Hivi ufalme wa BB(Blackberry) umeishia wapi??

Nicheki BBM


Usenge mtupu, simu ina hadi vifurushi special
Nilikua nikisikia mtu akisema hivyo namuogopa hatari, nahisi jamaa kashatoboa tayari 😁😁😁😁

Ilikua advance hapo in the early 2010s boys school bweni zima wahuni tunamsikiliza Diva. Halafu anakuambia check me on BBM na kuorganise BBM parties.

Diva ashukuriwe alikua anatupa faraja kipindi ambacho tunahitaji.
Na kipindi hiko unasikia sauti tu hata sura huijui wahuni tunabaki kumchora jinsi alivyo kwenye medulla oblongata
 
Kila zama na wakati wake mkuu! Wako wapi kina ZTE na HTC? Washkaji walikua na mashine hatari sana kwa kipindi hicho lakini nao zama zao zishapita, lakini kuna kampuni nyingi tu za simu za kisasa wanatengeneza simu zenye features za hovyo au kulingana na hiyo miamba ya wakati huo, Nokia, LG & Sony Xperia kidogo wanaenda na nyakati kimtindo..
ZTE bado wapo, wana gaming phone nzuri tu.
 
Kwa mujibu wa kitabu cha "Losing the Signal: The Untold Story Behind the Extraordinary Rise and Spectacular Fall of Blackberry" kampuni ya Blackberry, ukiachana na mambo mengine mfano: matatizo ya outage kwenye mfumo wao wa Blackberry Internet Service (BIS) uliopoteza trust ya watumiaji, mfarakano kati ya waanzilishi wa Blackberry, bei kubwa za vifurushi vya BIS (ambayo ilifanya washindwe kushindana kwenye consumer market) -- ni kupuuza tishio ambalo lilikuwa linaitwa iPhone na kushindwa kubadilishia strategy yao mapema kama walivyofanya Google (Android).
 
By the time wanastuka, iPhone imeshaaza kuchukuwa wateja wao wa Kibiashara pamoja na wale wa kawaida. Ndipo wakatoa simu yao Blackberry Storm (pichani) kama jibu lao la iPhone, lakini kutokana na matatizo ya ndani ya kampuni; simu hiyo ilikuwa Ina matatizo juu ya matatizo. Kuanza kuharibu heshima yao iliobaki.

Na kufikia 2009 simu nyingi za Android kutoka HTC, Motorola na Samsung zikaanza kutoka, na hapo ndipo blackberry ilipoanza kufa.

images%20-%202021-01-16T132912.716.jpg
 
Back
Top Bottom