Hivi tunatoka wapi na tunaenda wapi kielimu....

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,373
Najaribu kuwaza na kuwazua mimi kama FL1 ..sioni tunapokwenda ...lakini tunapotoka najaribu kukumbuka..
Nikianza kuwaza matokea mabaya ya watoto wetu yaliyopita ..sisi kama wazazi tumejifunza vip juu ya hili..
Naikumbuka sana elimu ya zamani waliyo soma mababu na baba zetu ..
Kipindi kile watoto ambao walikuwa fresh or cream walikuwa wanachukuliwa moja kwa moja na serikali na kupata mwongozo mzuri kabisa kielimu..na wale basi waliofeli ndio wataingia katika Private skuli.. ambazo sasa zinaanza na St.FL1 St. Kikwete ,St.JF

Lakini sasa mambo yamegeuka na kuwa Sivyo ndivyo ..
watoto wote wazuri wanachukuliwa na kupelekwa St. St na wale akina sisi ndio tunaendelea kubanana Sirikalini...kwenye huduma hafifu kielimu
Nikiendelea kuwaza sasa kuna shule hizi za kata ambazo utakuta shule ina mwalimu mmoja au wawili madarasa ndo usiseme Lakini Sijui kama serikali ipo na inaona .
ndani ya hizi Shule najaribu kuwaza ...watoto wa mawaziri ,Rais ,Wabunge na watu wote walio na uwezo na nyadhifa mbalimbali hawawezi kusoma shule hizi za kata sijui tarafa ..wanazosoma watoto wetu walalahoi..
Naendelea kuwaza zaidi ..
Ni afadhari akina sisi kidogo kuna baadhi yetu unaweza kumtoa mwanao katika shule hizi za Serikali na kumkimbiza katika mojawapo ya St. St. ajipatie elimu bora kwa maisha yake baadae

Je tunakwenda wapi jamani nisaidieni mwenzenu mbona nasikia uchungu na kizunguzungu na nchi hii..
Kura za maoni bado zinaonyesha chama chetu kinaongoza kwa kishindo pamoja nawatu walio katika chama hiki kuboronga na kuendelea kuboronga vibaya sana ..

naumwa mie FL1 naumwa hofu na mashaka juu ya nchi.......

jipu la kwapa hili mama, ukiinua mkono linauma ukishusha mkono linauma...............
 
Hayo uliyosema Sisy FL1 yanaukweli mtupu lakini hatma yake itakuwa kama kuimba wimbo wataifa sidhani kama kutatokea solution as time goes by its becoming even worst kwenye sekta ya elimu.
 
Hayo uliyosema Sisy FL1 yanaukweli mtupu lakini hatma yake itakuwa kama kuimba wimbo wataifa sidhani kama kutatokea solution as time goes by its becoming even worst kwenye sekta ya elimu.

Ndo maana wenzetu na wenye uchungu na nchi zao wanafanya mapinduzi..nimejaribu kujiuliza wanafanya hivi kwanini...inatokana na mambo haya haya kukosa imani na viongozi
 
Hayo uliyosema Sisy FL1 yanaukweli mtupu lakini hatma yake itakuwa kama kuimba wimbo wataifa sidhani kama kutatokea solution as time goes by its becoming even worst kwenye sekta ya elimu.

Na ndio maana tunasema Tanzania ni taifa linalokufa taratibu...a slowly dying nation. Ukiua Elimu na kisha ukaacha hata utamaduni wako na lugha yako ukafuata kila kitu cha kigeni kuendelea ni ndoto.

Angalia mataifa yote yaliyoendelea iwe miaka 1000 iliyopita au hata miaka ya karibuni kama China, India na Korea. Wametunza utamaduni wao (CULTURE) na wamewekeza kwenye rasilimari watu...yaani elimu!

Sisi tuna viongozi wanaoweza kusafiri masaa zaidi ya 24 kwenda kubembea na kupiga picha na wanamichezo maarufu. Halafu baada ya hapo unamwomba msaada wa kuja kufundisha riadha Tanzania! Yaani akili zetu zimedumaa, zinawaza kuomba omba tu, badala ya kujikombia kiuchumi!
 
Binafsi naona elimu yetu imepanuka zaidi na changamoto ni jinsi ya kukabiliana na upanukaji huoo kwa kuwa na mipango bora na imara.

Kwa sasa vijana/watoto wengi zaidi wanapata nafasi ya elimu kuanzia msingi, sekondari mpaka vyuo. changamoto ya ubora hasa kuwa na walimu wa kutosha na waliofuzu vema kwa malipo ya kuridhisha, makazi bora na miundo mbinu ya kuvutia pamoja na zana za kufundishia badoo ni swali pevu kupata majibu kwa wakatii.

binafsi nimefarijika sana na upanuzii wa elimu na matokeo yake ni changamoto ya wadau wote serikali ikiwa ndio kiongozi .
 
inaumiza sana jamani, wengi wetu ndio tunapata madhara haya maana hatuwezi kulipia hiyo elimu bora. tunaendelea kutanua lile duara la umasikini (poverty cycle)

the other day Masaki I trust you red about mwl Hassani wa huko sijui Rufiji
bado najaribu kufikiria future ya wale watoto baada ya elimu wanayopat
aaaaaaaaaaaahhhh bwana wee ngoja tuendelee kuwa mzoga unaotembea....
 
Thanks Nyauba ni kweli Elimu imepanuka lakini je huoni kama shule za serikali zinatakiwa ziboreshwe zaidi hata sisi wenye maisha ya chini tuweze kuwa na imani na elimu za watoto wetu..
Je huoni kwamba mazingira yanatufanya tuwaache waendelee kusoma shule hizi kwa vile uwezo wa kuwatoa huko hatuna ??
 
Na ndio maana tunasema Tanzania ni taifa linalokufa taratibu...a slowly dying nation. Ukiua Elimu na kisha ukaacha hata utamaduni wako na lugha yako ukafuata kila kitu cha kigeni kuendelea ni ndoto.

Angalia mataifa yote yaliyoendelea iwe miaka 1000 iliyopita au hata miaka ya karibuni kama China, India na Korea. Wametunza utamaduni wao (CULTURE) na wamewekeza kwenye rasilimari watu...yaani elimu!

Sisi tuna viongozi wanaoweza kusafiri masaa zaidi ya 24 kwenda kubembea na kupiga picha na wanamichezo maarufu. Halafu baada ya hapo unamwomba msaada wa kuja kufundisha riadha Tanzania! Yaani akili zetu zimedumaa, zinawaza kuomba omba tu, badala ya kujikombia kiuchumi!

thankx Masaki inauma sana inauma...
 
We F1 ulisoma st.? si ulisoma kwa kina Kayumba?
Tatizo wazazi wengi wanawapeleka watoto wao st. alafu huku kwa kina Kayumba wanakufumbia macho na hawakupi msisitizo bora yeisheeeeeeeee ndo hapo chacha tutakuwa na taifa mbumbumbu miaka 20 ijayo.
 
inaumiza sana jamani, wengi wetu ndio tunapata madhara haya maana hatuwezi kulipia hiyo elimu bora. tunaendelea kutanua lile duara la umasikini (poverty cycle)

the other day Masaki I trust you red about mwl Hassani wa huko sijui Rufiji
bado najaribu kufikiria future ya wale watoto baada ya elimu wanayopat
aaaaaaaaaaaahhhh bwana wee ngoja tuendelee kuwa mzoga unaotembea....

Mbaya zaidi watu ambao ni ''greedy'' wanatumia hiyo umasikini wa mali na mawazo wa Watanzania kama mtaji wa kisiasa! Yaani kuwatoa Watanzaia kwenye lindi la umasikini kutamaanisha kuwa na ugumu kwenye kuwadanganya wakati wa kampeni!

Taifa hili linahitaji maombi! Aliyetunga wimbo wa taifa letu aliona mbali, maana tunaishi kwa kudra za Mungu tu!
 
mbaya zaidi watu ambao ni ''greedy'' wanatumia hiyo umasikini wa mali na mawazo wa watanzania kama mtaji wa kisiasa! Yaani kuwatoa watanzaia kwenye lindi la umasikini kutamaanisha kuwa na ugumu kwenye kuwadanganya wakati wa kampeni!

taifa hili linahitaji maombi! Aliyetunga wimbo wa taifa letu aliona mbali, maana tunaishi kwa kudra za mungu tu!

am kinda tired.....................
 
We F1 ulisoma st.? si ulisoma kwa kina Kayumba?
Tatizo wazazi wengi wanawapeleka watoto wao st. alafu huku kwa kina Kayumba wanakufumbia macho na hawakupi msisitizo bora yeisheeeeeeeee ndo hapo chacha tutakuwa na taifa mbumbumbu miaka 20 ijayo.

Sasa sisi tusio na uwezo Fide wakwetu ndo hawa wameambulia zero na IV...........
mweeee, ishirini mingi!!!!!!!!!!!
 
FL1, Asante kwa kuliona hilo tatizo. Hili ni tatizo sugu litakalosumbua taifa kwa sasa na kizazi kijacho. Nakumbuka kuna usemi wa baba wa taifa usemao - (mtanzania bado hana elimu mbadala ya kuchimba madini, tuyawache huku chini maana hayaozi na wakati ukifika mtanzania mwenyewe atayachimba wakati akiwa na hio elimu ) Hapa nazungumzia elimu ambayo mpaka sasa mtanzania hana na serikali imelifumbia macho swala hili la elimu. Mkazo wa kujenga shule za kata pasipo na walimu wenye taaluma ya kutosha ina maana gani ?? unakua na ( majengo + wanafunzi + walimu voda fasta tena wawili shule nzima = uwiiiiiiiii sifuri ) Serikali lazima ibadilike kuhusu suala la elimu, mtanzania asipokua na elimu madhubuti ni kwamba taifa linaangamia !!! something has to be done somewhere hukoo mjengoni Do..
 
tatizo la kuyumba kielimu TZ lilianza pale serilaki ilipoanzisha mpango wa waalimu wa UPE. Sasa wasomi wengi ni wa kizazi cha UPE, hakika mpaka kizazi hiki kiishe ndio mambo yatatengamaa! Sumu ya upe bado inawatafuna baadhi ya watu! Sorry guys!
 
Nikianza kuwaza matokea mabaya ya watoto wetu yaliyopita ..sisi kama wazazi tumejifunza vip juu ya hili..
Naikumbuka sana elimu ya zamani waliyo soma mababu na baba zetu ..

Unaikumbuka we umekuwa bi Kidude? Tena unasema unaikumbuka sana...ati?

Anyway tuache utani tuwe serious sasa.....

''Mi watoto wangu wote wanne wanasoma International School of Ta....nanihii...naniliu...halafu ada kwa term ni USD 5,000 tu, siyo nyingi. kwa mwaka kila mmoja namgharimia zaidi ya USD 25,000 ambayo ni affordable.
Na wote wana bima ya afya Str.....naniliu. Wanapata First Class world class Education ndani ya Tanzanian Soil,.... nakumbuka wakati nikifanya kazi kama fundi umeme wa majumbani kule Athens ugenini nilikuwa nalipwa dola 25 kwa shift moja kwenye kampuni ya wagiriki nikiwa na watoto wawili kipindi hicho na sikuweza kuwasomesha vizuri........mjomba wangu akanipigia simu sikumoja na kuniambia amenitafutia kazi ya CEO kwenye kampuni moja Tanzania na wangenipa training ya mwezi mmoja ili niweze kazi.

Pamoja na wasiwasi niliokuwa nao nilipofika Tanzania nikakuta kumbe ukiwa m......ungu kama mimi na tena natokea Afrika kusini basi unakuwa CEO bila hata qualifications, ndiyo hivyo tena mwaka wangu wa xxxx sasa naula tu.'' siyo maneno ya akashube haya.... ni maneno tu ya wale jamaa ambao ukitoa Z unapata Mungu.

Yaani wa.....ungu.

Hivi First Lady kwa mapato yako wewe unaiweza hiyo ya CEO huyu wa kiafrikaan aliyekuwa mbeba box ugiriki??? Au wewe kama mimi shule ziko nchini lakini unazitazama kama mbingu vile...wanaenda watoto wa wa.....ungu tu.
 
Back
Top Bottom