Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Hauwezi kupinga kamwe mzazi hawezi wapenda watoto wote sawaa...!!! Ila hawezi mchukia mwingine kama sisi Kuna mmoja anapenda na baba na mwingine na mama so ni kawaida tu ila Ukileta shida yako mzee wetu hajawahi kubagua mtu anawasaidia wote sawa ila sisi tunajua anampenda sana Last born wetu
 
Kilichomtoa Simba ni ugomvi wake na Babra, sasa alituma audio clip mitandaoni kumchamba Babra, kuna kipande kwenye hiyo clip anamwabia Babra, "I promisee you" ...kwamba atamkomesha..

Hupendi mpira?

Back to business, si unanifungulia PM eti eeh?
Manara mwanaume suruali tu na hana akili wala ethics za kazi yake ila vile bongo uswahili uswahili wanaona sifa za bure.
Mpira mie napenda na ni shabiki kindakindaki loh.
Kesho nitafungua PM
 
Ndugu zangu (madada na makaka waliokuwa wanaishi Dar) walimpenda sana kaka yangu enzi za utoto. Wakirudi home likizo wanamletea zawadi lukuki ,, mimi naweza ambulia shati au tshirt moja au zero kabisa huku yeye anaweza pata pair zaidi ya tano ( tshirt/shati na suruali) na viatu na mabegi ya shule,, mimi alikuwa ananigawia begi shule ikifungua. Kakangu mmoja alikuwa ananiletea madaftari mazuri ambayo nilikuwa naibiwa mara baada ya kukusanya kwa mwalimu.

Ajabu najiuliza sasa ukubwani ,,hivi sababu ilikuwa ni nini kiasi ndugu zangu wa damu walikuwa hawanikumbuki! Kipindi icho sikuwai kujali wala kujiuliza.
Wakati mwingine nahisi ni hivi watu wanasema naonekana niko serious sana muda wote, hivyo pengine nilijenga umbali na ndugu zangu kwasababu ya mwonekano wangu ambao hauendani na ambavyo nilivyo.

Mimi ukinifahamu vizuri utagundua kuwa ni mpole na makarimu nisiyependa kujionyesha. Ikiwa nina kitu cha thamani nakausha lakini kimoyo natamani mtu mmoja akione ili anipigie promo.

Nimeongea ukweli mwingi sana
 
Manara mwanaume suruali tu na hana akili wala ethics za kazi yake ila vile bongo uswahili uswahili wanaona sifa za bure.
Mpira mie napenda na ni shabiki kindakindaki loh.
Kesho nitafungua PM
Hata mimi sijawahi kumuelewa Manara aisee, sema ndiyo hivyo tena, wabongo tuna shida mahali.

Asante sana, nitashukuru ukinifungulia PM my dear. Yani sijui kama ntalala usiku huu kwa ambavyo naisubiria kesho ifike; ambayo kimsingi imeshafika coz sasa hivi ni saa 02:55 usiku..
 
Nakumbuka wakati niko mdogo, mimi nyumban ndo first born....nilipita kipindi kigumu sana katika ukuaji, hasa nilikua naona waziwazi jinsi ambavyo wadogo zangu mapacha walivyokua wanapenda. Hawa mapacha ni wakike na wakiume, bwana hwa jamaa darasani walikua wazima..hivyo niliona ambavyo mama anampenda mdogo wangu wa kiume na baba alikua anampenda mdogo wangu wa kike. Iliniumiza na kuninyima raha, kuna siku tulikaa kibarazani, sijui ilikuaje tukawa tupo watatu mimi, mama na baba. Ndipo nikawaambia wazazi wangu kiukweli nyie mi hamnipendi mnawapenda hawa wenzangu, ila mama akapinga na akasema hapana si kweli.
Mimi kutokupendwa kwangu kulitokana na sababu nyingi, kama ugomvi aseeh wiki haipiti sijaleta kesi nyumbani, hizi ngumi nimepigana sana.
Kingine darasanai sikua nafanya vizuri kama watoto wengine, hasa huyu wakiume ndo alikua anakua wakwanza mara nyingi, huyu wa kike labda watatu hivi. Ila namba zangu mi huko 20 na kitu.
Kiukweli kutokuoneshwa sipendwi kulinikomaza kiakili, na nikaanza kupambana na kuwa mtu ambaye nataka kuwaonesha ndani yangu kuna kitu.
Kwasasa nyumban mi ndo napendwa hasahasa mama yangu, ananipenda sana na hilo nalijua na nampenda sana mama kuliko maelezo.
Nawasilisha.
Safi sana mkuu.umeamdika swadakta kabisaa na umeni bless.this is how the brave kid is n wazaz wako walikuchana live na ukajikuta unaji adjust mwenyewe
..good parenting..
 
Hii inatokan kupendwa au kukataliwa kwa sababu maalum, lkn pia kuna bond by nature mtoto anazaliw nayo ambyo inaweza kuendana na baba au mama, au mtoto bond yake inaweza isiendane na wote hii ikapelekea kuwa normal.
Kuna muingiliano na mfanano wa asili katika kushea bonds yaan yupi mnarandana nae katika hatima yako maishani.
 
Nashukuru wazazi wangu waliweza kubalance hiyo hali. Tupo wa 4 lkn sijawahi hisi nani anapendwa zaidi. Tumekuwa treated equally kwenye kila kitu.
Now nina Mtoto mmoja tu mapenzi yote yapo kwake.

Wewe inabidi utulie na kujifunza , tena usikilize kwa makini kwa wengine. Mtoto mmoja hauwezi kupima au kulinganisha kiasi cha upendo. Ila fanya fanya mrekebishe mkamletee mdogo wake mwenzake
 
Nashukuru wazazi wangu waliweza kubalance hiyo hali. Tupo wa 4 lkn sijawahi hisi nani anapendwa zaidi. Tumekuwa treated equally kwenye kila kitu.
Now nina Mtoto mmoja tu mapenzi yote yapo kwake.
Upendo wa mzazi kwa mtoto mmoja haimaanishi kua hao wengine hawapewi wanachohitaji na hawapendwi, kila kitu kitakua sawa kabisa, ila ukweli ni kwamba kati yenu wote kuna mmoja ndio favorite.
 
Kipindi cha utoto tuliishi kwa babu na bibi. Ndugu zangu walikuwa na majina ya upande huo walipata upendeleo kuliko mimi hasa kutoka kwa bibi na ma aunt. Mara mbili nimepata majeraha makubwa lakini response ya walezi ilikuwa hailingani na vidonda nilivyopata. Hio hali imeendelea mpaka ukubwani maana maneno na dharau vipo ila tu nazoea. Ukija kwa wazazi napo ni yaleyale mzazi mmoja ana upendeleo kwa mtoto mmoja pamoja na jitihada zangu za kuwa kijana mwema na mchapakazi ila ni kama sionekani ninachofanya.
Kwa kweli namuomba Mungu anijaalie nikipata watoto wasipitie niliopitia.
 
Hata mimi sijawahi kumuelewa Manara aisee, sema ndiyo hivyo tena, wabongo tuna shida mahali.

Asante sana, nitashukuru ukinifungulia PM my dear. Yani sijui kama ntalala usiku huu kwa ambavyo naisubiria kesho ifike; ambayo kimsingi imeshafika coz sasa hivi ni saa 02:55 usiku..
Wabongo hatupendi kufata ethics na nidhamu majority ni sadist ndio maana wanakuwa Happy wengine wakitukanwa na kuzalilishwa loh.
Pm nafungua baadae
 
Usipopendwa na wazazi wako au mmojawapo utapendwa sana Mungu,nilipitia maisha ya kutopendwa na baba leo hii baba ni rafiki yangu mkubwa.
Kuna kitu nimejifunza,wanaopendwa sana na wazazi wao wanakuwa vichwa maji ,wanageuka mizigo kwa wazazi wao na familia nzima kwa ujumla.
Wapendeni kwa kiasi watoto wenu.
 
Upendo wa mzazi kwa mtoto mmoja haimaanishi kua hao wengine hawapewi wanachohitaji na hawapendwi, kila kitu kitakua sawa kabisa, ila ukweli ni kwamba kati yenu wote kuna mmoja ndio favorite.
Sijakataa hilo linalowezekana. Nilichomaanisha mimi ni kwamba sijawahi hisi nani ndo favourite. Walijua kufanya tusigundue...hakukuwa/hakuna upendeleo wa wazi wazi.
 
Wewe inabidi utulie na kujifunza , tena usikilize kwa makini kwa wengine. Mtoto mmoja hauwezi kupima au kulinganisha kiasi cha upendo. Ila fanya fanya mrekebishe mkamletee mdogo wake mwenzake

Ha haaa mdogo wake haji tena nilishafunga hiyo chapter. She's 18 sasa.
 
Ha haaa mdogo wake haji tena nilishafunga hiyo chapter. She's 18 sasa.

Niwie radhi kwa kauli zangu ikiwa ni hivyo na bila shaka sijakukwaza Rafiki.

Mungu muumba mbingu na nchi amtunze na kumlinda binti, akue katika njia bora. Na yeye ajekua na upendo wa dhati kwa watoto wake atakaojaliwa...aendelee kuwa furaha katika maisha yenu.
 
Back
Top Bottom