Hivi Tulishawahi Kujiuliza kwa nini Watanzania ni maskini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Tulishawahi Kujiuliza kwa nini Watanzania ni maskini??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lord, Feb 18, 2011.

 1. Lord

  Lord Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna jambo lilikuwa likinisumbua kwa muda mrefu sasa kutaka kujua kwa nini sisi ni masikini wa kutupwa japo tumejaliwa kila aina ya nyenzo ya kutufanya tusiwe masikini. Sikupata majibu ya maswali yangu mpaka hivi juzi tu ndipo nimepata hayo majibu. Nilijiuliza swali dogo moja baada ya kuona mapinduzi ya wananchi wa Tunisia na Misri. Iweje hawa watu wa Misri na Tunisia mbali na uzuri na utajiri wa nchi zao unaoonekana kwenye TV leo wapoteze muda wao kuandamana eti hali ya maisha ni ngumu?? Ugumu upi wanaouona hawa jamaa? Au wameamua kumkufuru mungu tu? Hivi wana ugumu wa maisha kuzidi sisi Tanzania? Hapana nakataa. Hawana ugumu wa maisha kiasi cha kutufikia sie. Hawa wenzetu wametuacha mbali saana...
  Swali lingine likaja sasa wanasumbukia nini kuandamana wakati sie wenzao huku wala hatufikirii hilo jambo maana kila kitu ni shwari huku kwetu? Hapa ndo nikajua kwa nini Watanzania tu masikini
  1. Hatuna/Tumekosa moyo wa kuthubutu kutenda na kusema yaliyo na manufaa kwa taifa letu. Kwetu siye mbuzi hula kufuatana na urefu wa kamba yake. Na ndio maana basi hata kitokee nini mara zote tumekuwa waoga na wabinafsi kutetea maslahi ya umma. Leo hii tuna kila sababu ya kuwawajibisha watawala lakini hatutafanya hivyo na kamwe haitatokea labda mpaka kizazi chetu hiki kife. Tumeshuhudia kupanda kwa bei ya bidhaa, tumeshuhudia uzembe ulivyoua wenzetu lakini hayupo wa kumfunga paka kengele.
  2. Wengi wetu ni wanafiki ambao wapo tayari kuuza heshima na uwezo wao ili mradi apate fedha wakati jamii kubwa ikihangaika. Hapa nasema kama wakoloni wangekutana na kizazi hiki naapa hadi leo wangetutawala. Wazee wetu walithubutu kwa damu na jasho wakatupa nchi huru. Leo hii tumetawaliwa tena na ndugu zetu wa damu. Labda ndo maana hatuwezi kuwatoa madarakani hata wakikosea vipi??
  Tunahitaji kufanywa nini na hawa watawala waovu ndo tuone tumeonewa zaidi??? Shime watanzania hii nchi ni yetu sisi na watoto wetu. Nini tunawachia watoto na wajukuu zetu?? Mashimo yasiyo na madini? Nchi isiyo na rasilimali? Au tunawaachia nini hawa watakaotufuata??
  Tunahitaji kuonewa kwa kiasi gani mpaka ndio tuseme imetosha sasa??
  Wakati ni huu Tutafakari....
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Jibu ni rahisi tu sisi ni maskini kwa sababu ya UJINGA wetu
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  aaaaaaah!tumelemewa na welevu wetu
   
Loading...