Hivi tukimuomba muumba wetu hawezi kutusaidia kuwang'oa wanaotudhulumu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi tukimuomba muumba wetu hawezi kutusaidia kuwang'oa wanaotudhulumu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by khayanda, Dec 24, 2010.

 1. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni nchi nzuri ambayo viongozi wake wamekazania kuiharibu kwa makusudi. Tufunge na kuomba hawa watu wanotuharibia nchi yetu watahayari na kutuachia nchi yetu bila kutuachia matatizo makubwa ambayo yanaendelea kujijenga kila siku. Hawa watu hawana huruma na hawana aibu wala soni kama mfalme majuju. Tutafanyaje jamaniii?

  Nchi yoyote ambayo viongozi wenye dhamana ya kuhakikisha sheria zilizopo zinafanya kazi, wanakuwa wa kwanza kuzivunja, basi hakuna sheria itakayofanya kazi. Tunayoyaona kama ugawaji wa viwanja holela, wizi katika mabenk, mauaji ya hovyo, ni kwa vile viongozi wetu na walinzi wetu wa amani ndiyo wanaoongoza mauaji, wanachukua viwanja hovyo. Kuna mheshimiwa pamoja na kujiuzulu wadhifa wa uwaziri, amepewa eneo la Magereza Morogoro anajenga kitu chake. Nafuu hata aliyeteka eneo la wazi la pwani yetu.
  Tumwombe Mungu atusaidie kuwaadhibu hawa jamaa maana sisi wametushinda. Hatuwezi kugoma, hatuwezi kuandamana na wala kuwapiga. BASI TUTUMIE IBADA NA MAOMBI KWA DINI ZOTE
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ibada ni sawa lakini tunapashwa kufanya zaidi ya hayo. mungu usaidia wale wanaojisaidia. Mtu hawezi kukuibia akatumia utajiri huo kujenga mahekalu na kununua mashangingi wewe ukaendelea kushangilia tu ukiamini Mungu atakusaidia; angalau na wewe changia kwa kumzomea mwizi huyo popote apitapo, ataona haya. Nakumbuka BWM alikwishaanza kuogopa kukatiza mitaani.Hiyo ndiyo dawa
   
 3. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata ukikesha ukiomba itakuwa kazi bure kama wewe binafsi huchukui hatua madhubuti za kufanya uwezalo kupambana na hao viongozi dhalimu. Kila mtu ana wajibu wa kupinga uharibifu wa nchi hii. Hakuna mafanikio yanayopatikana kirahisi. 'Wadhungu" wana msemo "no free lunch". Lazima kuumia ili matunda yapatikane - tatizo wengi wetu tu waoga mno na huo ndio mtaji wa watawala. Wanajua hatuwezi kufanya kitu zaidi ya kulalamika chini ya uvungu wa kitanda!
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tukiomba Mungu ukumbuke na Mchungaji Slaa nae ataadhibiwa kwa kumzini mke wa mwenzake, bora tubaki tu hivihivi !

  May be, Tumuombee Prof Lipumba aongoze nchi hii, huyu anaonekana msafi na ni mtaalam, tuachane na mafisadi wengine
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  You can say better than this keep on trying.
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  you dont deserve to be a senior expert member, am surprised even those who cant think are senior expert members.
   
 7. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Usafi gani bwana, mbona wote tuna vinyesi tumbon. Ebo.
   
 8. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama tunataka Mungu atusaidie, lazima sisi wenyewe tukae sawa na Mungu kwanza,vinginevyo hatatusikiliza.We must change our ways.We are too evil.
   
 9. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu pamoja na kukuheshimu sana,lakini umekosea.Mungu hajasema popote kwamba anamsaidia mtu anayejisaidia mwenyewe.Hayo ni maneno ya mtaani yasiyo na msingi wa ki-Mungu kabisa.Mungu hahitaji msaada wa mwanadamu katika vendaji wake.Halafu vita vyetu si juu ya damu na nyama,bali juu ya falme na mamlaka.Kwa hiyo kuzomea kwa kuwa hakuna msingi wa ki-Mungu hakutasaidia sana.Dawa ni sisi sote kama watanzania kwa ujumla wetu kutubu,kuacha njia zetu mbaya na kuanza kuliitia jina la Bwana,vinginevyo tunaelekea kwenye uharibifu.Huu ndio ukweli whether you like it or not.
   
 10. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama tunataka Mungu awangoe lazima sisi wenyewe tukae sawa na Mungu kwanza,vinginevyo hatatusikiliza.We must change our ways.We are too evil.
   
 11. n

  nyantella JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  sisi wa-TZ watu wa ajabu kweli!!!!!!!!!

  Hivi mnakumbuka kabla ya uchaguzi wooooote tulienda kwenye nyumba za ibada kumuomba Mungu atusaidie tufanye uchaguzi kwa amani. Uchaguzi umefanyika na kumalizika kwa amani. Tuliombe Mungu atupatie viongozi, Mungu ametupa viongozi. Ma-Askofu (wakiwamo wakatoliki) na ma Ma-Sheikh wakashiriki kumuapisha Rais. Nashangaa kuona jinsi Ma-Askofu hao hao wanavyoongea kwa chuki kuhusu serikali!! Hivi wakati Tunaomba mlitwambia lazima Mungu amchague Slaa? kuna mmoja anachukizwa na magari ya fahari ya serikali, kwani yameanza leo? mbona zamani kulikuwapo Rolls Royce pale Ikulu? je wanajua bei ya RollS! and I tell you wakati ulehali ilikua mbaya kuliko leo. where were they then kulaani???

  Sote tulimuomba Mungu and ametupa serikali sasa kama tulikuwa tuna mdhihaki then atajua cha kufanya nasi. Besides kama kuna mafisadi serikalini sii lazima kwamba woote ni mafisadi kuna watu waaadilifu wengi tu tusiwakatishe tamaa. tuwasidie kusalvage whatever we can and together we shall overcome the rotes!!
   
Loading...