Hivi tunakosa basic decency kabisa jamani?

Pundit,

Ukosefu wa maadili miongoni mwa jamii yetu unachangiwa sana na uovu huu mbaya unoendelea sasa. Science na teke linalokujia ndiyo ame acceralate uovu huu. Watu wanshindwa kuitumia hii fulsa ya kuwa na Mtandao na kuanza kuitumia kwa nia isiyokusudiwa kabisa. Lakini haya tufanyeje maana mtu huyu anayefanya haya ni jibaba au jimama lizima kabisa na heshima zake nyingi tena linaaminiwa mpaka linafanya kazi nyeti za benki. WanaJF yafaa kujua kuwa Ibilisi anatumia watu bila kujali wadhifa, heshima wala umuhimu wake kwa jamii. Hizi ni kazi za ibilisi kuanzia yule anayekubali kupigwa picha akiwa uchi mpaka kwa yule anayesambaza na kufurahia. Kwani wapo watu wanaofurahia kupigwa picha wakiwa uchi na wakifurahi picha zao kusambazwa ktk mitandao. Lakini pia fulsa hiyo pia imetumika kama kukomoana miongoni mwetu na hizi ni kazi za Ibilisi zote, na hawa watu wanaofanya hivyo ni agent wa ibilisi.

Hii kuikabili ni ngumu kwa hali ya kawaida bali ni kwa wahusika kujithamini wao kuwa wameumbwa kwa mfano wa Mungu hawatakiwi kuuzalilisha uumbaji wa Mungu. Na wale wanaodhalilisha wenzao kwa kusambaza picha hizi wajue wandhalilisha uumbaji wa Mungu. Wanatakiwa wajirudi waombe rehema mbele za Mungu ili awasamehe na kuacha kabisa biashara hiyo.
 
Hapo ni katika kuendelezea hiyo mienendo ambayo inarekebishwa na kina punch na hayo magazeti ya udaku. Tukiangalia kwa upande wa pili wanaume (most of them) ndio wana mienendo michafu na mibaya sana na wanahitaji huduma ya ziada ya kuwarekebisha iwe punch, magazeti ya udaku au hata kudhalilishwa kama wanavyofanya kuwadhalilisha hao wasichana.

Pengine hapa tutatofautiana. Mimi naamini hii tabia ya wote kujifanya viranja wa maadili ndiko kulikotufikisha hapa. Kwa nini mambo ya watu binafsi tusiwaachie wenyewe wamaliziane? Kama mtu unamuona ana mienendo mibaya, jitenge naye lakini usimpeleke kwenye jukwaa la umma! Mimi naamini sisi sote, hakuna aliye kamilika sasa kwa nini tuanze kuwahukumu wengine kabla ya kujihukumu wenyewe? What's good for the gander etc. etc. Kama mtu anajiona amekamilika basi heri amshukuru Mungu ili aweze kuendelea hivyo hivyo.
 
Pundit,

Ukosefu wa maadili miongoni mwa jamii yetu unachangiwa sana na uovu huu mbaya unoendelea sasa. Science na teke linalokujia ndiyo ame acceralate uovu huu. Watu wanshindwa kuitumia hii fulsa ya kuwa na Mtandao na kuanza kuitumia kwa nia isiyokusudiwa kabisa. Lakini haya tufanyeje maana mtu huyu anayefanya haya ni jibaba au jimama lizima kabisa na heshima zake nyingi tena linaaminiwa mpaka linafanya kazi nyeti za benki. WanaJF yafaa kujua kuwa Ibilisi anatumia watu bila kujali wadhifa, heshima wala umuhimu wake kwa jamii. Hizi ni kazi za ibilisi kuanzia yule anayekubali kupigwa picha akiwa uchi mpaka kwa yule anayesambaza na kufurahia. Kwani wapo watu wanaofurahia kupigwa picha wakiwa uchi na wakifurahi picha zao kusambazwa ktk mitandao. Lakini pia fulsa hiyo pia imetumika kama kukomoana miongoni mwetu na hizi ni kazi za Ibilisi zote, na hawa watu wanaofanya hivyo ni agent wa ibilisi.

Hii kuikabili ni ngumu kwa hali ya kawaida bali ni kwa wahusika kujithamini wao kuwa wameumbwa kwa mfano wa Mungu hawatakiwi kuuzalilisha uumbaji wa Mungu. Na wale wanaodhalilisha wenzao kwa kusambaza picha hizi wajue wandhalilisha uumbaji wa Mungu. Wanatakiwa wajirudi waombe rehema mbele za Mungu ili awasamehe na kuacha kabisa biashara hiyo.

Ufunuo,

You bring a very important point about the use of this double edged sword called technology.Kuna rafiki yangu baada ya kuwa addicted na mitandao ya picha ambazo hazisemeki aliapa kutoikaribia computer yenye internet zaidi ya kwa ajili ya kutuma email kwa sababu alishaona internet ni "shetani mkubwa"

Wakati huo huo wengine tunakuja hapa JF na kukata issues za kitaifa, wengine inawasaidia katika homework za shule na research za kazini, wengine inawakeep in touch na familia ndugu jamaa na marafiki.Kwa hiyo internet ni kama moto, unaweza kuutumia kusonga ugali ukala au unaweza kuutumia kuunguza nyumba, shauri yako mwenyewe.

Sasa ukiona mtu anatumia moto kuunguza nyumba that tells you more about the person than about moto.

Bottom line is we have to be careful out there, always associate with good peeps and keep away from dubious characters.And even then, certain exposures are a huge risk if you get my drif.
 
Mkuu Pundit

kwa kuwa JF tunaongea kwa uwazi, naomba uweke wazi jina ra huyo mtu ariyepiga picha na kuzisambaza. Hii ni adhabu ndogo tu compared na kumdharilisha huyo dada.

Naomba kuwakilisha.
 
sijaelewa unazungumzia kina nani hao wasio na heshima

Offcourse hao wanaosambaza huo upuuzi tena bila kuombwa wanadhani watu wote wanapenda kushabikia upumbavu wao. I am sorry i am so touched though sijaona hiyo email thats why nikashindwa kuweka wazi what i mean
 
Pundit you have a very valid concern which I support fully! Lakini bottom line lazima tufikirie mbali zaidi. Pundit, believe me you, huwezi kumbadilisha mtu kwa "maombi" ndo maana haya yoote unayoyasoma na kuyaandika humu wenzetu kwenye nchi zilizoendelea wameshayakubali kama part ya maisha yao. Na sisi ndo tunaiga huko (thanks to google!) Ndo maana Ngono, ufedhuli, hizo night club uchwara,nk ni part ya maisha ya wazungu, precisely kwa sababu walishagundua kwamba si rahisi kuwazuia watu kufanya watakavyo, after all ndo uhuru wenyewe huo (wameshahalalisha umalaya, strippers.. You know better..)

Sasa je nakubaliana na haya mambo? hapana. Kikubwa hapa ni kwamba nchi zetu za kimaskini hatuna budi kuwa na sheria na UWEZO wa kuzitekeleza. Kama tungeinvest katika utekelezaji wa sheria tungeweza kupambana na haya majanga, lakini kwa mwendo huu wa waungwana kama wewe na wengine kusisitiza maadili..no body cares or listens! Dunia imeshabadilika sana. Ulaya hata malaya anaithamini kazi yake na anathaminika! is it the same here in bongo? I dont know! binadamu ni kiumbe tofauti sana na ingawa tuko billion sita na ushee tunatofautiana kila mtu kivyake...

Hili swala ni gumu sana, wengi especially watawala wetu..wanakimbilia katika kivuli cha "maadili ya mwaafrika" This stament is just outdated and full of hypocricy. Kama mtu akifanya mambo kama hayo angekuwa anaweza kuface consequences za sheria..hali ingebadilika. Kifupi, all those vices you see in our country/Africa ni kwa sababu people knows kwamba kuna level katika maisha sheria haiwezi kukugusa.

So we have to identify our commonalities kama bianadamu na tu move on..kuna vitu hata kama ungevipigia kelele..you will hardly succeed! Its sad but you have to do the doables...kuwaomba watu wafuate maadili..its not the nature of human beings. Nani hajui kwamba kuiba ni vibaya? viongozi wanaingia maofisini kwa viapo vya misahafu...Its disguisting, but hili swala la maadili mimi nashindwa kulielewa na kibaya linatumika kwa convinience za mhusika...
 
Wikiendi hii nilienda kuwacheki masela, mabaharia na machizi basi hapo ndani ya Upper West Side ya Soweto, six degrees north of nowhere -ruptured from the fabric of spacetime continuum if you get my drift-.Si unajua tena kijua kinatoka watu hawachelewi ma barbq na matoto ya kikunjani kutoka UCT na Wit yameshuka, ilmuradi kuondoa machungu ya boxes and what not.Picha zinapatikana nitumie bank account number yako kwenye PM, lol!

Basi story story na wewe, overregulated watered down beers that taste like orange juice, political and social punditry, whats new in town, watoto wakali wako wapi and all that good stuff.

Mara si playa mmoja akaingia mtandaoni kutuonyesha picha za watoto wazuri za kwenye social networking sites and who is who for some of us hermits with networking challenges.

Basi mara playa akafungua email ikatokea picha kubwa unaambiwa, wenyewe wanaita TIGO aka bumper aka junk in the trunk liko kitandani mdada yuko kwenye kitanda anajivinjari huku akiangalia vituz kwenye laptop.

Basi mimi kwa utashi wa kirijali, almost by reflext action nikamuomba mshashi aniforwardie ile email.

Najuta najuta.Maaana wamempiga picha huyu mdada wakamuuua kisawa sawa.Naona vibaya kwa upande mmoja kuandika hivi kwa sababu inaweza ku fuel interest na akaendelea kuwa exposed, lakini kwa upande mwingine imenigusa nikashindwa kujizuia.Zamani kidogo nilishawahi ku forwardiwa picha nyingine ya jamaa aliyefumaniwa Tabata akakimbizwa barabarani utupu wa mnyama.

Ninachojiuliza ni hivi inakuwaje mpaka mtu ukaamua kumpiga picha binti wa watu, regardless ya yuko loose kiasi gani au mchafu kiasi gani, even if that is the case, how low does a man have to be to be involved in that kind of shyt? Yaani in some aspects hii exposure ni kama rape fulani hivi mbaya sana kwa sababu huyu dada wamemuandika mpaka anapofanya kazi na jina lake na familia yake yote.

I hope this rather emotional and uncharacteristic post of mine will appeal to those amongst us who entertained such barbaric tendencies to adopt a higher standard of morality and denounce all and any such overly chauvinistic, masochist and purely ignorant tactics.Kama unakorofishana na demu unamdrop tu, haina haja ya kumuumbua kama hivi kwenye mitandao, mwishowe unaweza kusikia kiumbe wa watu kajinywea midonge bure aikatishe safari yake hapa duniani.The same applies kama ni mademu mmechukuliana mabwana, inasikitisha sana kuona watu wanafanya entertainment katika uchafu na aibu ya mtu mwingine.

Halafu mpuuzi mwenyewe aliyeandika anafanya kazi benki ya Standard Chartered YA 1 Aldermanbury Square, kwa upuuzi wake jina lake lipo na hata hakuondoa lile li liability disclaimer reeefu.Nina uhakika email policy ya Standard Chartered hairuhusu kutumia baruapepe ya kazini kutuma chains za emails za derogatory obscene photos with malicious intent.Huyu mjinga siyo tu anaweza kufukuzwa kazi, bali pia anaweza kuface charges na hata kuwa involve Standard Chartered katika litigation isiyo na msingi.

Tujue kwamba unapopiga picha uwe na hakika kwamba hutaionea hiyo picha aibu hata kama itawekwa kwenye homepage ya google for all the world to see.

Tujue kwamba huwezi kumuamini mtu kirahisi hata kama ni boyfriend/girfriend, unaweza kuwa nae leo kesho ikawa blackmail na vendetta issue.

It is just not cool to expose people like this, everyone has a vulnerable point, admittedly some are more vulnerable than others but to prey on some chick's gullibility and then promote one's own masochistic or she-male chauvinistic tendencies (and then women say men are the opressing sex...) camouflaged in righteous and judgemental anti-promiscuity tone (whether the promiscuity is real or manufactured in a personal vendetta is not known and immaterial) may be argued to be lower than the alleged promiscuity itself.

I just felt like airing some people out.Now do not ask me for that email, for reasons stated above the distribution of such materials is just beneath me.

Vijana wengi tu wana mapicha ya aina hiyo. Tena ukijaribu kuwaelimisha wanakuona hufai na umeachwa na wakati. Na wengine wana CDs maofisini wakati wanachapa kitu kwenye komputa huwa wanaangalia watu wakifanya mapenzi machafu (mfano kinyume na maumbile) na wanaona ni sahihi kabisa.

Yaani, kuna vituko vingi sana katika jamii yetu inayotokana hasa na ujinga tu. Sasa sijui kama ndiyo maendeleo au kurudi nyuma? Kitu kingine sisi tunaotumia usafiri wa daladala tunasikia matusi yakitolewa na madereva, makondakta na mashabiki wao utafikiri hawa watu hawakuzaliwa na wanawake.

Siku moja kondakta mmoja alikuwa akimtukana mama fulani wa makamo hivi mpaka nikaona aibu. Kijana huyo alikuwa akimwambia huyo mama, "Kwani kati yangu na wewe nani mwenye muhogo: mimi, wewe?" Kwa jinsi huyo kijana alivyokuwa akiongea nilielewa alimaanisha 'mzee'. Sasa kweli huu ni ustaraabu kweli? Inabidi tubadilike katika mambo mengi sana: elimu, mtazamo, maadili, kuongea, kufikiri, nk.
 
Pundit, kwa kweli nakushukuru na kukupongeza kwa kuweza kulisema hilo bayana. Nakubaliana kabisa na wewe kwamba pamoja na mapungufu ya wahusika kwani hafanyi hayo mambo peke yake, bado haistahili kuyaweka hadharani ili kila mtu ayaone. Kuna njia nyingi za kuonya watu na si lazima kudhalilishana. Vilevile inawezekana ukafikiri unawakomoa wahusika/mhusika kumbe ukute wala haliwagusi/halimgusi. Matokeo yake unadhalilisha umma mwingine usiostahili.
Kwa wasiokubaliana na Pundit, siwezi kuwalazimisha wawe na maoni kama yake kwani binadamu tuna mitizamo tofauti. Lakini naamini idadi kubwa itakubaliana naye na hasa tukizingatia malezi katika jamii nyingi za kitanzania kwa upande wa mila na desturi na hata dini zetu.
 
Let them forward the email to us halafu tuwatrack then tuwafundishe adabu ili siku nyingine wasifanye utoto huo hasa hao wasiofanyakazi walizoajiriwa nazo!
 
Back
Top Bottom