Hivi ulaya Trafiki huwa nao wanakaa barabarani kusimamisha magari?

Kule Sweden hakuna trafiki barabarani hata kidogo. Lakini kila mwendesha chombo cha anafuata sharia. Ukivunja sharia za usalama barabarani unapelekewa faini yako ikiwa na picha na eneo ulilotenda kosa kwenye address yako au hata nyumbani.
Sasa hapa Tanzania traffic wanafungua boneti kuangalia kile kidude chekundu. Huko Sweden wanakionaje hicho kidude?
 
Kwenye moja ya nchi za Ulaya nilipotembelea sikuona hiyo kasumba, but raia wanafuata nidhamu zilizowekwa...

Ktk barabara kuna njia maalumu za waenda kwa miguu, pia za waendesha beskeli, na za hayo magari. Zaidi ya 90% ya gari binafsi ni hizi gari ndogo ambazo kwetu Tz eti watu (kwa walivyoendelea kupita Europeans) wadai ni za kike!

Kukatiza barabara zipo taa maalumu kuruhusu ima watembea kwa miguu au beskeli kukatiza, ukifika wabonyeza mara zinaruhusu!

Ikitokea ajali ktk barabara fulani basi redio yako ndani ya gari itakujulisha...hata kama utakuwa wasikiliza kitu gani itabidi kisimame ili upatiwe taarifa ya ajali hiyo na hivyo kuepuka njia hiyo ili usiende tia foleni

Anayeendesha gari anamjali sana mwendesha beskeli na mtembeaji wa miguu. Gari ndo huwa kama zina macho!

Kufunga mkanda ukiwa kwenye gari yako ni lazima hakuna anayekufatilia ila ukionwa na askari wa barabara hujafunga mkanda, faini yake ni pesa ambayo thamani yake ni takriban Tsh 250,000.
 
Mi naomba tu kuuliza kwa anayejua au aliefika huko ulaya, hivi huko nako mapolice /trafik huwa wanasimama kando kando ya barabara na kusimamisha magari, na kama ni hivo je nao wanakuwa na vitabu vya risiti vya faini.
Mi sijui hii tabia naiona kama ni kitu cha ajabu yaani trafiki hamna mbinu nyingine zaidi ya kukaa chini ya mti pembeni ya barabara.
Na je nashindwa kuelewa hizo pesa za rushwa ambazo ni nyingi zaidi ya hizo zinazoandikwa huwa wanakula na nani, maana ni nyingi sana, je huwa wanapeleka mgao kwa wakubwa wao au?
Halaf kwanini trafiki wengi wanaroho mbaya sana, je wanakuwa trained kuwa na roho mbaya au ndo walivozaliwa
Ulaya traffic police utawaona barabarani mara moja kwa miezi mitatu.
 
Back
Top Bottom