Hivi umewahi kulala na mpenzi, mke au mume anayeota kwa kuongea,ilikuwaje?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,311
7,494
Hapa nilipo kwa sasa kuna ugomvi baina ya wanandoa,mwanamke anamgombeza mwaume kwa kuota na kumuongea mwanamke ambaye ni shost yake

"Suzi una tako zuri,mpaka natamani nilishike hivi"

Hiyo sentensi iliyotamkwa na mwanaume akiwa usingizini imeleta ugomvi mkubwa mpaka kwa shost wa mwanamke,mwanamke anaanza kumtuhumu huyo rafiki yake

Umewahi kuwa na mtu wa hivyo kwenye mahusiano yenu ambaye anaota kwa kuongea aliyokuwa anayafanya mchana,je ilikuwaje,na vipi ukiwa na mtu wa hivyo?

Usiku amelala anaanza kuzungumza aliyokuwa anayafanya mchana,huyu mtu ana siri kweli,anaweza akavujisha siri,na mtu wa hivyo akijijua anatakiwa mchana awe anatenda na kuzungumza mambo mema,la sivyo ugomvi hutaisha
 
Sijawahi kua na mwanamke wa namna hiyo...

Ila hizo kesi zipo... mwanamke kuongea mambo yake yote aliyotenda kutwa uzingizini...

Cc: mahondaw
 
Hata mimi huwa wananiambia nikiwa nimelala huwa naongea hii issue nikaja kumuuliza mama yangu akaniambia hata babu yangu naye alikuwa akilala usiku anaota huku anaongea ndio walivyokuwa wanaambiwa na mama yao
 
Siku ukioa una kazi nzito sasa kama na wewe utachepuka
 
Mh! Hiyo ya kuongea hapana, ila kutembea usingizini ndiyo zangu!! Mara kibao wife ananidakia mlangoni ananirudisha kwa bed

Sijawahi kutana na wa kuongea
usimkorofishe siku ukimkorofisha atakuacha uende gamboshi trust me
 
Mh! Hiyo ya kuongea hapana, ila kutembea usingizini ndiyo zangu!! Mara kibao wife ananidakia mlangoni ananirudisha kwa bed 😂😂😂

Sijawahi kutana na wa kuongea
Mkuu kuwa makini utakuja kupata ajali mbaya sana, unaweza paramia mti, ukuta au shimo.
 
Mimi kunakipindi nipo ugenini nikaanza kuota naongea na Salam Sk (meneja wa diamond) kubusu diamond kuja kufanya show moshi mjini hapa sasa asubuhi naamka kila mtu ananiangalia anacheka anaanza kusema "baba umeanza lini upromoter"
 
Mimi huwa naota sana hivyo ila wife akiniuliza namwambia sio mimi ni ndoto hiyo

Back
Top Bottom