Hivi ukifa/ukifariki unachukuwa muda gani kuitwa Hayati?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Kichwa cha Habari kimejitosheleza hivyo karibuni tu " mtiririke ".

Kikubwa nataka tu kujua tofauti iliyopo kati ya Marehemu na Hayati hivyo kwa mtakaotoa UFAFANUZI si vibaya pia mkaweka na mifano ya Watu ambao wanastahili kuitwa Marehemu na wale wenye haki ya kuitwa Hayati.

Nitawashukuruni.
 
hayati ni yule aliye pata kuwa kiongozi mkuu katika nchi au heshima kubwa nchini au dunian na mazishi yake huenda zaid ya wiki, ila mtu kama wewe ambaye tunakuzika baada ya siku moja, usie na uongoz ktk nchi tunakuita marehem
 
Kichwa cha Habari kimejitosheleza hivyo karibuni tu " mtiririke ".

Kikubwa nataka tu kujua tofauti iliyopo kati ya Marehemu na Hayati hivyo kwa mtakaotoa UFAFANUZI si vibaya pia mkaweka na mifano ya Watu ambao wanastahili kuitwa Marehemu na wale wenye haki ya kuitwa Hayati.

Nitawashukuruni.
Ntakuelewesha kwa mifano 2

Nielewavyo mimi!
Katika mazishi ya Julius Kambara sikusikia jina la Marehemu likitamalaki kama la hayati
Katika msiba alitambuliwa kama Hayati baba wa taifa ,
Maana yake ni MTU aliyekufa mwili lakini mambo, ukuu,heshma yake itadumu milele, hata Leo tunamtambua hivyo.

Marehemu ni mtu aliyekufa milele, hakuacha chochote cha kukumbukwa na jamii
Kama ambavyo mkuu wangu wewe ukifa watakusifu jina la marehemu Genty
 
Labda nikubariane na mchangiaji wa mwanzo, kuwa hayati ni kiongozi tena wa kitaifa. Ila hili swala kuacha mchango kwenye jamii, sijui mchango nini, mfano: Nina nyumba sita Dar tano napangisha familia kibao zonajihifadhi pale, kabla hawajapata uwezo wa kujenga za kwao. Pamoja na nyumba hizo ni daladala tatu, na Doctor wa hosptali moja jijini. Je huyu hana mchango kwenye jamii, hata mwalimu tu askari hawana mchango kwenye jamii.
 
Ntakuelewesha kwa mifano 2

Nielewavyo mimi!
Katika mazishi ya Julius Kambara sikusikia jina la Marehemu likitamalaki kama la hayati
Katika msiba alitambuliwa kama Hayati baba wa taifa ,
Maana yake ni MTU aliyekufa mwili lakini mambo, ukuu,heshma yake itadumu milele, hata Leo tunamtambua hivyo.

Marehemu ni mtu aliyekufa milele, hakuacha chochote cha kukumbukwa na jamii
Kama ambavyo mkuu wangu wewe ukifa watakusifu jina la marehemu Genty

Mkuu kabla ya yote naomba kukuuliza Je Wewe umetokea Kagera au Kigoma au Singinda au Kondoa au Ruvuma au Pwani? Kwani katika sentensi yako ya mwishi umenipiga " dongo " la " kimtindo " hivyo naanza kwanza kwa taratibu tu kukuuliza tena kinidhamu kabisa ili nijue kama unatokea hiyo Mikoa tajwa hapo ya WATANI zangu Wakubwa kwa upande wa Mara na Mtwara " nikupotezee " ila kama hutoki huko basi " nitiririke " nawe ili tuheshimiane. Kwani ni kama vile " umeninuwia " au unapenda " nidedi ".
 
Hili sio jibu, hunajibu soma pita kimwa.

Mkuu usijisikie vibaya na hilo jibu lake kwani najua amenitania tu katika kunogesha UZI na bahati nzuri na Mimi napenda mno UTANI hivyo naburudika nae tu. Mkuu humu ndipo wengine tunaondoa " stress " zetu za hawa " vyura " wetu ambao kila kukicha wanatutesa tu huku wakiwa hawana shukurani.
 
Mkuu kabla ya yote naomba kukuuliza Je Wewe umetokea Kagera au Kigoma au Singinda au Kondoa au Ruvuma au Pwani? Kwani katika sentensi yako ya mwishi umenipiga " dongo " la " kimtindo " hivyo naanza kwanza kwa taratibu tu kukuuliza tena kinidhamu kabisa ili nijue kama unatokea hiyo Mikoa tajwa hapo ya WATANI zangu Wakubwa kwa upande wa Mara na Mtwara " nikupotezee " ila kama hutoki huko basi " nitiririke " nawe ili tuheshimiane. Kwani ni kama vile " umeninuwia " au unapenda " nidedi ".
Usitiririke ngoja kwanza
Wengine waje ututiririkie kwa pamoja maana naona majibu yanafanana fanana , sasa ukinitirikia mi mwenyewe labda kama unataka niwe mfano wengine wakome
 
:D:D:D:D:D:D:D.
 
Back
Top Bottom