Hivi ujenzi wa barabara ya Kilwa ulitawaliwa na rushwa?

Tuyuku

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
3,292
1,919
Nimeona ni vema leo kuuliza maana hili jambo lanikereketa sana. Hii barabara imemalizika kujengwa mwaka 2008, lakini leo ukiitazama imechakaa vibaya mno. Eneo la Mivinjeni usipokuwa mwangalifu unapata ajali kirahisi sana kwa kuwa barabara imeota manundu kupindukia.

Pia ukitazama mitaro yake ingali shaghalabhaghala. Barabara tangu iwekewe minara ya taa miaka mitatu nyuma hadi leo hizo taa hazijafungwa.

Hii inaashiria nini? Kama si kuwa mradi uligubikwa na rushwa?

Mwenye ufahamu wa jambo hili atusaidie tafadhali.
 
mdau kwanza unapaswa kujua kua ile barabara ilijengwa kwa MSAADA WA PESA ZA WALIPA KODI WA JAPAN,then kampun iliyojenga ni ya KIJAPAN,serikal haikuwa na pesa hapo hata chembe,kwa hiyo usimamiz ulikua F,sidhan kama rushwa ilikuwepo ila mazngra hayo ndiyo yanaweza kusababisha hiyo hali
 
Back
Top Bottom