Hivi tukiachana na siasa, Twaweza walishawahi kufanya utafiti gani mwingine ?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Tangu nianze kuifahamu hii tasisi miaka iliyopita "kila nikipowasikia twaweza wao utafiti wao ni wa kisiasa.

Na tafiti nyingi ninazozisikia kila siku ni mgombea gani au ni mwanasiasa gani anayekubalika kwa wananchi?

Hivi tukiachana na siasa hivi utafiti upi mwingine ulishawahi kufanywa tasisi ya TWAWEZA?
 
Nadhani wakulima wa nyanya Morogoro, zile zilikuwa zinaliwa na ng'ombe wakaharisha
 
Wanaangalia akili zetu, siku tukizipuuzia siasa wataacha tu. Tuwe busy na mambo ya msingi, tuachane na majitu ya porojo kila kukicha.
 
Ndio kitendo chenye pesa Tanzania.Siasa inalipa hata kipindi hiki cha njaa.Waache wajikombe ili maisha yao yaende!
 
Achana na Fundings za Twaweza Mkuu, utajikuta ukipatwa na magonjwa ya tabia.

Hiki ni kikundi cha watu wachache wanaotumika kisiasa na chama tawala kwa Maslahi ya matumbo yao na si vinginevyo.

Tafiti zao ni kwa ajili ya kuifurahisha chama tawala na si vinginevyo.Hawana tofauti na hii tume iliyokusanya ripoti ya Makinikia.

They are differ in objectives but the essense is the same.

[HASHTAG]#PressFreedom[/HASHTAG] [HASHTAG]#UhuruWaHabari[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom