Hivi Ulaya na Marekani nako Mvua ikinyesha Umeme huwa unakatwa?

Tanesco wameudhi sana, kimvua hiki si cha kukata umeme...

Hata hivyo wanatakiwa kutoa taarifa kama wanatarajia kukata umeme kila mvua itaponyesha.

Vile vile hata kama watakata umeme kutokana na sababu za dharura warushe breaking news mitandaoni, hata humu wana thread waweke taarifa tutapeana.
 
Ni kweli kabisa.
Huo ndio ukweli
Wabongo tunazo akili za kumalizia na sio za kuanzia.

Mfano mtambulishe mtanzania kwa ndugu yako yeyote hafu uishie hapo.

Akikutana na rafiki yako atamzungumzia utafikiri walijuana miaka kumi iliyopita.


Hivyo hivyo kwa kila nynja ni hivyo hivyo.

Embu fikiria mtaalamu wa majengo anaongea majengo makubwa yanapumua, kisa nyufa zimeonekana


Hivi hayo majengo pekee ndio yanayopumua?? Kisa tu kuna mtu aliwahi kuzungumzia hilo.


Njoo kwenye umeme huko utakuta vituko mkuu.

Embu fikiria ni wangapi wenye mfumo sahihi wa umeme?? Utagundua ni nyumba chache sanaa zenye mfumo mzuri wa umeme
 
1961-1776=185.
Embu fikiria huyu mtu katangulia hiyo miaka hafu inataka kulingana nae??
Hapa ndio utaona tamaa ya wabongo.
Mtu anatuzidi hiyo miaka lakini mpaka leo hii demokrasia kwake ni kitendawili, sisi huku itakuwaje??

Tumechelewa kwa sababu tulichelewa kutawaliwa.
Tulikuwa na mfumo wwtu wa maisha.




Tusipokubaliana na hali yetu tukaanza kupambana tutaumia mnoo
Mapinduzi ya viwanda China yameanza mwaka gani Na vipi nchi Kama Malaysia,Vietnam,Thailand zipo juu yetu hali kwamba miaka ya 1960 tulikuwa nao pamoja.

Na ni karne ipi ambayo nchi zote duniani zilikuwa Na karibia kiwango sawa cha maendeleo? Na kwanini gape likaongezeka hapo katikati?
 
Mapinduzi ya viwanda China yameanza mwaka gani Na vipi nchi Kama Malaysia,Vietnam,Thailand zipo juu yetu hali kwamba miaka ya 1960 tulikuwa nao pamoja.

Na ni karne ipi ambayo nchi zote duniani zilikuwa Na karibia kiwango sawa cha maendeleo? Na kwanini gape likaongezeka hapo katikati?
Niambie tuu mkuu wameanza mfumo wa vyama vingi lini mkuu??

Hapo tuje tujadili wamejikwamua minyororo ya demokrasia lini??
 
Huku temeke ndio wanakata kila Siku asubuhi mpaka mbili usiku, au jioni mpaka saa 8 ucku ni hatari sana.
 
kila kitu ulayaa ulaya lini utafanya ya kwako hao wa ulaya waseme Africaa kuna wajinga kama ulaya?
Mimi nafikiri ameuliza kwa kutaka kulinganisha na sehemu nyingine angeweza kulinganisha na Afrika ya Kusini au Zimbabwe lakini akachagua Ulaya kutokana na maendeleo na uvumbuzi mwingi wa techonolojia kuanzia huko
 
Inategemea na hali ya hewa katika mji husika. Kwenye suburbs wanakata hasa vimiji ambavyo bado wanatembeza nyaya za umeme kwenye nguzo kama huku Tz
 
Umeshasema nchi zilizo endelea. Sisi ndio kwanza tunaanza safari. Kwa hiyo tuwe wavumilivu kuna milima na mabonde. Pia torch ni nyingi mnoo.
Hivi miaka ya 1961 wakati tunapata uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe nchi kama Singapore, Malaysia, Indonesia, China, Vietnam na nyinginezo za huko Asia uchumi wao na wetu ulikuwaje? Nauliza hili swali sababu umasikini wetu mnapenda sana kuuhalalisha eti Tanzania bado ni nchi changa
 
Umenikumbusha komedi moja, wengi tunaijua lakini.

Kikwete alimtembelea Obama akawa anatembezwa aone mitaa, wakafika sehemu Kikwete akakuta jengo halina umeme.

Akavunjika mbavu kwa kicheko Obama akamuuliza unacheka nini, akajibu "Kumbe kutusumbua kote na misaada yenu mara mtupangie vya kufanya hata nyinyi umeme unakatika!!?"

Obama akajibu "Huo ni ubalozi wa Tanzania"
 
Kuna sehemu na sehemu huku ulaya au America umeme kukatika.
Inapotokea mvua na upepo mkubwa kuna sehemu huathirika sana na kusababisha umeme kukatika, lakini huwa wanafanya kila hali ili urudi kwa haraka na kuendelea na shughuli kama kawaida.

Nchi zilizoendelea zinafanya kila juhudi za kurudisha hali ilivyokuwa kama ni barabara zinapoharibika au umeme unapokatika.

Nakumbuka mwaka 2011 huko Japan baada ya tsunami kuna barabara ziliharibika lakini moja ambayo ilishika taarifa za habari duniani ilikuwa great Kanto highway ambayo iliharibika sana lakini iliwachukuwa siku saba tu kuirudisha katika hali yake na kufunguliwa rasmi.
 
Back
Top Bottom