Hivi Ugaidi Au Uongozi Mbaya Tatizo Afrika?

Mbunge

Senior Member
Aug 7, 2008
104
9
Ndugu wapendwa Afrika Mashariki,


Kiongozi mmoja wa Marekani aliwahi kuwaambia Wamarekani wenzake kwamba kama kuna kitu cha hatari na kuogopa sana ulimwenguni sio kitu kingine ila hofu. Akawataka waiogope hofu kuliko ukoma!

Chini ya uongozi wa Bwana George Bush, hata hivyo, Marekani sio tu imeweza kuwatia hofu Wamarekani bsli pia viongozi mbalimbali Afrika wakiwemo wale wa Afrika Mashariki.

Sote tunajua kuwa hofu au kisingizio chochote cha hofu kwa Afrika ni biashara nzuri kwa polisi wa Kiafrika kufanya biashara ya rushwa na kumalizia hasira zao za kulipwa mishahara kidunchu kwa watu masikini ha kama ilivyo Kenya kwa Waislamu ambao mfumo mzima wa nchi hiyo pamoja na kuchaguliwa kwa Raila Odinga kuwa Waziri Mkuu [ambaye Waislamu wengi walikuwa na imani naye ya kuibadili hali hiyo] umejengwa kuwadhalilisha na kuwahujumu Waislamu wa nchi hiyo.

Hatuamini kuwa Wana Uslama wa Tanzania wanaweza kuwa na wivu, ubabe, uonevu na chuki dhidi ya Waislamu kama jamaa zao wa Kenya. Na kwa sababu Watanzania sio watu wenye akili fupin na kununulika kwa bei sawa na bure hatuamini kwamba watawapa polisi wanyanyasaji wa Kenya ushirikiano wowote wa kutafuta wachawi wa Ugaidi wakati mchawi mwenyewe ndio huyo huyo anayetoa kitu kidogo kwa viongozi wao ili wawakurupushe jamaa kila inapokaribia Agosti 8 ili waonekane wanafanyia kazi rushwa waliyopewa na Waibaji wakuu wa madini Kongo na wavurugaji wa amani nchini humo.

Inafaa bila kujali tofauti zetu za rangi au dini au nyinginezo kujadili 'tatizo la matajiri kuhehushwa na hofu ya ugaidi kama kweli ni tatizo letu Afrika!'

Binafsi yangu ninadhani tuna matatizo makubwa kama vile kuuawa maalbino, ubakaji tena na midubwana yenye ukimwi; watoto wetu kunyanyaswa, kuumizwa hata kuuawa wakati mwingine na mijitu isiyo na huruma wakati kuna polisi tunaowalipa mishahara; barabara mbovu na zisizopitika kwa urahisi; serikali za Kiafrika kutufanza masikini zaidi jana tulikuwa tuna magari leo tunapanda na kunyanyaswa kwenye taksi, matatu na daladala; umeme ghali tena kwa asilimia ndogo tu ya wananchi mijini; hatuoni biahsara yoyote ya maana kati ya nchi zetu; mashirika ya hifadhi, bima, mifuko mbalimbali na benki kuu kutuibia fedha zetu; watoto wa viongozi na matajiri kupewa nafasi zote nzuri za masomo na kazi wakati watoto wa walalahoi wananyanyaswa kwa mikopo ya fedha za wazazi wao wenyewe na kuwa na wakuu wa vyuo vikuu wanasesere waliowekwa na viongozi wa nchi kwa sababu wanazojua wao wenyewe; elimu na afya zimepanda bei kichaa; kwingine hatuna maji wengine hawana umeme; usafiri, vyakula na vitu kupanda bei mara kwa mara na kadhalika na kadhalika.

Ninaamini Waafrika wa Afrika Mashariki tunastahili kuwa na hofu lakini sio ya kubomolewa kwa majengo ya balozi za Kimarekani kutokana na uzembe wao wenyewe. Watamtukanaje mamba wakati wako mgongoni mwake?

Hofu yetu iwe juu ya matatizo yetu ya msingi-chakula, maji, usalama, afya, elimu, mawasiliano na mahitaji mengine ya msingi kwa watu wetu.
 
Nadhani pamoja na kwamba Afrika na hususani Tanzania tuna matatizo mengi ya kiuchumi, Sioni ni kwanini hili la ugaidi lifumbiwe macho.

Kama kweli mtu au kikundi fulani kinajihusisha na ugaidi kinastahili kutafutwa kwa gharama yoyote mahali popote na sheria ichukue mkondo wake bila kupendelewa kwa namna yeyote.

Ikiwa mtu ni gaidi ni lazima tuseme na kumchukulia hatua zinazostahili. Vivyo hivyo kwa mafisadi na makosa mengineyo. Sielewi kwanini kuwaonea huruma na kufikiri kuwasamehe magaidi wanaohatarisha maisha ya mamia/maelfu ya watu wasio na kuwaandama mafisadi.

Labda mwenzangu hajawahi kupoteza mtu anayemjua/rafiki wa karibu kwa ugaidi ndio maana anadiriki kuwatetea na kuwapata mafuta kana kwamba wanalolifanya ni sahihi.

Sote tungependa kuwa na Tanzania bora inayojali maisha ya watu, isiyo na Ugaidi,Ufisadi,Uonevu na mambo yoote yasiyofaa kwa jamii. Hiki ndicho kiwe kipaumbele kwa taifa letu. Tukianza kusema wanaofanya makosa fulani waache wasibughudhiwe tutakuwa hatuwatendei wakosaji wengine.

Siungi mkono kuwa na double standads katika swala la uhalifu. Kama mtu au kikundi fulani cha watu ni MAGAIDI, MAFISADI.....NK.SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom