N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,532
Mdau Prondo hii kitu itawasaidia sana by the way niliiona hii pia unapoingia parking area ya Ubungo plaza number plate inakuwa recognised haraka sana, badala ya tochi lukuki waweke hiiKwanza nchi nyingi za Ulaya polisi anawashughulikia wote, wenye magari na wengineo. Hawasimami barabarani ila wanakuwa kwenye magari yao maalum wanafanya patrol almost kila mtaa/barabara hadi vijijini.
Gari zao ziko fitted na system inaitwa ANPR yaani Automatic Number Plate Recognition. Humo kuna data za madereva na gari zote, gari yako ikipita system yao inasoma namba ya gari yako ndani ya sekunde inawapa jibu kama gari halina vibali au dereva hana leseni, anadaiwa au ana kosa lingine la jinai.
Mara nyingine huwa wanatega sehemu ambayo wanajua wahalifu wanapenda kutorokea. Hawakusimamishi bila kosa,aidha gari ina kasoro,wewe una kasoro au umeendesha vibaya.
Hii system sasa hivi polisi wetu wanaitumia kukamata wale wasiolipa faini, wangekuwa na magari ya kisasa ingekuwa ndani ya patrol car badala ya kukaa nayo kibandani.