkuu
 
Amoxlin

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
3,736
Points
2,000

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
3,736 2,000
View attachment 439332
Smartphone ni simu ya mkononi inayotumia "mobile operating system" kama vile "ios","Blackberry 10 Os","Windows mobile 10 OS","Android,Sailfish","Tizen" kwa kutaja chache inayofanya kazi kama vile "computer operating system" ambayo inaiwezesha smartphone kupiga simu, kutuma "texts" ,barua pepe ,kuperuzi internet na kuwezesha vifaa vingine vya ziada vilivyomo kwenye smartphone kama vile Fingerprint sensors, GPS,Radio na Camera kufanya kazi kikamilifu.

Nchini matumizi ya smartphone yameongezeka kwa kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni ukiliganisha na siku za nyuma kidogo kutokana na watu kuwa na ufahamu mkubwa kuhusiana na manufaa ya matumizi smartphone na pia kutokana na ushindani mkubwa miongoni mwa wazalishaji wa smartphone duniani uliopelekea kushuka kwa bei ya bidhaa hii na kuifanya iweze kununulika hata na mwananchi wa kawaida mwenye kipato cha chini.

Makampuni kama vile Blackberry na Apple yamejikita katika kutengeneza smartphone za daraja la juu kwa ajili ya watu wenye kipato kikubwa wakati makampuni kama vile Samsung, Huawei, Techno,LG,Mi,ZTE,HTC kwa kutaja machache yanatengeza smartphone za daraja la juu kwa wenye kipato kikubwa na daraja la chini pia kwa watu wenye kipato cha chini hasa wa nchi za dunia ya tatu.

Watu wengi ambao wanatumia smartphone hasa katika nchi za dunia ya Tatu kama vile Tanzania wana uelewa mdogo kuhusiana na technologia ya habari na mawasiliano hasa katika masuala yanayohusu usalama wa taarifa zao za siri kwenye smartphone zao.Mara nyingi wanajikuta wanafanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa Taarifa zao za siri bila hata ya wao kujua wakati wa matumizi ya smartphone zao.

Taarifa muhimu za siri kwenye smartphone yako kama vile taarifa za kibenki , texts,Emails, mafaili ya siri au muhimu ya picha ,audio ,video au mafaili ya ofisini zinaweza kuvuja au kuibiwa au kunaswa na wadukuzi .Wadukuzi pia wana uwezo wa kuingilia mawasiliano yako wakati wa kupiga simu na kusikiliza mazungumzo yako na mtu mwingine upande wa pili.

Wadukuzi (Hakers) ni waovu wenye uelewa na utaalamu wa hali ya juu wa masuala ya computer wanaotumia technoligia ya habari na mawasiliano kufanya uharifu wa mtandaoni ili kukidhi mahitaji yao).Yafuatayo ni mambo makuu yanayoweza kusababisha Taarifa za siri au muhimu kwenye smartphone yako kuangukia mikono isiyo salama:

1.Kupakua na kuingiza kwenye simu 'Apps' dukuzi au Pelelezi:
Ni vizuri ukafanya utafiti kuhusiana na "App" fulani kabla ujaipakua na kuitumia kwenye smartphone yako kwani kuna App nyingine hasa za games na mitandao ya kijamii ambazo zinaweza dukua taarifa zako bila ya ya wewe kujua au kupeleleza mwenendo wa matumizi yako ya simu bila ya wewe kujua kama haujachukua hatua za kiusalama.Hatua za kiusalama unazoweza chukua ni kuzima mibadala ya kuona taarifa na vifaa kwenye simu yako kwa App husika.

2.Kuwa na kuta(firewalls) zisizo imara au zilizozimwa kwenye smartphone : Hakikisha unanunua smartphone yenye kuta imara zisizoweza kuvunjwa kirahisi na wadukuzi pia hakikisha wakati wote huwe zimewashwa.Simu zenye kuta ngumu ni Blackberry na Apple simu nyingine pia zina kuta ngumu ila kama una taarifa nyeti ni vizuri ukatumia simu nilizotaja kwani zinaaminika kwenye suala hili sana.

3.Kutokuwezesha "encryption" au kutokuwa na encryption :
Inatakiwa uwezeshe encryption kwenye smartphone yako na memory card kama ipo wakati wote ili mdukuzi akifanikiwa kuiba taarifa zako za siri asiweze kuzisoma au kuzielewa."Texts",au "Emails" na faili nyingine mbalimbali au "audio calls" zilizo "encrypted" ni vigumu kuingiliwa hivyo, encryption ni muhimu sana.

4.Kutochukua hatua za kiusalama wakati wa kutumia WiFi ya Umma:
Unapotumia WiFi hakikisha umechukua hatua zote za kiusalama kama vile kuwasha kuta (firewalls),kuwezesha encryption usipofanya hivyo mtu mbaya ambaye mnatumia WiFi pamoja anaweka kuingia kwenye smartphone yako na kuchukua anachotaka na kuondoka bila ya wewe kujua kama ufahamu wako utakuwa ni mdogo kwenye masuala ya technologia ya habari na mawasiano au kama hautakuwa na programme ya kiusalama kwenye simu yako.

5.Kutokuwa na "software" ya usalama au kuto "update" "software" hiyo: smartphone yako inapokuwa haina software ya usalama au unaposhindwa kui "update" kwa wakati inakuwa kwenye hatari kubwa ya kushabuliwa na wadukuzi hivyo hakikisha smartphone yako ina "security software" nzuri kama haina na kama inayo hakikisha wakati wote inakuwa "up to date".

6.Kutoweka passcode au kutotumia Fingerprint sensors :
Watu wengi taarifa zao uvuja au kuibiwa kutokana na kutotumia passcode au Fingerprint sensors kwenye kufunga simu zao hivyo kuziweka taarifa zao za siri matatani pindi smartphone zao zinapoangukia kwenye mikono isiyo salama.

Hakikisha hautumii passcode rahisi kukisiwa kama vile jina lako au jina la mtoto wako au tarehe yako ya kuzaliwa tumia passcode yenye mchanganyiko wa maneno na namba na picha kama smartphone yako inaruhusu.

Kwa kuwa watudukuzi wanajifunza mbinu mpya kila kukicha za kudukua taarifa za siri kwenye smartphone inawezekana hatua nilizozitaja hapo juu zisiweze kumzuia mdukuzi kuchukua anachokitaka kwenye smartphone yako.

Hivyo auna budi kuwa na sehumu mbadala salama ya kuhifadhia taarifa zako za siri kama vile "external SSD" au "HDD" kwa kuwa hizi haziwezi kudukuliwa au kupelelezwa kutokea mbali (remotely) kama hazijaunganishwa na mtandao au kwenye smartphone yako.

Nawakilisha,

Article.
Tumia neno Nawasilisha kwani ndilo sahihi.

Binafsi nashukuru kwa elimu nzuri na yenye nia njema ya kulinda taarifa zetu.

Ubarikiwe.
 
utakuja

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
919
Points
1,000

utakuja

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
919 1,000
Mbona hapa kuna android version ni ndogo lakini hyo option encryption phone ipo? Hilo lipoje mkuu
Kwenye Android 5.0.1 ina Full disk encryption ambayo kwa namna moja ama nyingine ni bora kwenye security lakini ina punguza kidogo ufanisi wa simu yako (simu inakua slow kidogo)

Lakini Mkuu kama una simu yenye Android OS 4 ya kitkat au chini zaidi nakushauri tu ungefanya mpango wa ku upgrade maana hizo OS za chini ni rahisi sana kuzi ibia data kwa sababu ya kukosa security updates za maana.
 
Ngushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
9,115
Points
2,000

Ngushi

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
9,115 2,000
Kwenye Android 5.0.1 ina Full disk encryption ambayo kwa namna moja ama nyingine ni bora kwenye security lakini ina punguza kidogo ufanisi wa simu yako (simu inakua slow kidogo)

Lakini Mkuu kama una simu yenye Android OS 4 ya kitkat au chini zaidi nakushauri tu ungefanya mpango wa ku upgrade maana hizo OS za chini ni rahisi sana kuzi ibia data kwa sababu ya kukosa security updates za maana.
mkuu naomba nimegee kidogo hapo namna ya kuupgrade imekaaje hiyo!
somo zuri sana ubarikiwe
 
utakuja

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
919
Points
1,000

utakuja

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
919 1,000
mkuu naomba nimegee kidogo hapo namna ya kuupgrade imekaaje hiyo!
somo zuri sana ubarikiwe
Upgrade naongelea sana sana kwenye aspect mbili ya kwanza ni kwa ku upgrade kwa custom rom (maana hizi simu nyingi huwa watengeneza simu wengi awatoi update) name pili kwa kununua simu mpya
 
Forum statistics

Threads 1,389,236
Members 527,879
Posts 34,020,584
Top