Hivi umewahi kuona askari wakifanya uhalifu halafu wakijichunguza wenyewe?

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Kumeibuka mijadala kila kona ya nchi swali kuu wanalohoji wananchi na baadhi ya watawala ni swali je askari waliofanya mauaji iweje waunde tume kuchunguza mauaji hayo?

Swali hili limekolezwa na moto aliouwasha Mh Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa mjini Magu njiani kuelekea mkoani Mara kwenye maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM.

Polisi Mtwara walitekeleza mauaji ghafla hao hao wakatangaza kuunda tume kuchunguza mauaji hayo ni kama kesi ya mbuzi anapewa fisi.

Sheria ya kuwalinda polisi pindi wafanyapo uhalifu ni miongoni mwa sheria mojawapo za kikoloni zinazofumbia uhalifu unapofanyika ,zinakandamiza haki za binadamu lakini pia zinawalinda polisi kana kwamba wao sio binadamu Bali malaika.

Sio watanzania wote wanaotambua udhaifu huu kwenye katiba yetu ,sheria hizi zinapaswa kukataliwa na umma kupitia mabadiliko ya katiba mpya(turejee rasimu ya Warioba).

Laiti kama hatutapinga sheria hizi kandamizi tutarajie nchi ya watawaliwa ,kuburuzwa na kukandamizwa.period

IMG_20220209_072208_377.JPG
 
Kazi ya polisi na ualimu si za kuruhusu mtoto kufanya ni shida tu basi.
 
Back
Top Bottom