Hivi tunajifunza nini katika uchaguzi mkuu huko zambia? Hasa tume ya uchaguzi kulinganisha na nec

KONDOO

Member
Jan 17, 2011
31
1
Afrika na viongozi wasioridhiki na wachoyo wakubali kwamba kuwa wimbi ya mabadiliko linavinjali hawawezi kuzuia kwa mkono.
 
Unahitaji watu wenye uelewa wa kutosha ili kufanikisha mabadiliko. Tanzania bado. WaTz wengi, wasomi kwa wasio wasomi, bado wanafikiri kwa kutumia matumbo yao na si kuhusu issues. Nafikiri tatizo kubwa ni elimu rojorojo au ukosefu wa elimu kabisa. Tazama Igunga. Ukitazama wanachama/mashabiki wa CCM ni choka mbaya lakini uwaelezi kitu kwa Magamba yao. Hali zao za maisha hawawezi kuzihusisha na aina ya utawala uliopo. Wape vikofia, vilemba na khanga kazi imekwisha. Ikishindikana hiyo (ni nadra) nunua shahada zao za mpiga kura na mwaga FFU umemaliza.
 
mungu akitaka ukombozi utafika tu broo

Tume huru ya uchaguzi kwa sasa ni muhimu kuliko hata katiba mpya tunayoililia. Bila tume huru nawahakikishia wapinzani hawatakaa waichukue ikulu hata kama watashinda kwenye sanduku la kura.
.
 
Ni swala la muda tu. Pamoja na elimu isiyo ya uhakika vijana wengi wanoipata elimu hiyo watachangamka mda si mrefu. Pongezi kwa rais Banda kwa kukubali matokeo. Kwa CCM ni somo ambalo ni gumu kulielewa lakini kwa vijana hawa wanaojazwa shule za kata muda ukifika somo litaeleweka.
 
Back
Top Bottom