Hivi ulaya Trafiki huwa nao wanakaa barabarani kusimamisha magari?

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
842
1,363
Mi naomba tu kuuliza kwa anayejua au aliefika huko ulaya, hivi huko nako mapolice /trafik huwa wanasimama kando kando ya barabara na kusimamisha magari, na kama ni hivo je nao wanakuwa na vitabu vya risiti vya faini.
Mi sijui hii tabia naiona kama ni kitu cha ajabu yaani trafiki hamna mbinu nyingine zaidi ya kukaa chini ya mti pembeni ya barabara.
Na je nashindwa kuelewa hizo pesa za rushwa ambazo ni nyingi zaidi ya hizo zinazoandikwa huwa wanakula na nani, maana ni nyingi sana, je huwa wanapeleka mgao kwa wakubwa wao au?
Halaf kwanini trafiki wengi wanaroho mbaya sana, je wanakuwa trained kuwa na roho mbaya au ndo walivozaliwa
 
Umeuliza maswali mengi sana mpaka nimesahau swali la msingi..
 
Nimeendesha gari zaidi ya miaka mitano nikiwa sina licence hapa UK na kukamatwa na traffic police mara mbili tu.
Mara ya kwanza niliingia kwenye mzunguko (round about) bila kupunguza mwendo, ilikuwa usiku wakaniotea, wakanipiga fine na kukata point tatu kwenye licence yangu(nilikuwa na provisional licence)
Mara ya pili waliniotea kwenye gas station sababu walikuwa na record zangu kuwa sina full driving licence.
Traffic police wa UK hawakusimamishi kama gari yako ina vibali vyote (insurance,road tax, MOT) na ukiwa na leseni ndio unawasahau kabisaaaa.
Vitabu vya risiti hawana, wao wanakuandikia then utaletewa barua ya msala wako kisha utalipa online.
N.B: ila ukiendesha gari lenye msala basi tegemea kusimamishwa sana tu au ukiwa unayumba barabarani
 
Zamani traffic police hata Ulaya walikua na kitabu cha faini, kama umepita na red light kwa mfano utakuta faini yako utakapoenda kurenew road license, Yaani kama traffic amewahi kuandika Namba ya gari, wanasimamisha magari wakati wakukagua bima na driving license, na anakua amesimama katikati ya njia panda (junction) huku akiwa amevaa gloves nyeupe nakuongoza magari kwa ustadhi mpaka unaona raha mikono yake inavyo move!
 
mom can I see your ID please? kauli hii ni common sana kwa trump.
 
Nimewahi kutembelea nchi fulani iliyoendelea kule ukifanya kosa kuna sensor barabarani utaenda mwenyewe kulipa faini maana usipoenda pesa inazidi kwa masaa mwisho wa siku utawaachia gari.
Jamaa alinidaka naenda 65 kwenye eneo la 45 akanipa tiketi ya dola 70. Basi mi nikapuuzia. Kuja kushtuka baada ya miezi kama minne hivi kupita tayari nikakuta nahitajiwa kwenda mahakamani na leseni yangu kumbe imeshakuwa suspended. Jasho lilinitoka. Ndipo nikajifunza kuwa ukipata tiketi ilipe kama hutaki nenda mkapambane mahakamani. Huko nako kama wamekudaka kwenye maCCTV yao basi ukishindwa inabidi ulipie gharama zote za kesi. Tiketi ya dola 65 unaweza kujikuta inaondoka na dola kibao !!!
 
Mi naomba tu kuuliza kwa anayejua au aliefika huko ulaya, hivi huko nako mapolice /trafik huwa wanasimama kando kando ya barabara na kusimamisha magari, na kama ni hivo je nao wanakuwa na vitabu vya risiti vya faini.
Mi sijui hii tabia naiona kama ni kitu cha ajabu yaani trafiki hamna mbinu nyingine zaidi ya kukaa chini ya mti pembeni ya barabara.
Na je nashindwa kuelewa hizo pesa za rushwa ambazo ni nyingi zaidi ya hizo zinazoandikwa huwa wanakula na nani, maana ni nyingi sana, je huwa wanapeleka mgao kwa wakubwa wao au?
Halaf kwanini trafiki wengi wanaroho mbaya sana, je wanakuwa trained kuwa na roho mbaya au ndo walivozaliwa
Kwanza nchi nyingi za Ulaya polisi anawashughulikia wote, wenye magari na wengineo. Hawasimami barabarani ila wanakuwa kwenye magari yao maalum wanafanya patrol almost kila mtaa/barabara hadi vijijini.
Gari zao ziko fitted na system inaitwa ANPR yaani Automatic Number Plate Recognition. Humo kuna data za madereva na gari zote, gari yako ikipita system yao inasoma namba ya gari yako ndani ya sekunde inawapa jibu kama gari halina vibali au dereva hana leseni, anadaiwa au ana kosa lingine la jinai.
Mara nyingine huwa wanatega sehemu ambayo wanajua wahalifu wanapenda kutorokea. Hawakusimamishi bila kosa,aidha gari ina kasoro,wewe una kasoro au umeendesha vibaya.
Hii system sasa hivi polisi wetu wanaitumia kukamata wale wasiolipa faini, wangekuwa na magari ya kisasa ingekuwa ndani ya patrol car badala ya kukaa nayo kibandani.
 
Hiyo kawaida kuna ukaguzi ambao haufanywi na mashine traffic ni duniani kote sio bongo tu nchi nyingine kama Malaysia kila ukitembea km 20 lazima ukutane na kituo
 
Kwanza nchi nyingi za Ulaya polisi anawashughulikia wote, wenye magari na wengineo. Hawasimami barabarani ila wanakuwa kwenye magari yao maalum wanafanya patrol almost kila mtaa/barabara hadi vijijini.
Gari zao ziko fitted na system inaitwa ANPR yaani Automatic Number Plate Recognition. Humo kuna data za madereva na gari zote, gari yako ikipita system yao inasoma namba ya gari yako ndani ya sekunde inawapa jibu kama gari halina vibali au dereva hana leseni, anadaiwa au ana kosa lingine la jinai.
Mara nyingine huwa wanatega sehemu ambayo wanajua wahalifu wanapenda kutorokea. Hawakusimamishi bila kosa,aidha gari ina kasoro,wewe una kasoro au umeendesha vibaya.
Hii system sasa hivi polisi wetu wanaitumia kukamata wale wasiolipa faini, wangekuwa na magari ya kisasa ingekuwa ndani ya patrol car badala ya kukaa nayo kibandani.
Mmh hawa wetu wakipata mavifaa hayo mbona tutakoma na tulivyo na roho mbaya hivi. We fikiria saivi tu hadi mtu anakupandia mitini.

Juzi kati kuna mmoja kanidaka pale salendar kisa nimepita kwenye taa ya njano...fyuuuu
 
Sio nchi za ulaya tu hapa hapa Africa kusini huwezi kuta polisi wa trafiki barabarani kama huku kwetu.Jijini Joburg na karibu na uwanja wa Oliver Tambo kila mahali kuna sensors ukifanya kosa sensors zinakuona na namba ya gari imejirekodi utakutanana risiti yako huko mbele.Kule kuna line hata kuendesha gari speed ndogo ni kosa unachelewesha wenzako.Trafick utamkuta tu mahali ajali imetokea umeme kule haukatiki mara kwa mara kama huku.Ni suala la technologia tu hata wao walikuwa hawako hivo na sisi tutafika huko
 
Sehemu nilizopita wao wanakuwa ndani ya magari yao , ila sometimes wanapaki sehemu ku monitor magari japo sio sana, kifupi ni tofauti kidogo na hapa bongo.

Hapa kwetu wamekaa kiulimboulimbo hawapo kikazi
 
Ukiwa hata porini usije dhani hawa jamaa hawapo wapo we endesha tu speed inayotakiwa othewise kutoka dar hadi Mwanza usafiri na bulungutu la hela.
 
Attachments

  • police2.PNG
    police2.PNG
    87.5 KB · Views: 42
Tofauti kabisa na na bongo..... Utasimamishwa km kuna tatizo umelifanya... Muda mwingi wako kwenye magari yao ya vimulimuli!!!!!!
 
Back
Top Bottom