Hivi uendeshaji sekondari za serkali zinagharimiwa vipi?

Omulangi

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
1,036
265
Serkali iliondoa karo kwa wananchi na michango kwa wananchi ili kuwezesha elimu ya sekondari iwafikie wengi hairuhusiwi kuchangisha wazazi ila tu kwa kibali maalum toka wizarani. Ruzuku serkali iliyoahidi ya uendeshaji hadi sasa haijatolewa ( nina uhakika kwa shule za mikoani nisijue huko mijini) Sasa hizi shule zinaendeshwa kwa miujiza gani?
 
wizara hutoa pesa kidogo. Ada inayotozwa hubaki shuleni kusupplement pesa ya wizara. Hii pia inatokea ktk vyuo vikuu ndio maana wanawakomalia wanafunzi walipe pesa ya ziada. mfano kama mtu amepewa mkopo na Loan Board wa 60% basi 40% inayobaki inatakiwa ilipwe chuo moja kwa moja.

kwa sababu ya ufinyu wa bajeti sekondari nyingi za bweni huwomba wazazi wachangie say gunia moja la mahindi kwa kila kichwa.
 
Shule nyingi zina kabiliwa na madeni makubwa hasa kwa upande wa wazabuni ambao husambaza vyakula mashuleni. Hata hivyo pamoja na serikali kufuta michango bado michango hiyo ina endelea kwa kiasi kikubwa.

Fedha zinazotolewa na serikali ni ndogo na hazitoshelezi mahitaji muhimu. hivyo wazazi hutakiwa kuchangia michango kati ya 60,000 hadi 100,000 kwa mwaka.

Kusema kweli sasa hivi shule za serikali zimebaki majina tu, ila ilemi inayotolewa ni ubabaishaji mkubwa. Nyingi zinakabiliwa na ukosefu wa walimu pamoja na vifaa vingine vya kufundishia kama vitabu na vifaa vya maabara.

Nina mdogo wangu anasoma Tabora boys, PCM hawana walimu wote wa PCM. wamekuwa wanafundishwa na walimu wa o-level na wakati mwingine huambiwa wachange pesa ili kumlipa mwalimu kutoka mirambo aje kuwafundisha hesabu.

Yaani ni kero tu. Mimi nilifika mahali nikaamua akae tu DAR asome tuition ili baadae aende tu kufanya mtihani. Niliamini akaikaa DAR ataweza kujifunza zaidi kuliko hata shuleni. Hata hivyo mkuu wa shule alikataa akasema kama hatafika shule basi atafutwa.

Kwa kweli Elimu tunaichezea kwa kiasi kikubwa. Sijui tunajenga jamii ya watu wa aina gani hapo baadae.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom