Hivi unadhani kuna athari gani zilitokea?

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,492
8,295
Wakuu nimekaa nawaza kuhusu kuondoka kwa wayahudi Misri kuliacha athari gani kijamii na kiuchumi huko Misri.
Sote tunajua walikuwa ni watumwa,walifyatua matofali na kujenga mapiramidi. Sasa wanapoondoka huko wanaendelea kutuelezea tu safari yao jangwani mpaka kaanan.

Lakini je huko walipotoka kulitokea nini labda kwenye jamii na uchumi wa Misri. Kwanini Wamisri hawajapublish kilichotokea kwao ili tukijue,au uchumi wao uliyumba sana kiasi hawakuona kama ni kitu kizuri kukielezea. Wakati mwingine tunapaswa kuwaheshimu na kuwathamini wanaotutumikia hata kama wamekuja kwa njaa zao?

Hivi Kuna mtu anafurahia kukimbiwa na mtumwa wake kweli,lakini mbona akiwepo unamdharau?

Naomba tujiulize kidogo nini matokeo ya kuondoka kwa wayahudi misri. Sote tunajua farao halutaka kabisa waondoke,hata baada ya kuwatoa kwa shingo upande aliamua kuwafuatilia na akajikuta anapata hasara pale bahari ya sham.

Unahisi nini kilitokea?
 
Kilichotokea ni kua Uzalishaji ulipungua..
Kwani nini kilichotokea baada ya Abolition of slave trade?
 
Kilichotokea ni kua Uzalishaji ulipungua..
Kwani nini kilichotokea baada ya Abolition of slave trade?
Huenda ni kweli ila umesemea uchumi tu, vipi ile jamii iliyobaki huko iliyokuwa imezowea luxury ilifanyaje labda.
 
Back
Top Bottom