Hivi tuseme ukweli, kati ya CCM na CHADEMA ni nani hasa chama imara cha siasa?

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
CCM pamoja na historia ndefu ya kutokea TANU, Pamoja na kwamba ipo madarakani miongo kadhaa, haijui maisha nje ya utawala, bado ni chama dhaifu sana kiasi kwamba hakiwezi kusimama chenyewe bila kubebwa na baiskeli ya wagonjwa ya Polisi, msukumaji usalama wa taifa. Haiwezi kufanya chochote bila mkono mmoja upo daima kwenye fuko la Hazina.

Angalia wanaume wa shoka pale ufipa. Daima wanatafutiwa kesi za kubambikizwa, viongozi wake mara wanafilisiwa na akaunti zao kufungwa na TRA. Mara miradi yao inavurugwa. Yaani ni mpambano muda wote.

Kiongozi wa CCM usipoangalia, hata mjumbe utapigiwa saluti na polisi. Viongozi wa CCM ni mayai mayai. Mambo mteremko.

Wala huhitaji kuhangaika kujua vyama wafuasi wa CCM. utaona chama cha upinzani lakini kinabebwa na polisi. Fedha ya ruzuku nje nje. Hakuna kesi wala mikwaruzo.

Katika mazingira haya, CCM wala siyo chama cha siasa. Ikijitenga na na madaraka tu, inakufa. Haifui dafu hata chembe kwa CHADEMA
 
CCM ikifa Mali mtaridhi nyie Chadema au TLP na CHEYO.

Mshawishi CCM waandike wosia
 
Mkuu upo sawa ni wachache Sana wanaojua ccm au wengi wanaoijua ila hawajui maumivu ya ccm katika upatikaji wake , Wana TANU NA ASP ndo wanajua maumivu na bahati mbaya wengi hawapo na waliobaki wamekua wazee Sana

That's vijana wengi wa ccm hufanya Mambo ya ovyo maana hawajui maana ya kuitafuta haki ,wamekuta ccm ipo wamedandia kutafuta miteremko, ni Kama Kama kuku wa kizungu ukimtoa Marekani akija Afrika anawika mda na saa ambazo sio za Marekani, unashangaa kuku anawika saa sita usiku akifili ni saa 11 hasubui, usumbufu tu

KWA uzoefu CHADEMA IPO JUU, sisemi kisa ni mwanachama hapana ,
 
Twaha__Mwaipaya_on_Instagram:_“Kumekucha_Chadema”%22_.jpg
Twaha__Mwaipaya_on_Instagram:_“Kumekucha_Chadema”%22_.jpg
 
CCM ikifa Mali mtaridhi nyie Chadema au TLP na CHEYO.

Mshawishi CCM waandike wosia
CCM ikifa, TLP na Cheyo watalia. Si ndio humchagua mgombea wa ccm wa urais kuwa ndio mgombea wao
 
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli,!

CHADEMA wamesambaza mitandaoni vijana wa kumtetea Mbowe.

Kazi yao ni kuwapumbaza wanachama na wananchi kwa ujumla waone tatizo la CHADEMA ni Magufuli wakati Magufuli hayupo na hakuwahi kuongoza chadema . Kila uzi humu JamiiForums lazima vijana wa Mbowe wataje na kutukana mwendazake!

Mwenyekiti na aliyekabidhiwa usukani wa kuiongoza CHADEMA ni Mbowe lakini hawataki aulizwe chochote.!!!

Kutokana na CHADEMA kufa kila mahali kwa kupoteza mvuto na kukimbiwa na madiwani na wabunge ,viongozi wamebuni mbinu ya kukwepa aibu hii kwa kujificha kwa hayati rais Magufuli!

Viongozi wa CHADEMA wakihojiwa kwa nini chama hakina ofisi watakujibu tatizo ni Magufuli.

Tundu Lissu akiulizwa kuwa yeye ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA lakini kwa nini hafanyi kazi za Chadema? Bavichaa watakujibu chanzo ni Magufuli!

Bavicha ukiwauliza kwa nini kamati kuu ya CHADEMA wanafanyia vikao vyao kwenye hoteli za kitalii na kuacha ukumbi wa ufipa ? Utajibiwa tatizo ni hayati Magufuli!

CHADEMA wakiulizwa kwa nini kwenye uchaguzi mliwatosa makada wenu waliokipigania chama, mkabadili gia angani na kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame (orodha ya chadema ya mafisadi wakuu wa nchi )? Utajibiwa tatizo ni mwendazake!

BAVICHA na vijana wote mliosambazwa mitandaoni kumtetea Mbowe ,tambueni anayepaswa kuulizwa kuhusiana na mabaya na mazuri ya CHADEMA ni Mbowe na Tundu Lissu hao ndio viongozi wenu mliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa sasa.

Hayati Rais Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa chadema ,hivyo kukaa mnamhusisha na kuporomoka kwa chama chenu ni kupoteza muda na kuonyesha uzwazwa wa hali ya juu.

Kuporomoka kwa CCM wataulizwa Samia na Chongolo na lazima watoe majibu kwa sababu wao ndiyo viongozi wa CCM kwa sasa.

Kwanini nyinyi hamtaki kupata majibu kwa Mbowe badala yake mnataka majibu yatoke kwa Magufuli?
 
Back
Top Bottom