Hivi ubunifu na vipaji ni kosa la jinai tanzania+afrika kwa ujumla?

Balozi Chriss

Senior Member
Jan 21, 2011
153
16
Kwa waliofuatilia Taafifa ya habari ktk television yaTBC1 ni dhahiri kabisa tumeona kuwa kuna Kijana anaitwa Petro a.k.a.Mzimu ambaye ni mkazi wa Kigoma,ambaye amekamatwa na mtambo wa kutengeneza silaha aina ya gobore.Kweli mimi nimemtukuza Mungu kwa kumpa kipaji kama kile cha kipekee kijana yule wa kitanzania.
Lakini kk jambo la kunishtua ni jinsi ambavyo hawa mapunguani ambao wamepewa dhamana mbalimbali maofisini jinsi ambavyo wanafurahi kumtia mbaroni kijana huyu na dhahiri wakionekana ni lazima wamtie gerezani akateseke huko..
Hivi ipo wapi au zipo wapi zile taasisi za kushughulikia vipaji?Vijana kama hawa ni wengi sana mitaani na kutokana na uzembe wa serikali zetu toka tupate uhuru,hawajawaandalia mazingira muendelezo watu wa aina hii.
VIWANDA vyetu vyote vimejaa wageni na bidhaa zetu nyingi ni za nje.
Unadhani kama Kijana Petro angewezeshwa ,ni aina ngap ya silaha za kijeshi angetengeneza?JAMANI nashindwa kuendelea kuandika hili dukuduku....
 
Unajua bongo hii tunapenda sana kukumbatia mawazo ya wenzetu kuliko kuthamini yetu.
Kama angekuwa anaishi USA leo hii angepewa scholarship M.I.T . Na wasiojua, teknologia hii ilianza enzi za Kina mtemi Mkwawa. Baada ya wakoloni kuchukua nchi wakaona itakuwa hatari kwa wenyeji kumiliki teknolojia kama hii maana ingehatarisha utawala wao. hivyo wakaweka sheria za kupiga marufuku viwanda vya asili kama hicho cha kuzalisha magobore. Bahati mbaya kwakuwa viongozi wetu tuliwapa dhamana hawakuwa/hawana na muda wakupitia sheria kama hizi, leo hii ndio tunashuhudia vitu kama hivi.
Nadhani imefika wakati muafaka wa watunga sheria kuangalia suala kama hili. Na vilevile taasisi zetu kama SIDO, VETA, D.I.T, UDSM( College of Engineering science) na nyinginezo kuwatumia watu wenye vipaji vya asili kama hawa
 
Mkwawa na askari wake walikuwa wanatengeneza bunduki siku nyingi tu. Ndio kisa mjerumani alikiona cha moto pale Iringa. Ni vizuri wenye vipaji hivyo wa endelezwe. Ndio chanzo cha nchi kama China,France na Russia kuwa na bunduki zao na ndege zao za kivita.
 
kwa mfano mm nina utaalamu wa kutengeneza mabomu from household equips..., je, nikiwa nayatengeneza ntakua nadhihirisha kipaji(uwezo) changu au ntakua nafanya kosa kisheria??
 
kwa mfano mm nina utaalamu wa kutengeneza mabomu from household equips..., je, nikiwa nayatengeneza ntakua nadhihirisha kipaji(uwezo) changu au ntakua nafanya kosa kisheria??

Kama huna uhusiano na Hezibolaa, Alqaeda au Hamasa, hakuna shida yoyote!
 
Kwa waliofuatilia Taafifa ya habari ktk television yaTBC1 ni dhahiri kabisa tumeona kuwa kuna Kijana anaitwa Petro a.k.a.Mzimu ambaye ni mkazi wa Kigoma, ambaye amekamatwa na mtambo wa kutengeneza silaha aina ya gobore. Kweli mimi nimemtukuza Mungu kwa kumpa kipaji kama kile cha kipekee kijana yule wa kitanzania....
Inawezekana alikuwa akitumia hizo gobore kwa njia za kiharifu, na kisheria unatakiwa kuwa na leseni ya umiliki wa siraha za moto.

kwa mfano mm nina utaalamu wa kutengeneza mabomu from household equips..., je, nikiwa nayatengeneza ntakua nadhihirisha kipaji(uwezo) changu au ntakua nafanya kosa kisheria??
Ukiwa na utaalam wa kutengeneza vitu hatari na ukawa unavitengeneza bila ya serikali kukupa ruhusa ni kosa la jinai, na ukikamatwa unashtakiwa kwa kuhatarisha usalama wa raiya na nchi kiujumla kwa sababu serikali haijui baada ya kutengeneza uko lengo lako ni nini, labda unawauzia wavuvi haram wanaotumia miripuko au majambazi n.k
 
Back
Top Bottom