Hivi tutawapoteza watu wetu wa karibu mpaka lini kisa Pesa.!?

Mimi kuna rafiki yangu ameniomba nimkopeshe pesa lkn kwa kutambua atasumbua kunilipa niliamua ni muahid ntampa. Ilipofika siku nikakataa kumpa aisee huwezi amini amenichukia adi sasa ivi. Imekua km ni ma adui ss. Wakati alikua rafiki yangu wa karib kbs.
Au nlikosea ndugu zangu?
We una miaka mingapi mkuu?😅😅😅
 
Angalia hii para 1 ulivyoandika:
ukweli hili suala limenifika shingoni, kadri muda unavyozidi kwenda naona khali inazidi kuwa mbaya, na hii tabia inazidi kuota mizizi mno, yaani sahii ukitaka uwe na uadui na mtu wako yeyote yule wa karibu wala hata usitumie nguvu kubwa, wewe ihusishe tu PESA.
Mtu wa karibu anaweza pia kuwa mpenzi. Au nasema uongo Carleen? 😂😂😂
BAK hii haina uhusiano na mapenzi kabisa..!!
 
Nimejifunza roho mbaya kwasababu ya watu wasio waaminifu kwenye kulipa madeni mtu anakuja mikono nyuma na shida ilhali anajua kabisa na wewe upo juu ya mawe unajitolea kumdhamini kwa mtu akipewa hela kurudisha majanga anakuachia msala. Nitasaidia ndugu yangu wa damu ambaye najua hata nikifulia hanitupi au mpita njia najua nakua nimetoa sadaka ila rafiki sisaidii asilani bora urafiki uishe. E, S, N mlichonifanya kunibebesha madeni ya mamilioni ya shilingi na kuniacha nilipe nimewasamehe ila sitakuja kuwasahau na mmenifundisha kitu.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app

PAIN changes people.

-Kaveli-
 
Angalia hii para 1 ulivyoandika:
ukweli hili suala limenifika shingoni, kadri muda unavyozidi kwenda naona khali inazidi kuwa mbaya, na hii tabia inazidi kuota mizizi mno, yaani sahii ukitaka uwe na uadui na mtu wako yeyote yule wa karibu wala hata usitumie nguvu kubwa, wewe ihusishe tu PESA.
Mtu wa karibu anaweza pia kuwa mpenzi. Au nasema uongo Carleen? 😂😂😂
Nguvu ya Carleen imemshinda BAK
 
Roho inauma jamani hii dunia😭😭😭😭😭😭mtu hakulipi hana hata wasiwasi unamkumbusha mpaka unaona noma wapi hashtuki nimelost tena 300k kwa jamaa tena ni mkubwa kwa cheo kwangu anapokea kwa mwezi take home ya mill 3 na nusu kakataa kunilipa anarukisha mwezi wa pili sina raha kwa kweli we acha roho inauma sana then anabet na kulewa tu
Nilitaka kuwafanyia suprise wazazi ka hela kangu kuwanunulia chochote eid kubwa mwezi wa saba

Kama kuna mtu umemkopa rudisha kwa kweli jamani mi sina raha kabisa jmaa hajibu text siku mbili nilikuwa out of office naumwa pesa imeingia trh 25 kagoma eti ntakupa leo 28 wapi 😭😭😭mungu niongoze zaidi maana kukopa sijwai
 
Pole mahondaw ila nimecheka huko mbele ulivyomuwahi pia..!
Navyokwambia mpaka leo hii tunapigiana simu kama kuna tatizo la kifamilia tu ambalo ni lazima kama ndugu kujulishana! Sasa ilipopita tarehe 30 sasa alipotaka kwenda kulipa ada benk akanipigia kunikumbusha nikamwambi tu mwezi huu mambo yamekua mengi dada nimekwama kidogo weeeee alilalamika mpaka. Makusudi tu nikamkumbusha ileee nilomkopeaga kalipa kidogo akamute ikanicost kuimalizia mimi mwenyewe afu ilikua nyingi sasa weeee aliongeeaa aliongeaaa wewe umeninyea wewe nimefua mikojo yako jamani!!!
 
Ninashukuru Mungu huwa nina roho ya kisultani Son of Gamba..!!
Basi kama ni kweli, you are one in a million.
Women loves money and money makes women crazy, I mean 99.99999% of women are crazy about money.

A woman can marry or divorce because of money.
A woman can kill or make babies because of money. If you are not one of them, then you blessed.
 
Hiv wimbo ya Ali kiba na Barnaba wa Cheketua mbona mnajifanya kama hamjaskia?Bonge ya jiwe
Samahn mleta mada.
Ila usiogope kupoteza au kupotezewa.ni kawaida tu kwenye maisha
 
Nimeona hii post roho ikaniuma sana jamani mie nimedhulumiwa pesa ndefu mno na rafiki jamani,ameishia kuniblock kabsa,sasa sijui watu kama hawa tunadeal nao vipi!
Pole saana, mwachie ili upate amani, tena msamehe tu.

watu wa hivyo nahisi huwa wana roho flan mbaya, afu wao wanajiona ndo wajanja, wabinafsi sana.

Huwa hawaumii wala hawawazi juu ya Hilo.., we ndo unawaza.
 
Hili suala ni gumu saaana.

Hatujitoshelezi wenyewe kwenye maisha haya, lazima tuhitaji watu wengine kushirikiana nao.

Itatokea tu uliowaamini watakuumiza katikati ya mashirikiano hayo. WALA USIUMIE maana ni mapito tuu, hata usikome maana kama hujapata wewe, basi kapata yeye.

Rafiki yangu saana, classmate toka primary mpaka chuo tulikuwa roommates, niliamini tunapendana sana nilimtegemea kuwa nina mtu wa kunisaidia ninapokuwa na shida. Baada ya chuo akawa anafanyia kazi sehem ambayo kila akiwa anaenda home lazima apitie mji niliopo, tena analala kwangu ndo kesho yake anaenda. Siku amepata msiba nyumbani, katikati ya mwezi, akaniomba nimkopeshe laki mbili tu mwisho wa mwezi atairejesha, kusema ule ukweli wa moyoni sikuwa na ile pesa Ila tuliitafuta wote, nilivaa lile tatizo kama langu, nikaipata nikampa ile hela. akaenda msiba wakati anarudi akapitia kwangu ndo akarudi kazini kwake..., sikuwahi kumwona tena imepita miaka 6 sasa. Nilipiga simu, nimeandika sms zote, mpaka nimetumia watu wengine hakuwahi kurespond, nikailipa ile hela.

Miezi kama miaka miwili tangu anikope, akaja kunitafuta, nilifurahi saana, maana niliona huenda urafiki wetu utarudi tena, sikuitaka ile hela tena mana niliona kama ilitutenganisha. Kumbe siku hiyo jamaa ana shida ya elfu 30, Kwa txt aliyonitumia niliona ana shida mno, nikampa tena. hiyo aliirudisha japo kwa mbinde lakin baada ya hapo akaingia mitini tena.

Nimemsamehe kabisa, lakin nafikiri hata yeye hajisikii vzr huko aliko, nataman itokee namna tulisahau hilo deni ili maisha yarudi kama mwanzo lakin imeshindikana.

Wapili rafiki wa ukubwani, huwa namkopa saana, tena naamini Mimi ndo niliyemkopa saaana kipindi flan cha maisha, siku amekuja na shida kubwa, na alikuwa anajua kuna project naifanya, akaniomba nimkopeshe kiasi flan, kwamba mpaka ifike stage flan ya project pesa itakuwa imesharudi ili niendelee na mambo yangu. Pesa aliyochukua alikuwa anatengenezea gari yake iliyokuwa inafanya biashara. Nilimpa, gari ikapona ikaendelea na biashara, lakini pesa haikuwahi kurudi.

Namwona kabisa pesa ya kunilipa anayo lakini hanilipi, nakasirika mpaka mwisho wa hasira lakin sina cha kumfanya maana hatukuwa na maandishi. Nimeona niache tuu.

Scenarios zipo nyingi, kwenye zote huwa napata amani moyoni ninapoikumbuka dhamiri yangu kipindi naitoa pesa.

Tabia za mtu Mimi zisinihusu, japo inaumiza lakin ukijifundisha kuachana nayo unaweza kusahau na kuendelea na maisha.

CHA KUSHANGAZA, HUACHI KUWA NA MARAFIKI WENGINE NA MNAENDELEA KUKOPESHANA.
 
Hahahaha poleni Sana sameheni madeni yenu Mimi niliamua kusamehe wote ninaowadai na hawanilipi


Sasa hivi hela sikupi hata uwe mpenzi wangu..nafuu Nile


Acha tu niwe na roho mbaya niwe mbinafsi maninaView attachment 1794593View attachment 1794595
Umesomeka Mura,Ila kwenye roho mbaya kuliko kote Ni taasisi pendwa mnazoziskia,huko Kuna maajabu,huwezi amini kuwa hao ni wasomi pendwa na wenye distinction kibao,hao watu Ni hatari kwa nchi.Afrika ina laana,ndo maana wachina hawataki kitu kinaitwa chotara,mzungu,yeye na blood line yake pekee
 
Pole saana, mwachie ili upate amani, tena msamehe tu.

watu wa hivyo nahisi huwa wana roho flan mbaya, afu wao wanajiona ndo wajanja, wabinafsi sana.

Huwa hawaumii wala hawawazi juu ya Hilo.., we ndo unawaza.
Wahasibu wa nchi hii pamoja serikali yetu,wanatakiwa washtakiwe,ni watu wako kama allien.Mnaambiwa mlime soko hawaonyeshi,wadhabuni mkiona wanaumwa jua wazi wametapeliwa na mfumo
 
Hii mada nimeipitia imenipa moyo na mimi
Kuna mtu alinikopa pesa nikajua yupo vizuri atanilipa kwa mda kwa kua bznez zake nazijua
Kuja kushtuka mpaka anakuja kunikopa kumbe alikua cornered
Sasa hv napewa viswahili kila leo
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom