Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Unakuta mtu anatoa ushauri tu, achilia mbali kukusoa lakini anayeshauriwa anavyokuwa mkali mpaka unashangaa. Sijui shida inakuwa ni nini. Na hii ipo kwa karibu vyama vyote. Viongozi, wanachama na Wadau wa vyama vya siasa husika; wakishauriwa bila kujali ubora, manufaa na msingi wa ushauri husika, wanawageuza watoa ushauri kama maadui badala ya kuwachukulia kama marafiki.
Yaani mtu anatoa ushauri tu (achilia mbali kukosoa) lakini utakavyokimbizwa huku ukipopolewa mawe; atatamani ni bora ungeweka mkono kwenye mzinga wa nyuki. Sijui shida hasa inakuwa ni nini?
Ukitaka kundi unalotaka kulishauri muende sawa (Isipokuwa wachache ambao wana utulivu wa akili), basi lisifu (Hata kama linafanya kitu cha hatari). Ukitaka mwende sawa zaidi, liahidi kwamba litaenda mbinguni na una uhakika huo;hapo sawa ila ukishauri tu bila kujali ubora wa unachoshauri, umekwisha. Yaani sijui tumekuwa watu wa namna gani.
Cha ajabu hao hao ambao wakishauriwa wanakuwa wakali kama pilipili,nao wanalaumu wenye mamlaka kwamba hawataki kushauriwa ;sasa unajiuliza kama wao wala hawana mamlaka makubwa kwa sasa ila hawasikii la kuambiwa je wakiwa na mamlaka makubwa itakuwaje?
Na hoja zinazotolewa huwa zinakuwa ni dhaifu mpaka unajiuliza ni nini hiki? Yaani inakuwa ni kama mtoto anaambiwa “hauwezi kusoma vizuri, ni vizuri kujifunza kusoma ABC kwa sababu itakusaidia kwenye XYZ”. Anayeshauriwa jibu lake ni “wewe umeniona mimi tu? Mbona huwaambii kina fulani? Mbona fulani pia hawezi kusoma ina maana yeye humuoni? N.k
Lakusikitisha zaidi, hao ndio wanategemewa waoneshe njia wengine. Ni muhimu kubadilika vinginevyo ni changamoto kubwa.
Kuna siasa fulani hivi zinazofanywa na baadhi ya vyama ambazo ni “siasa za aibu”. Tujisahihishe !