Hivi unajisikiaje Mswahili mwenzako akikusalimia "jambo?"

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,617
28,720
Mzuka wanaJF!

Yani unakutana na Mmatumbi mwenzako anakusalimia JAMBO haki ya nani siitikii nanyoonya tu.

Japo ni neno sahihi la kiswahili katika kusalimiana ila automatically na rasmi ni kwa wazungu kulitumia kutusalimia.

Kiukweli kabisa waswahili wengi huona Ugumu kulitumia kusalimiana.
 
Bora hiyo kiko ile ya kiarabu wanaolazimishia watu hata wasio amini dini na lugha ya kiarabu kama media of communication
Labda mtu kama hajui kama wewe sio muislamu au aliyekusalimia hajui kama haitakiwi kuwasalimia hivyo wasio waislamu.

Lakini uislamu haujafundisha kuwasalimia hivyo wasiokuwa waislamu.
 
Labda mtu kama hajui kama wewe sio muislamu au aliyekusalimia hajui kama haitakiwi kuwasalimia hivyo wasio waislamu.

Lakini uislamu haujafundisha kuwasalimia hivyo wasiokuwa waislamu.
Hiyo salamu si inamaanisha "Amani iwe juu yako?"

Ni ya kawaida nafikiri yeyote inamstahili.
 
Hiyo salamu si inamaanisha "Amani iwe juu yako?"

Ni ya kawaida nafikiri yeyote inamstahili.
Naam ndio maana yake

Lakini waislamu wote duniani huitamka kwa matamshi ya kiarabu, ni salamu, ibada na alama kwa waislamu na haitamkwi vinginevyo yapo ina maana yake kama uliandika.

Hivyo sio sahihi kumsalimia hivyo asiyekuwa muislamu, na haishangazi kwa asiyekuwa muislamu kukataa kuslamiwa hivyo.
 
Back
Top Bottom