Hivi ulipokuwa shule ya msingi,O-level na A-level ushawahi kuwa na cheo gani???

kuna nyingine nilikuwa nazitoa wino nahamishia kwenye peni nyingine.. Utoto bana..!

teh teh yaani unajipa kazi kubwa,mi nilikuwa naiacha nyumbani halafu nakuja nayo shuleni baada ya kama wiki mbili hivi.
 
Hahahah hahha hahha,
Sio mm bana,mie sikuwahi kupigana hata siku moja,
Kuna wakati walianzisha ule mchezo wa kila tukitoka shule mnachaguliwa 2 unachorwa mstari mpigane lol,nikajipendekeza kwa mwalim mkuu ikawa kila tukitoka jioni nawahi kwenda kumbebea mkoba wake na kumpelekea kwake ambapo niliepuka kuchaguliwa kupigana!
kwahiyo hapo kupigana siyo hiari ya mtu,ukishachaguliwa lazima ushiriki dondi....duh hapo hamna demokrasi
 
duh..
nlikuwa singer wa darasa from class 2...yani mi mwalimu ka kidhungu akiingia ananiita niimbishe wimbo kwanza then somo!
ilikuwa raha maana mara nyingi alikuwa ananikuta mbele nimepigishwa magoti na monita kwa usumbufu, akifika tu najua ndo muda wangu wa kusimama...gud old days!!
 
mkuu enzi hizo ni kama unaonewa ila leo ukikumbuka yaani unaona ilikuwa raha sana
 
kwahiyo hapo kupigana siyo hiari ya mtu,ukishachaguliwa lazima ushiriki dondi....duh hapo hamna demokrasi
Hapo hakuna cha hiari unachochewa mpaka unapata hasira mstari unachorwa mtanange unaanza,ukishinda unatafutiwa mwingine siku ijayo,ukifanikiwa kuwadunda wote ww ndio unakua mbabe wao!
 
Nilipokuwa darasa la 5 nilipewa cheo cha mgonga kengele a.k.a mtunza muda, cheo hicho nilipewa ili nisiwe mtoro maana nilikuwa kilaza mbaya, nilipoingia form one nikawa kocha wa timu ya form one(footbal)
 
Hapo hakuna cha hiari unachochewa mpaka unapata hasira mstari unachorwa mtanange unaanza,ukishinda unatafutiwa mwingine siku ijayo,ukifanikiwa kuwadunda wote ww ndio unakua mbabe wao!

sisi tulikuwa tunazipiga hizo tukitosha shule kuelekea nyumbani,ila kwa waliokorofishana siyo kupangiwa
 
Nilipokuwa darasa la 5 nilipewa cheo cha mgonga kengele a.k.a mtunza muda, cheo hicho nilipewa ili nisiwe mtoro maana nilikuwa kilaza mbaya, nilipoingia form one nikawa kocha wa timu ya form one(footbal)

teh teh mi nilikuwa kipa wa ziada,basi nilikuwa napenda kipa mwenzangu aumizwe ili mi nipate nafasi
 
sisi tulikuwa tunazipiga hizo tukitosha shule kuelekea nyumbani,ila kwa waliokorofishana siyo kupangiwa
Bora na nyie bana,
Yani sie kulikuwa na watu wanashabikia hiyo kitu acha kbs,
Ilienda mpaka mwali mkuu akaipiga marufuku lkn wapi ikatafutwa location nyingine na watu wakawa wanaendelea kudundana tu!
 
Mawenzi primary nilikua kingozi wa kuiba pipi toffie na blue band kwenye mabegi ya wanafunzi, na kuvuta watoto wa kihindi nywele, Secondari nilikua monitress form1, form 2 nikawa academic prifect, form 3-4 nikawa assistant wa head girl lakini kwa miaka yote mi4 nilikua kiongozi wa kuiba mahindi ya shule,
 
teh teh teh kumbe ulikuwa unaihujumu shule halafu unaonea watu
 
me nilikuwa monitor lakini baada ya siku tatu nilivuliwa cheo baada ya ticha aliyenipa cheo hiko kuniuliza 8 mara 6 ngapi?? Me nikamjibu 21
 
Mimi nilikuwa na cheo kikubwa sana shule msingi hadi walimu walikuwa wananiheshimu darasa la nne, mwenzenu nilikuwa TIME KEEPER. Yani hata mwalimu akiwa anafundisha somo limenoga mimi huyoo time ikifika naenda kugonga kengele basi mwalimu anakusanya virago anasepa. Jamaa walikuwa wananigombania kweli niwaachie wagonge. Kukiwa na emergency nafuatwa , Walinikoma.

Nataka nitumie hii title yangu ya Primary kuja kugombania urais wa Jamhuri ya muungano baadae maana sikuwahi tena kupata wadhifa mwengine shule wala chuo na sikutaka kabisa majukumu.
 
Back
Top Bottom