Hivi ukilema ndiyo tiketi ya kuwa ombaomba?

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
577
Juzi ITV niliona Regnald Mengi akilaumu kwamba ombaomba wametengwa katika jamii kwa kukataliwa kuwa ombaomba, ati hawasaidiwi tena barabarani. Jana nimesikia tena ITV Mwenyekiti wa Vilema Tanzania akilalamika kwamba vilema wanakiona cha moto sababu ombaomba hawapati tena.

Akadai kwamba kama ni kampeni ya aina fulani isiwe hivyo lakini hakutoa mbadala wake. Mtangazaji alienda Salender bridge akaonyesha kwamba hakuona kilema hata mmoja akiomba. Wengine vilema wanalia kwamba wananyanyapaliwa hata kwenye daladala kwa hofu kwamba watu wataota manyoya ya paka mikononi.

Nimebaki na maswali mengi pasipo kupata majibu. Hivi kuwa kilema ndio tiketi ya kuwa ombaomba? Mbona kuna wakati Makamba aliwakusanya wakaundiwe kijiji ambako watapata huduma za msingi na kufundishwa jinsi ya kujitegemea wakatoroka na kurudi barabarani kuomba?

Sidhani kwamba ombaomba wanafanya hivyo kwa sababu maisha ni magumu, nadhani ni hobby kwa sababu kuna vilema wengi walio wajasiriamali makini katika fani rasmi mbalimbali, mabosi wakubwa na mamilionea. Nafikia mahali kufikiri kwamba vilema wanajiendekeza na kujidhalilisha.

Hivi ni kweli hao vilema hawawezi kujishughulisha na uzalishaji wowote isipokuwa kuomba? Hata Matonya anadai hana uwezo lakini Dodoma ana mji wa familia wenye mifugo mingi na anasomesha watoto hadi vyuo vya elimu ya juu! Lakini bado yumo barabarani kuomba akilala chali na kopo juu, huku ameminya macho kuashiria ni kipofu!
 
Back
Top Bottom