Hivi Tundu Lissu ni adui wa nchi au adui wa CCM?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,110
2,000
Hivi Tundu Lissu ni adui wa nchi au adui wa CCM?

Mimi MAHANJU kama mwanajukwaa huru wa muda mrefu ndani ya mtandao huu kuna kitu nataka kusema kwa wanajukwaa wenzangu humu;

Nimejaribu kufuatilia kwa makini kabisa malamiko, matusi na kejeli zinazotolewa dhidi ya mwanasiasa maarufu nchini na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mh Tundu Lissu, ni malalamiko yanayotolewa na wanaCCM peke yao tu, kwamini malalamiko yatolewe na makada wa Chama cha mapinduzi peke yao? CCM peke yao ndio wana uchungu na taifa kweli?

Kwanini mbona hatuwasikii wananchi wazalendo wasiokua na itikadi zozote wakilikemea hili? Ni kwanini CCM tuu? CCM wanafaidika nini na mfumo iliopo?

Hii inatupelekea tuanze kupaisha mawazo yetu sisi tusiokua na vyama vya siasa kwamba huenda hao hao CCM wanafahamu ni nani aliyemshambulia Lissu?

CCM wasijifichie kwenye koti la Uzalendo kumtutusi na kumkejeli mtu ambaye kila mtanzania anajua mchango wake kwa taifa, CCM wameshindwa nini kukaa kimya na kusikiliza kero za wananchi waliowapa ridhaa kwenye uchaguzi mkuu wakaachana na maneno yake majukwaani?

2010-2015 serikali ya awamu ya nne ilikuwepo na Tundu Lissu alikuwepo, kuna mahali Tundu Lissu alizuia serikali kutimiza wajibu wake? Kuna mahali Tundu Lissu alikua na mikataba ya kimaslahi na wazungu? Kuna mahali Lissu alizuia miundo mbinu ya bara bara kujengwa!

Ninachofahamu mimi ni kwamba Tundu Lissu alikua msaada mkubwa sana ndani ya bunge letu na spika wa wakati huo Mama Makinda analijua hili na nadhani aliumia sana aliposikia shambulio lake. Enzi hizo kulikua na CCM iliyoweza kuhimili siasa za majukwaani, hoja zilijibiwa kwa hoja na sio hoja kwa kuumizana.

Tusidanfanyane kwa kuwafanya watanzania kua ni wajinga kwa wanaCCM kujifichia ndani ya koti la Uzalendo wa nchi, Mwalimu wangu mzee Rwaitama alisema mnajifanya kushindia mashati ya chama kutwa nzima hakuna kitu , awamu hii chini ya sasa hakuna mwenye uwezo wa kuhimili siasa za majukwaani,vifua hivyo hakuna.

Ni mawakala wa Shetani tuu ndio wanaoweza kufikiria kutoa uhai wa wengine ndio kupumua kwao, ni roho ya ibilisi anayefikiria kuondoa nafsi au kumwaga damu ya mwingine itamsaidia yeye alale usingizi. Ni dhambi kubwa sana iliyobadili roho za watu kua nyeusi tii kua mithili ya mkaa wa jikoni.

Anayetekeleza haya atakufa na hiyo roho na moto wa jehanama utamuunguza milele na hawezi kukwepa kwa sababu ya tamaa za kidunia.

Tundu Lissu ni adui wa nchi au adui wa CCM?
 

Mwami Ntale

Senior Member
May 26, 2018
167
250
Kusema ukweli, jambo pekee ambalo linawapa CCM majuto ni kitendo cha Lissu kubaki na uhai wake mpaka Sasa! Hawajutii hali mbaya ya kiuchumi, kuporomoka kwa shilingi ya Tz, ukosefu wa ajira, kuongezeka kwa umasikini wala hawajali jinsi watoto wetu wanavyokaa chini kwenye madarasa yaliyojaa vumbi.
Hoja za kejeri na matusi wanayotoa dhidi ya Lissu vina lengo la kumkatisha tamaa ili asiendelee kusema yale yanayoendelea nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,772
2,000
Kitu cha msingi ni kuwa Tundu Lissu asiwe kipaumbele kikubwa cha Serikali kwa sasa kwa yale anayoyasema mpaka Serikali ikapoteza uthubutu wake katika kuliletea Maendeleo Taifa letu. Lengo la Lissu ni kuiondoa Serikali kwenye mstari kwa kutengeneza kashfa za kubumba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom