Hivi tunajenga taifa la namna gani kwa vizazi vijavyo kama tunaacha misingi ya uzalendo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi tunajenga taifa la namna gani kwa vizazi vijavyo kama tunaacha misingi ya uzalendo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, Mar 3, 2011.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taifa letu limeanza kupoteza dira baada kuacha misingi alitufundisha Hayati baba wa taifa Mwl.Julius K. Nyerere.Ninasema hivi kwa sababu kama taifa halina vipaumbele vya kuliongoza taifa kila kiongozi anakuja na mambom yake ambayo anataka kuyafanya yawe yana maslahi kwa taifa au la.

  Katika hili napenda kuzungumzia suala la WIMBO WA TAIFA ambao ni alama mojawapo ya taifa letu pamoja na alama nyingine kama fedha,ngao ya taifa nk.Siku hizi ndugu zangu wimbo wa hautiliwi mkazo kuimbwa mashuleni kama ilivyokuwa siku za nyuma miaka ya 90.Ndugu zangu msishangae kuona siku hizi mwanafunzi anamaliza kidato cha nne hajui kuimba wa taifa wote.Na sehemu nyingine hata kama unaimbwa umekosa heshima yake kabisa.

  Kuna nyimbo nyingine kama "Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo" na nyingine ndo zimesahaulika kabisa na kuna baadhi ya walimu wa siku hizi hazijui nyimbo hizi.Nyimbo hizi zilikuwa zinajenga moyo wa kizalendo kwa wanafunzi.Nimezungumzia suala hili moja tu japo na mengine mengi tu ambayo tumeyaacha na kukimbilia utandawazi.Ndio maana nauliza ttunajena taifa la namna gani kama tunaacha misingi ya uzalendo kwa nchi yetu?

  Ndio maana nimetangulia kusema kama taifa halina vipaumbele vya kuongoza taifa letu basi taifa linakosa dira na kwenda tusikojua.Na hii yote nimkwa sababu ya kukosa viongozi wenye maono mema na taifa hili ndio maana kwa mfano tu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kila anayeingia anaenda na ya kwake matokeo yake tunaona kinachoendelea.

  Najua hapa jamvini kuna watu wana fikra pevu na mchango wenu ni wa muhimu sana ili kuona tunafanyaje ili kufanya mabadiliko na kujenga jamii iliyo na moyo wa uzalendo kwa taifa japo najua kwa upande mwingine kuna mambo mengi yamechingia kuondoka kwa moyo wa uzalendo kwa wananchi kama vile ufisadi, rushwa zilizokithiri, uonevu, ugumu wa maisha pamoja na mambo mengine mengi tu ambayo sijayataja hapa.

  Naomba kutoa hoja.
  " IF YOU WANT TO KILL A NATION YOU JUST DISTRUCT THE EDUCATION SYSTEM"
   
Loading...