Hivi unaanzaje kumwambia mwenzako katika mahusiano au ndoa kwamba umeathirika?

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,793
5,372
Kwa mfano, wale walioko kwenye ndoa labda baba na mama wote wanapenda michepuko au mmoja wao ni bingwa wa michepuko mbaya zaidi wanafika mbali hata kinga kwao inakuwa habari gani hawawezi kula pipi na maganda. Pia uhusiano wenu ni long distance labda mnaonana kwa mwezi au miezi kadhaa.

Je ikatokea umepima na ukagundulika umeathirika na Mr au wife amekuja na anahitaji kuwa na wewe utakuwa na guts za kumwambia kwamba umeathirika na unaanzaje,wife or Mr naomba tutumie protection why protection:tape:

Wife or Mr nina jambo la kusema oops naomba tuongee mmh.Jamani michepuko sio dili baki njia kuu kama inavyosemeka nusu ya wanandoa ndio sasa wanaogundulika wameathirika wanawake sasa nao wanamichepuko duuh.

Janga hili
 
Kubaki njia kuu ni muhim sana ila kwa sasa Kuna ndoa chache ambazo ni za mapenzi nyingi ni za kutafuta njia ya kutokea na kufikia lengo bila kujali upendo wa kweli hali hiyo hupelekea michepuko kwani baada ya muda unashindwa kuvumilia kuwa na mtu ambaye hukumpenda sana ila ulitaka kutimiza lengo.

Nirudi kwenye mada huwezi kumwambia mpenzi nimeathirika kwani hujui kama yeye ni msafi kiasi hicho kusema hivyo ni kuhalalisha fact kwamba kama nae kaukwaa ajue wewe ndio chanzo kaa kimya maisha yaendelee kupata maradhi hayo haimaanishi kesho unakufa maisha bado yapo

Ushauri:
Oa au olewa na mtu ambaye unampenda na uko tayari kuishi nae bila ya kuchepuka na usitengeneze mazingira ambayo mwenzi wako anaweza kutafuta furaha nje.
 
uhurumoja

Ooops hii ngumu mie nadhani ni kutafuta namna ya kwambia mwenzio kucheki maana inawezekana yeye hajaathirika
ukawa umemwambukiza gonjwa kwa namna moja ama nyingine
 
Last edited by a moderator:
Sio jambo rahisi hata kidogo. Mwaka 2008 Shangazi wa mama yangu alitumiwa msimamizi wa ndoa kuambiwa mume wake ni muathirika. Ni kama vile alikuwa ashajiandaa kwa habari kama hizo, tabia ya mume wake ilishashindikana. Alisema anamshukuru Mungu watoto wake walishaanza kujitegemea hakwenda kupima na mpaka leo ni mzima wa afya anafurahia wajukuu. Mume alikufa mwaka uliofuata.
 
ooops hii ngumu mie nadhani ni kutafuta namna ya kwambia mwenzio kucheki maana inawezekana yeye hajaathirika
ukawa umemwambukiza gonjwa kwa namna moja ama nyingine
hapana mi naona kukaa kimya ni busara zaidi ukimwi sio ajali kwamba unakufa hapo hapo unaweza ishi miaka mingi sana huku ukitengeneza mazingira ya ye kujua binafsi.
 
God forbid lakini ikitokea hivyo nitakachofanya ni kumwambia twende tukapime afya.
Majibu yakitoka ndio atajua....!
 
Kama unampenda na kumjali utajua jinsi ya kumwambia tu!hivi utakuwa tayari kumuua mtu asiye na hatia coz of your own ego???You lay all the cards on the table and handle the situation as it comes!!
 
Sio jambo rahisi hata kidogo. Mwaka 2008 Shangazi wa mama yangu alitumiwa msimamizi wa ndoa kuambiwa mume wake ni muathirika. Ni kama vile alikuwa ashajiandaa kwa habari kama hizo, tabia ya mume wake ilishashindikana. Alisema anamshukuru Mungu watoto wake walishaanza kujitegemea hakwenda kupima na mpaka leo ni mzima wa afya anafurahia wajukuu. Mume alikufa mwaka uliofuata.
Taarifa nayo huchangia MTU kwenda kwa haraka zaidi unaweza kuwa kimya na uache kabisa michepuko uanze kuishi maisha maaminifu.
 
Inatakiwa unamwambia huku ukiwa na sura ya tabasamu tu isiyoonesha kuwa hilo ni tatizo kubwa kiviiiiiiile, maana ukimwambia huku we mwnyw una sura ya simanzi yeye ndio ataumia zaidi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom