Hivi ukitoa pesa katika ATM huwa unahesabu au unakunja unaweka katika wallet?

kuna siku network ilikuwa inazngua, sasa kuna bidada mmoja alifanya muamala ila haukukamilika kadi ikatoka, ye akaondoka ile naingia mim nikakuta machine ya pembeni inacount pesa after a seconds mihela hiyo ikatoka, nikaangalia kushoto kulia hamna mtu sema mchawi alikuwa camera tu ikabidi nimwambie mlinzi, ile natoka tu namuona bidada anarudi anasema ametumiwa SMS kuwa katoa hela
Uli fanya vema, maaan hujui hela zake hupataje na anaenda kufanyia nini.

Usione watu wanapendeza, kuna watu wana majukumu hatari
 
Sasa pata picha, umetoa laki tatu na ishirini, risiti inaonyesha ni laki tatu na iahirini, lakini kuja kuhesabu unakuta ni laki tatu kamili.

Utamdai nani.?!

Kwanza believe me, kesi za pesa kukwama kwenye ATM huwa zipo, ingawa ni chache mno. Hutokea note moja au mbili kuStuck kwenye ATM.

Kama umehesabu na umejiridhisha kuwa pesa ni pungufu, fanya mambo yafutayo.
Malalamiko hupelekwa kwenye benki husika inayomiliki ATM.
Wasiliana na benki husika, wapatie malalamiko yako katika barua maalumu (watakupatia wao) halafu watakupatia acknowledgement copy.
Bank itafuatilia lalamiko lako wakishirikiana na Idara maalumu ya ATM.
Muhamala wowote unaofanyika kwenye ATM unakuwa Recorded kwenye ATM, kwahiyo lalamiko litalinganishwa na record za system, kama lalamiko litalingana na record za system pesa huwa inarudishwa. Hiyo process huchukua zaidi ya masaa 72.


Ziada; Katika ATM, pesa ikishafika mahali ambapo huRecordiwa kabla ya kutoka nje ya mashine. Haiwezi kukwama. Pesa hukwama kabla ya kuifikia recorder.
 
doh mimacho huwa inanitoka kodo nkitoa hela tuu kwa atm machine huwa natamani kuzihesabu aseee napatwa na hofu sometimez uvumilivu ukinishinda huwa nahesabu....ela si zanguuu metoa mwenyew.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
smiles-kid.jpg
 
jenga utamaduni wa kuhesabu.

kwa sababu, atm huwa inaharibika kama vyombo/mitambo mingine,
ikiharibika na wewe itakuharibia, utakachofanya unapiga simu huduma kwa wateja na kuripoti tatizo ili uhudumiwe.

siku moja nilikuwa safarini, tarehe ya marejesho ya mkopo ikawa imefika nikiwa mbeya halafu ilikuwa weekend nikaenda kutoa hela kwenye acount ya benki ili niingize kwenye m pesa nizitume kwenye benki nyingine, mashine ikanipa risiti kwamba huduma imekamilika kutoa tsh 400,000/-
wakati imetoa risiti tu!!

kwa hiyo kuhesabu ni muhimu, ili uone kama haijakosea,
na risiti ni muhimu ili uone kama kiwango kilichoandikwa pale ndicho kilichotolewa
 
Kwa aliyezoea kushika pesa. Hata noti moja ikipungua atahisi kwa uzito wa pesa alizobeba.
 
Back
Top Bottom