masara
JF-Expert Member
- Jul 20, 2016
- 1,738
- 2,279
Habari za mchana huu wadau na wapenzi wasomaji,
Nikiwa kwenye pilika pilika za kutafuta mwenza wa maisha (mwanamke) sehem yotote nitakapompatia hata hapa jf kama yupo mimi namkaribisha PM tuone nini kitafata hasa hapa Mwanza. Nimejikuta najiuliza tu kwa sauti na nimeona niulize hapa ili tubadilishane uzoefu.
Mara nyigi katika miaka ya kuoana unakuta bado kijana yuko kwenye nyumba ya kupanga na binti na yeye kama kaanza kazi mkoa tofauti na kwao basi ndio yuko kwenye ka ghetto kake na au yuko kwao eidha amechoka kimaisha na anaishi maisha ya mizinga kwa ndugu jamaa na marafiki.
Lakini kuna wengine unakuta kimaisha sio mbaya maana tayari labda kijana ameshajenga na ana gari yake na maisha yanaenda vizuri tu vivyo hivyo kwa dadaz
Au msichana ana maisha yake na anajimudu bila shida lakini kwa vile kuolewa na kuoana ni jambo la kheru basi wanalazimika kuishi pamoja na maisha yanaendelea.
Lakini pia inawezeka ikatokea upande mmoja anaweza kuwa mwanaume au mwanamke akamkuta mpz/mchumba/mme/mke akiwa katika maisha duni.. kama ni mwanamke anatolewa kijijini hana hili wala lile halafu jamaa ndio anawekeza kumpanga hadi anaonekana kweli ni mama fulani yule
au mwanamke anamkubali mwanaume na kumkuta akiwa na maisha duni.. yaani ya chumba kimoja na godoro (kama unavyojua) lakini anamvumilia na baadae maisha yanabadilika akiwa naye
Lakini pia mnaweza kuoana mkiwa na maisha mazuri na ghafla maisha yakaporomoka na kurudi chini na hali ikawa ndivyo sivyo kabisa.
Hivyo baada ya utangulizi huo mrefu kwa wale walio kwenye ndoa tayari sio mbaya tukasikia, wewe mwanaume/mwanamke ulio(a/lewa) ukiwa na hali gani kimaisha na maisha yamebadilikaje ukiwa ndani ya ndoa? . Na hayo mabadiliko yameathiri vipi ndoa yako na upendo wenu kwa ujumla... huenda upendo unaongezeka au ndio hukutarajia kama atakuwa hivyo na unajutia kukutana naye. Na unavyofikiri mabadiliko ya kimaisha yanahusiana na mabadiliko ya kimahusiano.
Sababu ya kuleta uzi hii ni pale unaposikia mwanandoa analalamika na kudai kuwa.. alimkuta akiwa na hali fulani lakini maisha yamembadilisha.. mfano alikuwa anawahi kurudi nyumbani au alikuwa hanywi pombe lakini baada ya maisha kubadilika na tabia zimebadilika na hazieleweki kabisa.... Na mengine mengi
NB. Hata kama hauko kwenye ndoa ila unalo la kuchagia we karibu sana