Hivi unajua bia moja kwa siku inaweza kubadili maisha yako?

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,710
Hahaha!!! naona jinsi unavoshangaa na unataka kuniandalia bonge la tusi. Yaani hapo unajiuliza bia moja ya Tzs 2,500 inawezaje kubadili maisha ya mtu?

Penginepo wewe ni mlevi kama mimi katika umri huu miaka 25 maana wengine ulevi tumejifunzia chuo. Au penginepo wewe nakuona ni baba wa katoto kamoja katika umri wako huo wa miaka 30 lakini na wewe ni mlevi yaani kila siku ni mzee wa 'masanga' na umekuwa ukiwaapia wenzako hapa baa kwamba wewe bila chupa nne za castle larger kwa siku wewe huuoni usiku kabisa.

Nakuona pia pamoja na kuwa mlevi bado hujafanikiwa kupata ajira maana kwenye nchi yetu hii hapa tulipo sasa na tunapokwenda inawezekana kabisa kuna watu bila kupenda hawatakuja kuajiriwa kabisa kwenye maisha yao kutokana na ukweli kwamba uchumi wetu umeshindwa kutengeneza ajira ambazo zinaenda sambamba na ukuaji wa nguvu kazi yaani labour force inayotokana na utitiri wa vijana wanaotoka kwenye taasisi za elimu kila mwaka.

Kwa hiyo na assume wewe ni kijana mlevi ambaye huna ajira lakini kwa sababu jiji limeshakuvaa na umeshakuwa mtoto wa mjini na mishe mishe daily haukosi hata Tzs 20,000 kwa siku ambayo ndiyo inakufanya ugharamie castle larger chupa nne kabla usingizi haujakuchukua.

Lakini nakuambia hivi, kati ya hizo bia nne kwa siku unaweza kupunguza bia moja na ukawa unakunywa tatu. Ukifanya hivo utakuwa umeokoa Tzs 2,500 kwa siku.

Tzs 2,500 kwa siku ni sawa na Tzs 75,000 kwa mwezi

Sasa tuanzie hapo Tzs 75,000 kwa mwezi unaweza kufanya nayo nini? Najua wengi wanawaza kwamba wanatakiwa wakaweke akiba benki. Ila mimi sikushauru hivyo, hii Tzs 75,000 ukaweke benki au uende sijui ukafungue biashara hapana, hakuna biashara ya mtaji wa Tzs 75,000. Nakuambia uende ukawekeze kwenye mifuko ya kijamii, nikiwa na maana kuna haya mashirika kama NSSF, PPF, LAPF etc.

Ntatoa mfano kwa shirika kama PPF ambalo wao wameanzisha kitu kinaitwa 'wote scheme' kama sijakosea na naomba kama kuna mtu wa PPF atanirekebisha hapa. Ambayo hiyo inakuwa ni scheme kwa ajili ya watu ambao hawako katika mfumo rasmi wa ajira na wanaamua nao ku contribute ili nao waje kupata mafao kwa baadae. Nikisema mfumo ambao sio rasmi naweza maanisha may be mtu wa mishen town anapiga dili zake au labda mama tu anatembeza matunda yake au labda dereva wa daladala etc. Sasa inakuawaje na hiyo Tzs 75,000 yako?

Kwa sababu contribution katika hii mifuko ya pension inakuwa ni kama 20% ya mshahara wako basi tuna assume hiyo Tzs 75,000 ni asilimia 20% ya mshahara wako kwa hiyo basi tuna assume wewe mshahara wako ni Tzs 375,000 kwa mwezi ambayo baadae tutaitumia kwenye ku calculate mafao baada ya kipindi fulani kupita.

Sasa kwa mfano tu assume kwa sisi walevi ambao tumeapa kunywa bia mpaka siku ya kufa ina maana kwamba kama ukifanya contribution ya hiyo Tzs 75,000 kwa mwezi ina maana kwamba wakati natimiza miaka 55 ambao ni umri wa kustaafu ntalipwa old age pension ambayo ni

Benefit Type
Old Age
Period Contributed (MONTHS)
360
Average Best Salary of Three Years (TZS)
375,000.00
Monthly Pension (TZS)
174,568.97
Pension Gratuity (TZS)
8,728,448.28

Yaani hapo ndo na miaka 55 halafu pension ya bia moja kwa siku ambayo nili forgo miaka 30 nyuma inanipa Tzs 8,728,448 halafu hapo hapo wananiambia kwamba mzee Davion tutakulipa kila mwezi Tzs 174,568 mpaka siku ya kufa. Sasa can you imagine hapo mtu una miaka 55 na kama lets say utaishi kwa miaka 30 ijayo it means kwamba total utayopewa ni (174,568*360=62,844,480)

Au pia unaweza uka opt kufunga mkataba na hawa watu wa pension kwamba ukishafikisha miaka 55 ukaamua kuchukua gratuity ambayo utapata kiasi hichi.

Benefit Type
Gratuity
Period Contributed (MONTHS)
360
Average Best Salary of Three Years (TZS)
375,000.00
Monthly Pension (TZS)
0.00
Pension Gratuity (TZS)
27,270,000.00

Kwa hiyo ina maana hapo ukiwa na miaka yako 55 penginepo unaweza kuwa majalala kama wazee wengi wa umri huo ambao tunawaona sahiv lakini kwa sababu uli sacrifice bia moja kila siku kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita unajikuta sasa una Tzs 27,270,000 ambayo kwa namna moja ama nyingine ni pesa ambayo inaweza kukufanyia jambo fulani katika maisha yako kwa kipindi hicho una miaka yako 55.

Lakini pia ikumbukwe pale unapokuwa member wa hii mifuko ina maana kuna mafao mengine unakuwa unapata kwa kipindi cha ndani ya hiyo miaka yako ya kuchangia hiyo Tzs 75,000

Mfano kwa NSSF na PPF wao wanasema kwa kipindi baada ya miezi 3 ya kuchangia member atapata bima ya afya ambayo inasomeka hivi;

-Mume, Mke na Watoto 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na 21 kwa wanaosoma
-Wastaafu watakaotaka huduma hii baada ya kustaafu.

Mfano tu hapa kwenye bima ya afya kuna watanzania kibao hawana bima ya afya yaani ikitokea mfano mtu mke na watoto wanaumwa anaweka mikono kichwani kuanza kukopa hela akati angetumia akili kidogo akaacha ile bia moja ya saa tano asingekuwa na shaka yoyote angetibu mke na watoto bila shida.
Mafao mengine ni mengi tu kama

-Kujitoa, yaani saa yoyote mfano baada ya miaka yako kumi ukawa upo juu ya mawe unaenda kuchukua pesa yako.
-Elimu
-Kifo
-Ugonjwa
-Mikopo n.k.

Japo kuwa mtu unaweza kuona sio big deal ila kwa kweli kwa ulimwengu huu wa uncertainties inafika wakati mtu unakwama kabisa kimaisha na nimeshuhudia hii hata kwa wazazi wetu na jamii tunayoishi.

Kuna watu wengine humu humu kwa mfano wamekuwa wazazi wao walishindwa hata ada za chuo na wameshindwa kusoma. Na hivo hivo kwa sisi vijana baada ya miaka 30 huwezi jua utakuwa na hali gani financially kwa hiyo si vibaya ku consider vitu vidogo kama hivi na kuvitilia maanani.

Ni hayo tu kwa leo nisije nikarefusha sana maana mradi nimeeleweka maana nikiamuaga kuandika mimi napumzika kwenye page ya kumi. Halafu msidhani nafanya marketing hapana wala sipo kwenye hiyo sector ya pension ni katika kujaribu ku fantasize fursa mbalimbali katika maisha na kuamua ku share na nyie. Nadhani pia hapa kuna wataalamu ambao wanaweza kujazia nyama pale ambapo watahisi sijaweka sawa.

Mwisho kabisa kwa walevi wenzangu nasema sina bifu na nyie maana naona Bavaria na Econometrician wananiangalia kwa hasira kubwa na nasema mnaweza kuja kujumuika na mimi hapa yetu bar maana ndipo nilipo kwa sasa na haya mawazo yamenijia baada ya kumaliza bia yangu ya nne.

Regards Davion Delmonte Jr.
Nasomeka kutoka yenu bar
 
hizo mambo zinaanza muda gani. naweza kujiunga na kujitoa? baada ya muda gani? kiwango cha chini kujiunga ni bei gani.?
 
Dawa ni kuacha bia ni pepo.
Mkuu mi sijasema uache bia, just kupunguza tu na ku allocate ulicho kiacha kwenye matumizi sahihi.

eeeh umenishitua sana mkuu "kuacha bia"...:redface::redface: hata mimi sijawahi kufikiria hivo. we kitu hakina sukari lakini unaambiwa kitamu... unakiacha vipi sasa hapo kwa mfano :spy:
 
hizo mambo zinaanza muda gani. naweza kujiunga na kujitoa? baada ya muda gani? kiwango cha chini kujiunga ni bei gani.?
unaweza kuwa consult hao mabwana wa pension. Kuna hawa wa NSSF na PPF wanatoa hiyo scheme. Hii ya NSSF wanaiita Hiari scheme na ya PPF ni s'thing like "Wote scheme" kama sijakosea. Nadhani wahusika watakupa maelezo mazuri kuliko mimi nenda tu kwenye ofisi zao.
 
mwendelezo wa stori za wababu,
Sijawahi kusimuliwa story na mababu maana sikubahatika kuishi nao kijijini. Embu wewe mkuu unaweza kutuanzishia introduction babu zako walikuwa wanakuambia story gani wakati ukiishi nao. Unaweza ukasaidia wengi pia, hata mimi nikiwemo maana unaweza kuwa na nyongeza yenye tija maana mawazo chanya ndicho kitu tunahitaji kuliko kitu chochote kwa sasa. Karibu
 
Mkuu ubarikiwe sana.
Yaani bonge la mchanganuo aisee.
Tena wewe umesema bia moja tu,lakini viumbe vinaondoka bia teleeeee.

Naungana na mdau,muhim kuacha tu,maana wengine wakilewa wanagegedana mbele ya watoto,Ukimwi ndio rafiki zao.Wanakufa kila siku kwa Sukari na magonjwa ya moyo.
 
Mkuu ubarikiwe sana.
Yaani bonge la mchanganuo aisee.
Tena wewe umesema bia moja tu,lakini viumbe vinaondoka bia teleeeee.

Naungana na mdau,muhim kuacha tu,maana wengine wakilewa wanagegedana mbele ya watoto,Ukimwi ndio rafiki zao.Wanakufa kila siku kwa Sukari na magonjwa ya moyo.
Hahahahah ni kweli mkuu ila wakiamka watakushambulia... si unajua sisi walevi ukituambia tuache pombe tunavokuwa wakali lakini kabisa kuna umuhimu wa kufanyia kazi issue kama hizi japo ni ndogo.
 
Ikiwa sasa una miaka 25..wakati huo Mil. 8 itakuwa sawa na l?kitu... Bia nayo itakuwa inauzwa elfu 15 kwa chupa! Uliliangalia hili? Kuna watu hawajawahi kunywa Bia na ni masikini wa kutupwa...!!
 
Dogo sijakusoma kabisa!
Ngoja ntarudi baadae nikusome vizuri nikiwa pale [C/[Red]YAO BAR/Colour] na bia zangu tano mkononi.
 
Back
Top Bottom