Hivi tuna Jaji Mkuu na Mahakama nchi hii! Mbona Rais anavunja sheria hivi?

Unajua watu walizoea miteremko kila mahali, Rais Magufuli kaleta heshima za mifumo ukosoaji ndio unaanza? Naomba muelewe mfumo umeshabadilika, kamwe hatuwezi kurudia Madudu ya zamani
Tunazungumzia mfumo wa mahakama kuingiliwa wewe unasema ishu za jiwe kuleta heshima!! Akyanani bao potevu
 
Hayo yote muarobaini wake ni katiba mpyaa ambayo itakata kabisa mizizi yote inayomuwezesha Raisi kuwa na nguvu ya kuingilia mihimili mingine.

-Tunahitaji kuwa na judicial independence
-Tunahitaji kuwa na parliamentary independence
-Tunahitaji kuwa na Executive body itakayokuwa na mipaka kwenye majukumu yake.

Jamani tudaini katiba mpyaa vinginevyo tutaendelea kulia lia hivi hivi mpaka Yesu anarudi atatukuta bado tunalia lia tu.
 
Mkuu unakumbuka kuwa Bw Yule alishasema yeye ndiye anaewateua na yeye ndiye anaewalipa mishahara na kuwapatia Magari? Je umesahau vitisho dhidi yao? Kwa ujumla Nchi yetu imeoza na hatuna wakutusafishia bali ni sisi wenyewe.
Tufanye nn basi? Kila mmoja wetu atafute jibu.
Katiba mpyaa ndio sululisho la kitu.

Let's rescue our country from dispair through New constitution.
 
Unajua watu walizoea miteremko kila mahali, Rais Magufuli kaleta heshima za mifumo ukosoaji ndio unaanza? Naomba muelewe mfumo umeshabadilika, kamwe hatuwezi kurudia Madudu ya zamani
Ni mfumo wa nini huo uliobadilisha na ameubadilishaje?

Ametutoa kwenye demokrasia na kutupeleka kwenye monarchy au?
 
Wabongo watalalamika humu mitandaoni halafu wataacha kama ilivyo na issue nzima inaishia mitandaoni ila hutaona wakifanya kitu chochote kuonesha kilichofanyika si sawa na watanzania si wajinga,yani hata ukiona tunaandama basi mpaka wahusike wanasiasa tena pale mambo yao yanapoguswa. Akili zetu tumekabizi kwa wanasiasa na ndiyo wanye kutuamulia kila kitu sie wenyewe hatuna makali yeyote.
 
Hahahahahahahaha..
But Mkuu nakumbuka sana ulivyomremba huyu Jaji Mkuu Prof Juma baada ya uteuzi wake kuthibitishwa..
Nakumbuka kwenye ule Uzi wako ukisema sasa Judiciary imepata mtu madhubuti..
Kumbe lahaula..!!!
Tupia hapa ule uzi Mkuu Paskali.
P
 
Kiukweli mihimili ya bunge na mahakama hapa kwetu ni dhaifu sana, ndo maana rais anafanya chochote awezacho na atakacho.kweli rais anapanga hata muda Wa kutoa watuhumiwa toka mahabusu, kwanini Rais asingesubiri wahukumiwe na mahakama kisha awatoe kwa msamaha wake kama katiba inavyotaka?

Nawashauri wabunge Wa upinzani waanzishe mchakato Wa kumshitaki rais kupitia bunge hata kama huko mbeleni watashindwa kupitia mchakato huo bungeni.

Wafanye hivo kwa sababu ya rais kavunja katiba yetu Na kushindwa kusimamia kiapo chake.wakifanya hivo watakumbukwa Na taifa letu huko mbeleni.
Watamshatki vipi kupitia bunge, yaani bunge hili ambalo amelitia mfukoni na yeye ndio analiamulia nini cha kujadili?

Unachokisema ni sawa na kumpiga mwanao sasa hivi halafu baadae aje alete mashtaka kwako wewe huyo huyo ambaye umempiga akitegemea kwamba utajiadhibu.

Kiufupi hiki unachokisema hakiwezi kusaidia chochote, na kwanza hata kabla ya kuanza kumjadili anaweza akavunja bunge.

Tatizo ni katiba tunayotumia
 
Suluhisho la kudumu na litakaloirejesha nchi kwenye mstari mnyoofu na wa heshima ni PEOPLES REVOLUTION. MAPINDUZI YA UMA.

Haya mapinduzi yanapaswa yaanzishwe na raia kwa dhati kabisa bila kujali gharama zake.

Kwa mfumo huu, hakuna mabadiliko yatakayoshuka kutoka kwa wanasiasa wanaopigania matumbo yao.

Ila naamini, IPO SIKU watu wataamua na watawala watasikiliza.
Alafu tumuweke nani?
 
Acheni kuwahusisha wasukuma na huo ujinga mnatukera sana ambao hatumuungi mkono huyo jiwe wenu.

Unazungumzia bia tatu kwa wasukuma sisi huwa tunanunua kreti nzima ikiisha tunaongeza tena mpaka ziishe bar na pesa za kufanyiwa hivyo tunazo

Mchukieni jiwe ila msituhusishe wasukuma na huo ujinga wa jiwe.
Hoja zakitoto sana hizi
unajua tukisema tunaambiwa ni ukabila , lakini Tabia ya msukuma hata akinunua bia 3 tu atataka dunia nzima ijue kwamba anatwanga bia bar fulani .
 
Wabongo watalalamika humu mitandaoni halafu wataacha kama ilivyo na isdie nzima inaishia mitandaoni ila hutaona wakifanya kitu chochote kuonesha kilichofanyika si sawa na watanzania si wajinga,yani hata ukiona tunaandama basi mpaka wahusike wanasiasa tena pale mambo yao yanapoguswa. Akili zetu tumekabizi kwa wanasiasa na ndiyo wanye kutuamulia kila kitu sie wenyewe hatuna makali yeyote.
We need to make a huge sacrifice for changes!! No changes come easily it always comes with bloodshed.
 
Nchi hii mtu anaweza kujiandikia kitu tu kutoka kichwani kwake, mara paap; jamii nzima inafuata mtazamo huo.

Ukiachana na maswali ya moral aspects za huu msamaha hivi ni sheria gani ya nchi raisi anavunja kwa kushauri DPP achukue a different approach?

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria kwa kusikiliza kesi na kutoa haki, hila sio ku-enforce Law.

Jukumu la ku enforce sheria ni kazi ya polisi, TAKUKURU, etc to do with institutions with legal powers to conduct policing work.

Kwenye kutafuta haki au tafsiri ya sheria, DPP kwa upande wa serikari ndio mshtaki mkuu kwa niaba yao, na anamamlaka ya kuamua kutoendelea na kesi muda wowote; mahakama aina mamlaka ya kulazimisha kesi isikilizwe mshtaki anapoamua kuifuta.

Sasa hapo raisi anavunja sheria gani? Walau basi mtu alete hiyo sheria sijui sehemu ya katiba anayotaka watu waamini raisi anavunja.
 
Hawa watu wanaoteuliwa wakadhani ni hisani badala ya kusimamia maslahi ya umma ni watu wasiojielewa.

Mbona CAG Assad alisimama kiume akalinda hadhi ya ofisi yake?
Precedence aloyoiweka Assad itaisaidia sana taasisi ya CAG miaka na miaka ijayo

Huyu Profesa Ibrahim vipi mbona mwepesi sana kushinda karatasi, hajiamini kuwa yeye ni jaji mkuu au kitu gani?
 
Hata kama unaye.
Unajua kateuliwa na nani?
Wana JF!

Nchi yetu ipo katika wakati mgumu sana tangu tupate uhuru.
Ni dhahiri utawala huu wa Magufuli umeamua kuingilia mhimili wa mahakama na mahakama yetu chini ya uongozi wa Jaji mkuu wa sasa inaonekana kuwa legelege mno kusimamia independence yake kitu ambacho kinaelekea kutufanya sisi wananchi tukose imani japo kiduchu iliyokuwa imebaki kwa chombo hiki.

Nchi hii ina Jaji mkuu ambaye dhamana kuu ya nafasi yake ni kuhakikisha chombo cha mahakama hakiingiliwi, hakinyang'anywi hadhi yake na kikubwa kabisa taratibu za kimahakama zinaheshimiwa.

Katika kipindi hiki cha utawala huu tumeona mahakama ikiingiliwa waziwazi kabisa lakini hatuoni Jaji Mkuu akisimama kidete kutetea hadhi na wajibu wa chombo hiki. kwa mfano

1.Tunaona mhimili wa serikali ukipeleka watu mahakamani, kuwafungulia kesi nzito za uhujumu uchumi, kisha wakati mwingine kuachana nazo bila maelezo yaliyonyooka huku watu wakiwa wameshasota rumande Je Jaji mkuu yuko wapi kuintervene katika mazingira kama haya?, Uko wapi muongozo wa mahakama katika kesi ambazo zinaletwa mahakamani bila ushahidi wa kutosha?

2.Tunaona leo Rais eti anashauri "Watuhumiwa wa makosa fulani waachiwe kwa kufanya kadha wa kadha", Halafu eti ushauri huo unaandaliwa siku maalum ya kuona umetekelezwa vipi, kisha mshauri anatoa siku nyingine saba ushauri wake huo utekelezwe!!, Hivi umewahi kuona wapi mshauri anatoa time limit ya ushauri wake kutekelezwa?

3. hivi karibuni pamekuwepo na kesi kadha wa kadha ambazo huhitaji kuwa genius kuona kuwa mhimili wa Serikali unaiendesha mahakama kwa remote control, Kesi ya Lissu na ishu ya Fatuma Karume. Kesi ya Lissu hakimu anadai hawezi kuingilia mhimili wa bunge, Ina maana Bunge lisipotenda haki mahakama haiwezi kulinda haki kwa ambaye hakutendewa haki?, Hii mahakama ya wapi inayojivua wajibu wake?, Si ni katiba ya nchi inayosema kuwa mahakama ndicho chombo kikuu cha utoaji haki nchini, sasa hii ya kutwambia wananchi kuwa mahakama ina hofu ya kuingilia bunge maana yake nini?.
Ishu ya Karume, sote tunajua kuwa hakupewa haki ya kusikilizwa, na kama tamko la TLS lilivyosema kwa precedence ya matukio ya nyuma mtuhumiwa wa makosa kama aliyoadhibiwa nayo Fatma hupaswa kusikilizwa ili haki itendeke maana hiyo kazi ndiyo kazi inayompatia rizki na pia kufanya kazi halali ni haki ya mtu kikatiba

4.Lakini pia wakati hayo yakiendelea kuna Masheikh wa uamsho wako Jela sasa tunakwenda mwaka wa tano, bado kesi yao inapigwa danadana, Je ni kweli mahakama imeshindwa kusimama hapa na kuiambia Serikali ilete kesi ya msingi dhidi ya wananchi hawa au la Iachane na kesi?, If there is no evindence it means it doesn't fit and if it doesnn't fit equit!!

Nchi hii ina Jaji mkuu, Je cheo chake ni ceremonial tu au ni Jaji mkuu kweli kweli wa kuhakikisha haki za wananchi katika kona za mahakama zinalindwa?

Kama Jaji mkuu ameshindwa kulinda haki za watu, na kama anaendelea kuona mienendo ya haki inaingiliwa na mhimili wa serikali huku akiangalia tu basi namshauri kuwa kabla wananchi hatujapoteza hako kachembe kadoogo sana ka imani juu ya mahakama basi pengine si vibaya akajiuzulu tu

HAKI HUINUA TAIFA BALI UDHALIMU NI AIBU YA WOTE!

Mheshimiwa JAJI Mkuu, Wananchi tunataka haki katika mahakama zako!
 
Kosa lake kubwa ni hilo lakumshauri DPP kujadiliana na Watuhumiwa namna ya kuipatia Serikali Mapato BILA kumahauri aharakishe upelelezi kwa Watuhumiwa ili Kesi yao ya Msingi iweze kuanza kusikilizwa. Baada ya hapo wale watakaodhibitika kutenda kosa basi wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

Sasa yeye kwa maana nyingine ameshawahukumu Watihumiwa wale na kuwapangia adhabu au walipe faini.
Je hilo wewe unaona ni sawa tu?
Nchi hii mtu anaweza kujiandikia kitu tu kutoka kichwani kwake, mara paap; jamii nzima inafuata mtazamo huo.

Ukiachana na maswali ya moral aspects za huu msamaha hivi ni sheria gani ya nchi raisi anavunja kwa kushauri DPP achukue a different approach?

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria kwa kusikiliza kesi na kutoa haki, hila sio ku-enforce Law.

Jukumu la ku enforce sheria ni kazi ya polisi, TAKUKURU, etc to do with institutions with legal powers to conduct policing work.

Kwenye kutafuta haki au tafsiri ya sheria, DPP kwa upande wa serikari ndio mshtaki mkuu kwa niaba ya serikari na anamamlaka ya kuamua kutoendelea na kesi muda wowote; mahakama aina mamlaka ya kulazimisha kesi lazima isikilizwe mshtaki anapoamua kuifuta.

Sasa hapo raisi anavunja sheria gani? Walau basi mtu alete hiyo sheria sijui sehemu ya katiba anayotaka watu waamini raisi anavunja.
 
Ni mfumo wa nini huo uliobadilisha na ameubadilishaje?

Ametutoa kwenye demokrasia na kutupeleka kwenye monarchy au?

Awamu ya nne walikua wakisema ukiwatoa wenye vyeti feki utawalipa pesa nyingi, Awamu ya tano imerekebisha na maisha yanaendelea
 
Back
Top Bottom