FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,792
- 5,373
Najaribu kuwaza na kuwazua mimi kama FL1 ..sioni tunapokwenda ...lakini tunapotoka najaribu kukumbuka..
Nikianza kuwaza matokea mabaya ya watoto wetu yaliyopita ..sisi kama wazazi tumejifunza vip juu ya hili..
Naikumbuka sana elimu ya zamani waliyo soma mababu na baba zetu ..
Kipindi kile watoto ambao walikuwa fresh or cream walikuwa wanachukuliwa moja kwa moja na serikali na kupata mwongozo mzuri kabisa kielimu..na wale basi waliofeli ndio wataingia katika Private skuli.. ambazo sasa zinaanza na St.FL1 St. Kikwete ,St.JF
Lakini sasa mambo yamegeuka na kuwa Sivyo ndivyo ..
watoto wote wazuri wanachukuliwa na kupelekwa St. St na wale akina sisi ndio tunaendelea kubanana Sirikalini...kwenye huduma hafifu kielimu
Nikiendelea kuwaza sasa kuna shule hizi za kata ambazo utakuta shule ina mwalimu mmoja au wawili madarasa ndo usiseme Lakini Sijui kama serikali ipo na inaona .
ndani ya hizi Shule najaribu kuwaza ...watoto wa mawaziri ,Rais ,Wabunge na watu wote walio na uwezo na nyadhifa mbalimbali hawawezi kusoma shule hizi za kata sijui tarafa ..wanazosoma watoto wetu walalahoi..
Naendelea kuwaza zaidi ..
Ni afadhari akina sisi kidogo kuna baadhi yetu unaweza kumtoa mwanao katika shule hizi za Serikali na kumkimbiza katika mojawapo ya St. St. ajipatie elimu bora kwa maisha yake baadae
Je tunakwenda wapi jamani nisaidieni mwenzenu mbona nasikia uchungu na kizunguzungu na nchi hii..
Kura za maoni bado zinaonyesha chama chetu kinaongoza kwa kishindo pamoja nawatu walio katika chama hiki kuboronga na kuendelea kuboronga vibaya sana ..
naumwa mie FL1 naumwa hofu na mashaka juu ya nchi.......